Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Hivi bado hujajua kuwa utaratibu mpya wa kutoa mikopo ndio uliokiwezesha chuo cha Tumaini kuongeza idadi ya wanafunzi wake toka 200 mwaka 1997 hadi 8000 mwaka huu? Je hizi sio jitihada zinazostahili pongezi?
Wakati mwingine watanzania sijui tumelogwa ama vipi. Hebu tuangalie takwimu hizi.
Mwaka 1961 wakati tunapata uhuru idadi ya magraduates tulio kuwa nao ilikuwa 571 na tulikuwa watu karibu milioni tisa.
Mwaka 1963 Kenya ilipopata uhuru miaka miwili baadaye ilikuwa na jumla ya graduates 711 kwa watu karibu milioni saba.
Mwaka 1990 idadi ya waliokuwa wanajiunga na Chuo Kikuu nchini Tanzania ilukuwa karibu 3,000 wakati Kenya ilikuwa 30,000.
Mwaka 2000 (baada ya miaka 40 ya uhuru) jumla ya magraduates wa Tanzania ilikuwa karibu 40,000 kwa watu karibu 32,000,000 - ikiwa na maana ya graduate moja kwa kila watu 1,000 !!
Huo huo mwaka 2000, Kenya walikuwa na graduates zaidi ya 200,000 kwa watu karibu milioni 30,000,000 sawa na graduates moja kwa kila watu 150 !!
Inawezekana hizi takwimu si sahihi 100% lakini zinatoa mwanga jinsi sera zetu za elimu zilivyotudumaza. Halafu bado hatuoni umuhimu wa kutafuta njia bora za kuwasomesha wanetu badala yake tunatumia FFU kuzima manung'uniko yao. Uhadili wa wanafunzi Chuo Kikuu unafanywa chini ya uangalizi wa polisi walioshika bunduki.
Hapa Afrika Mashariki tu, tunaongoza kwa ujinga - je huko kwingine ? Inahitaji moyo kujaribu kutetea hali kama hii hata kwa muumini wa utulivu na amani. Kwa kukosa elimu tumeshindwa hata kuchagua kilicho bora.
Last edited: