Kazi ya serikali ni kujenga capacity, uwezo, mazingira, ngazi, kuwazesha watu kujiinua, kuinuka.
Serikali makini inafanya hivi
1Afya. kuwa na huduma za afya nzuri kwa wote ni muhimu sana. tunazaliwa hospitalini, wote tukiumwa, ajali tunaenda hospitalini, mwisho wetu wengi tunakuwa hospitalini.
2. Elimu. (Elimu bure) ni kitu muhimu sana watoto zaidi ya milioni 10 kwa miaka mitano wameenda shule. Maisha yao, upeo wao, uwezo wao wa kufikiri umebadirika na kubadilishwa na elimu. Bila elimu tusingejua kusoma na kuaandika chochote hata hapa JF, simu yako usingeweza kuitumia.
3. Utawala wa sheria, kupinga rushwa ukiritimba, kusisitiza uwajibikaji,kupunguza kodi zai ili kuwezesha biashara kushamiri.
4. Miundombinu:- Muhimu sana kwa kila kitu. Mfano kutoa mazao yako kijijini kuuza mjini, nchi jirani, Ulaya, Duniani. Kwenda kazini, kurudi nyumbani, kufanya biashara zako. Ukiumwa, ajali kwenda, kuwahi hospitali ili kuokoa maisha yako. Kwenda shule, kununua chakula kwa bei rafiki, biashara zote kukua, kuongeza kodi za serikali.
Maisha yote ya binadamu yanajengwa, kila kitu kinajengwa na kuwezeshwa kwanza na juu ya miundombinu.
Kwahiyo serikali yoyote makini itawapa wananchi wake wote elimu bure, bima za afya rafiki, itawapa umeme, maji bila kuleta sababu za kipuuzi eti kwanini haiwezi kufanya hivyo kila siku. Itajenga barabara, reli ya kasi utoe mazao yako kijijini uuze mjini, Duniani, kuiwezesha biashara yako, kilimo, wewe kufanya kazi, kukua, kustawi.
Sababu ukifanya hivi vitu watu watafanya biashara, kazi, export zitaongezeka, mapato ya nchi yatakua.
Automatically Wafanyakazi wa serikali watalipwa vizuri. Na wale wa sekta binafsi mshahara wao utaongezeka. Nchi itaenda uchumi wa kati, mkubwa.
Sasa kama umeme ni issue, tunarudi kwenye ujima taratibu hata kama tukiongeza mishahara kwa 100%.
Vitu vya msingi vitavyowasaidia na kuwainua wengi Watz tumeviacha. Hatuna muda navyo kabisa. Tunapiga siasa badala ya kuchapa kazi.