Tanzania Economic Freedom Advocacy (TEFA)

Safi sana mkuu, naunga mkono hoja. Ni vizuri haya mawazo yakiwafikia wenye mamlaka/watoa maamuzi.
 
Nyie mumeshajenga hicho kiwanda kuonesha mfano au mnabwabwaja ujinga wenu tuu?

View: https://x.com/MwananchiNews/status/1898077481002799233?t=XsZBteoG1S07nIRymVmsXw&s=19
 
Mwekezaji asijenge tu kiwanda cha kuchakata gesi asilia (natural gas refinery), bali ajenge na kiwanda cha petrochemical kwa pamoja.
 
Usitumie chatgpt kwenye kuwakilisha hoja tumia akili yako
NDUGU,

Hii si ChatGPT...

Ni koherensia ya Ufikirifu, Uono na Ufikirifu Mifumo.

Wewe kama mtu, una unaivu katika mafikara na udhanifu wako.

Humu wadau kadhaa wanaingilia kati mashauri na mitazamo yako kwa kheri lakini wewe kama mtu 'umejifungia kiakili' na kucheza mchezo wa kujihami--kujihami mno isivyolazima.

Si kila mtu anachangia kwenye nyuzi zako kwa kuwa wewe una nidhamu na adabu stahiki ya kimazungumzo--HAUNA!

Alhamdulillah, mashauri yako ni mbegu ya kuvutia watu makini--unawavutia wengi kwa ujuaji na unaivu wako pia.

Siyo Kesi kivile... Kwa kuwa Unasaidia wengine kufahamu mambo ilivyobora--wewe Je?

Ulijizima data kwenye hili:


Halafu tena:

NASHAURI, usiogope kupewa changamoto ya kile unachodhani 'UMEMALIZA KIMAWAZO NA UJUAJI' na kumbe, kwa wakati huu, unako kule kujua mambo kwa sehemu tu;

Na tena, ujumla wa shauri lako ni Utoto/Ujuvinali wa Kujiwazia Ubab' Kubwa kwa kule tu kujidhania eti Umeshika 'Bunduki fulani Kubwa';

Unaweza kujisahihisha, kwa kuwa bado una nafasi ya kujipanga na kujipangua kimawazo na utashi ili uwe ni mtu mwenye kujua ilivyobora.

Hakuna ubaya kuachana ni mienendo ya kijuvinali...

Je, Unataka 'Umimi katika Ujuaji-Juvinali' ama nidhamu bora ya kujiweka kiakili na adabu kwa ajili ya nasibu ya 'Tujuzane hata ikibidi kwa Kuleeana na Shauri Bora'?

... Amua mwenyewe.

Hmmm
 
We jamaa unaonekana ni mjuvi wa kiswahili
 
Sihitaji shauri wako ndugu kwa sababu haukunituma kufanya hichi nachofanya
 
Kuanzia mwaka huu 2025 mwezi march hatutakubali kuendelea kuburuzwa maji shida, umeme haueleweki, huduma za kijamii mbovu safari hii hatukubali tena tutagawana fito.
 
Serikali itafute wawekezaji wazalishe zaidi ya megawatts laki moja (100,000+) za umeme kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vilivyopo nchini.
 
Shule za msingi za serikali kuongeza wigo wa masomo ya kingereza (english) na kuwa matatu nayo ni kingereza, hesabu kwa kingereza na science kwa kingereza huku kiswahili kikifundishwa masomo mawili kiswahili na uraia-hii haitawaacha nyuma watoto wa kimaskin kama ilivyo sasa kwamba kuna watoto wanamaliza msingi wakiwa na msingi mzuri wa lugha ya kingereza huku wengine wakiwa na msingi mbovu wa lugha ya kingereza na mitihani iwe sawa kwa shule za msingi za serikali na binafsi ambazo sio za kimataifa.
 
KILA NINAPOWAZA KUTOKA JAMII FORUM, HUWA MUNGU ANANIKUTANISHA NA MADINI KAMA HAYO...YAANI HAPA HAMNA MAWAZO YA CHAWAA.. SAFII SANA, TENA SANA..
taasisi ya urais iwe inabeba mawazo kama hayo, iachane kutafuta real ID, BALI IBEBE MAWAZO TU YANATOSHA.
 
Serikali kutonunua magari ya kifahari kwa wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi na budget hio kuielekeza sehemu zenye uhitaji.
 
Unit moja ya maji kuuzwa sh 400 mpaka 500
kupiga marufuku wale wanaouza maji na magari mitaani
 
Huduma za dialysis ziwe bure asilimia 100 kwa kila wilaya nchi nzima kwenye hospital za serikali
 
VETA itakuwa na umuhimu kama tutakua na viwanda vingi tofauti na hapo ni uongo sababu hata sahivi tuna watu wengi wamesoma VETA na hawana kazi viongozi waache kutumia shortcut na kauli nyepesi nyepesi ambazo sio na msaada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…