Kha! Kama haujajua basi humu ndio kwenyewe ambapo unapaswa kutumia ili kubaini hisia za Watanzania, unajua nyie desturi yenu ilivyo, sio watu wawazi, nahisi ni kwa ajili ya mfumo wa ujamaa. Maana Mtanzania kuachia kilicho moyoni mwake ni jambo nadra sana, nimeishi na nyie na nililiona sana hili.
Ni tofauti sana jinsi tulivyo huku kwetu, Wakenya tumezeoea kuambiana kama ilivyo, yaani haturembi wala kukupaka kwa mgongo wa chupa, unaambiwa ilivyo na ulivyo!! Umeze, uteme, upasuke, utokwe povu utajua mwenyewe, sasa mara yangu ya kwanza kuishi Tanzania nilishangaa watu wakarimu, wanaamkiana kwa maneno matamu, wanaitana 'mkuu', yaani nikahisi dah huku ndiko binadamu walipo.
Lakini muda ulipokwenda nikawa nawaona kwa rangi yenu yenyewe, kwamba Mtanzania atakusifia, na kuonyesha ukarimu sana wakati mpo naye, ila ukiondoka atakusema mpaka basi. Watu huko wamelea majungu, wanaishi kwa hasira za ndani kwa ndani, wengine hata wanahujumiana.
Sasa kwa mtandao kama huu wa JF, ndio wanapata fursa ya kuyasema maana wamejificha nyuma ya ID zao, mtaani anacheka lakini akipata fursa ya kuandika kwa simu, atatiririka maneno humu balaa.
Nilikua naona mameneja wa Kitz wakipata wakati mgumu sana, anashindwa kumuwajibisha Mtanzania maana hataki aonekane mbaya, ndio maana makampuni yenu huajiri mameneja Wakenya na wageni wengine, maana Mkenya hata kama rafiki wako wa karibu, ila ukiboronga na kuzingua kazini anakubadilikia papo hapo.