Wilhelm Johnny
JF-Expert Member
- Jan 13, 2016
- 1,369
- 1,338
Wakuu mimi sio mtaalamu sana wa mambo ya siasa ila nilichokiona asubuhi wakati naelekea kwenye mihangaiko yangu hapa jijini Dodoma mitaa ya Chang’ombe B, wanafunzi niliowaona ni wa Shule ya Msingi Chang’ombe B wakiwa wanachota maji ya mvua yaliyotuama barabarani yanatakribani wiki moja au mbili, yaani ni toka zile mvua zilipita Dodoma.
Nikasimama kuwauliza kwanini mnachota hayo, maji wakanijibu ni ya kunyeshea miti na kudekia. Kweli inamaana serikali inatoa mabilioni ya pesa kwenda Uturuki kwenye nchi iliyojitosheleza wanashindwa hata kuweka matanki ya maji angalau kwa huu mkoa wa kiserikali?
Hayo maji watoto wanashika ni na machafu mno, yaani nilitumia ubabe kuwafukuza hapo maana wanahatarisha maisha yao. Nikawasihi wakanawe ila nikakumbuka hata maji ya kudeki hakuna maji masafi, ya kunawa watatoa wapi?
Mchana watanunua kachori wakatiane na mikono wameshika maji taka, si magonjwa watoto wanaenda kufata mashuleni huko jamani?
YANAYOJIRI
Kuna mdau anamakasiriko hapo kanipa namba za mkurugenzi wa jiji la dodoma mimi bila hiyana nikasend picha whatsapp na location ya shule ilipo mkurugenzi akanijibu atafatilia pakifungwa Tanki nitawajulisha maana nipo karibu na shule