Tanzania haina mfumo wa vyama vingi vya siasa!

Tanzania haina mfumo wa vyama vingi vya siasa!

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
1,730
Reaction score
2,230
Hivi majuzi nilitakiwa nitoe maoni kuhusu miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania tangu 1992. Ni suala ambalo naulizwa mara nyingi ila majibu yangu hayazingatiwi au hupuuzwa, pamoja na ukweli au uhalisia wa hoja zangu.

Uhalisia ni kwamba Tanzania haina mfumo wa vyama vingi vya siasa na haujawahi kuwepo tangu hiyo 1992. Ila tuna "mfumo wa chama kimoja cha siasa" wenye vyama vingi vya siasa. Vyama vyote vimo ndani ya mfumo wa chama kimoja! Hata katiba inayotumika sasa ni ile iliyoundwa na chama kimoja 1977

Kipengele kinachoruhusu vyama vingi vya siasa kilichomekwa tu ndani ya katiba ya chama kimoja kinachotamalaki kila pembe. Hata serikali huitwa ya CCM, si taasisi ya umma!

CCM ni chama dola na kinadumu kwa kutegemea zaidi dola. Tunahitaji tuwe na katiba mpya inayoweka mfumo, mazingira au uwanja sawa wa vyama vingi vya siasa.

Nahitimisha kwa kusema tena katiba mpya ije sasa na kutoa haki kwa wote, pamoja na vyama vingi vya siasa.
 
Back
Top Bottom