Tanzania bado nchi masikini sana, kwa miaka 8 watanzania wameagiza magari 561,875

Tanzania bado nchi masikini sana, kwa miaka 8 watanzania wameagiza magari 561,875

Mengi sana
Avg ya magari 180 kwa siku kuingia ni mengi sana

Bajaj, guta piki piki piki no D yao imeanza mwaka Jana mwishoni Hadi Sasa imeshafika DL

Kwenye magari ilichukua miaka minne kufika DL
Mkuu nashukuru sana kwa kunikumbusha. Basi magari hesabu zitashuka zaidi na kua 517,824 kwa miaka 8 sawa na gari 64,728 kwa mwaka sawa na 5,392 kwa mwezi sawa na gari 180 kwa siku. Hatari sana.
 
Ivi namba D mwisho mwaka huu ..kwa hiyo kuanzia mwakani tutegemee namba E siyo?! Na gari ya mwaka 2000 au 2010 kushuka chini inaweza kuwa namba D kweli?
Hata combi ya 1957 inaeza kuwa no E kabisa ni usajili tu
 
Unaonaje muasisi wa jf Maxence Melo ukianzisha mchakato wa kuchangisha japo tsh elfu 2 kwa mwezi kwa kila member wa Jf, na kusaidia kutununulia magari wale tusiyonayo ili kuongeza uagizaji na pia kupunguza umaskini wa watanzania?

cc Maxence Melo
Kwaio hela ya kununua gari haipo je service ya gari, mafuta, bima ya gari nayo tutachangishana humu?
 
Kwaio hela ya kununua gari haipo je service ya gari, mafuta, bima ya gari nayo tutachangishana humu?
Hilo ni wazo tu mkuu.
Likipitushwa manaake ni kwamba utaratibu, vigezo na masharti vitawekwa.

Hivi zaidi ya kutuma na kuchangia post, JF ina program gani nyingine kwa jamii na kwa members?

Mi nadhani tunaweza kufanya zaidi!
 
Hii ni kwasababu gari serikali imeifanya kama luxury commodity,kodi inakaribia nusu ya bei ya gari...gari inauzwa Japan/UK kiasi cha $3000 hadi ifike Dar port yaweza kua $3500 ila sasa kuitoa hapo uwenayo mkononi kodi inaweza kua hadi $2500 utashangaa ile gari utaipata kwa $6000 ....iyo kodi waipunguze kwa nusu ili watu waagize magari kwa wingi pesa watapata tu kupitia kuuza mafuta,vipuri,parking kwenye maeneo ya manispaa nk ...
Gari kwa sasa ni kama tu simu ,pikipiki sio usafiri rasmi mana risk yake ni kubwa sana na ndio imekua kama usafiri rasmi sasa
 
Kodi inazidi bei ya ununuzi. Hongereni TRA , ACHA tuendelee kutumia magari mabovu
 
Attachments

  • 20220814_222534.jpg
    20220814_222534.jpg
    211.8 KB · Views: 9
Usivyo na akili huwezi kuelewa kua 999-100 ni 899.

Hesabu ndogo hivyo nayo inakushinda sasa utaweza kujadiliana na watu humu ukaelewa hoja zao?
Ulivyosema hapo kuwa namba zinaishia 899 ndio hapo ambapo haikuwa sawa kwa mana ya registration namba, ila kwa idadi ni sawa kusema hivyo, kumbuka ulivyosema.mwisho wa namba za usajili ni 899 hapo ndio kauli tuliyopingana na wewe.

Halafu kuwa na akili au kutokuwanazo ni huku mtaani ndio kunatupa heshima na si humu kila mtu mjuaji yeye amesoma sana ana mali na maisha mazuri ila tukikutana mtaani ndio kwenye heshima ya ukweli.
 
Hivi zinaanzia 100 au 101 hadi 999? Just asking.
101 -999 hapo inaanza moja kwenye 01 kutoka 01-999 hapo kama ni DMA inaisha ukianza DMB 101-999 inaisha tena inafata DME.
 
Wakati namba D ikielekea kuisha tujikumbushe idadi ya magari yaliyoagizwa chini ya namba D.

Kwa mfano, Namba T100DAA, ili kubadilika na kua T100DAB inahitajika magari 899, herufi ziko 25 kutoa herufi I. Hivyo kubadili herufi moja inahitajika magari 899 mara herufi 25 unapata magari 22,475.

Kubadili kabisa herufi kutoka DAA kwenda EAA inahitaji magari 22,475x25 sawa ma magari 561,875. Kwa maana kwamba kwa namba D ambayo imeanza mwaka 2014 na inaisha mwaka 2022 ni miaka 8 Tanzania imeagiza magari 561,875.

Kwa maana kwamba kwa mwaka Tanzania wastani tunaagiza magari 70,234 ama magari 5,852 kwa mwezi sawa na magari 195 kwa siku.

Hii ina maana kwamba kwa wastani wa watu milioni 60, milioni 30 ikiwa ni nguvu kazi tunaagiza gari 5,852 kwa mwezi ni ishara ya umasikini mkubwa sana.

Mbaya zaidi magari hayo 95% ni second hand ya miaka mingi. Ukiangalia Watanzania wanaagiza magari ya mwaka 2000 hadi 2008. Hayo ni ya kutembelea, ya usafiri kama daladala ni ya kuanzia mwaka 1995 hadi 2000.

Magari ya kuanzia 2010 Tanzania ni ya kutafuta kwa tochi. Serikali pekee na watanzania wachache sana wanaagiza magari ya kuanzia 2018 na kuendelea.

Mimi mwenyewe kimkweche changu ni cha mwaka 1999 niko vidudu[emoji23]. Aibu ya mwaka.

Hii nchi miaka 62 ya uhuru bado ni maskini wa kutupwa. CCM imenajisi hii nchi kwa kiwango kisicho na mfano.
Nenda Masaki uzaona utajiri wa watanzani.
 
Wakati namba D ikielekea kuisha tujikumbushe idadi ya magari yaliyoagizwa chini ya namba D.

Kwa mfano, Namba T100DAA, ili kubadilika na kua T100DAB inahitajika magari 899, herufi ziko 25 kutoa herufi I. Hivyo kubadili herufi moja inahitajika magari 899 mara herufi 25 unapata magari 22,475.

Kubadili kabisa herufi kutoka DAA kwenda EAA inahitaji magari 22,475x25 sawa ma magari 561,875. Kwa maana kwamba kwa namba D ambayo imeanza mwaka 2014 na inaisha mwaka 2022 ni miaka 8 Tanzania imeagiza magari 561,875.

Kwa maana kwamba kwa mwaka Tanzania wastani tunaagiza magari 70,234 ama magari 5,852 kwa mwezi sawa na magari 195 kwa siku.

Hii ina maana kwamba kwa wastani wa watu milioni 60, milioni 30 ikiwa ni nguvu kazi tunaagiza gari 5,852 kwa mwezi ni ishara ya umasikini mkubwa sana.

Mbaya zaidi magari hayo 95% ni second hand ya miaka mingi. Ukiangalia Watanzania wanaagiza magari ya mwaka 2000 hadi 2008. Hayo ni ya kutembelea, ya usafiri kama daladala ni ya kuanzia mwaka 1995 hadi 2000.

Magari ya kuanzia 2010 Tanzania ni ya kutafuta kwa tochi. Serikali pekee na watanzania wachache sana wanaagiza magari ya kuanzia 2018 na kuendelea.

Mimi mwenyewe kimkweche changu ni cha mwaka 1999 niko vidudu😂. Aibu ya mwaka.

Hii nchi miaka 62 ya uhuru bado ni maskini wa kutupwa. CCM imenajisi hii nchi kwa kiwango kisicho na mfano.
Nchi inanufaisha machawa ,Kupe na walamba asali vilaza flani hivi
 
Back
Top Bottom