''...Tanzania haitakalika''

''...Tanzania haitakalika''

Hivi bado hujajua kuwa utaratibu mpya wa kutoa mikopo ndio uliokiwezesha chuo cha Tumaini kuongeza idadi ya wanafunzi wake toka 200 mwaka 1997 hadi 8000 mwaka huu? Je hizi sio jitihada zinazostahili pongezi?

Wakati mwingine watanzania sijui tumelogwa ama vipi. Hebu tuangalie takwimu hizi.

Mwaka 1961 wakati tunapata uhuru idadi ya magraduates tulio kuwa nao ilikuwa 571 na tulikuwa watu karibu milioni tisa.

Mwaka 1963 Kenya ilipopata uhuru miaka miwili baadaye ilikuwa na jumla ya graduates 711 kwa watu karibu milioni saba.

Mwaka 1990 idadi ya waliokuwa wanajiunga na Chuo Kikuu nchini Tanzania ilukuwa karibu 3,000 wakati Kenya ilikuwa 30,000.

Mwaka 2000 (baada ya miaka 40 ya uhuru) jumla ya magraduates wa Tanzania ilikuwa karibu 40,000 kwa watu karibu 32,000,000 - ikiwa na maana ya graduate moja kwa kila watu 1,000 !!

Huo huo mwaka 2000, Kenya walikuwa na graduates zaidi ya 200,000 kwa watu karibu milioni 30,000,000 sawa na graduates moja kwa kila watu 150 !!

Inawezekana hizi takwimu si sahihi 100% lakini zinatoa mwanga jinsi sera zetu za elimu zilivyotudumaza. Halafu bado hatuoni umuhimu wa kutafuta njia bora za kuwasomesha wanetu badala yake tunatumia FFU kuzima manung'uniko yao. Uhadili wa wanafunzi Chuo Kikuu unafanywa chini ya uangalizi wa polisi walioshika bunduki.

Hapa Afrika Mashariki tu, tunaongoza kwa ujinga - je huko kwingine ? Inahitaji moyo kujaribu kutetea hali kama hii hata kwa muumini wa utulivu na amani. Kwa kukosa elimu tumeshindwa hata kuchagua kilicho bora.
 
Last edited:
Wakati mwingine watanzania sijui tumelogwa ama vipi. Hebu tuangalie takwimu hizi.

Mwaka 1961 wakati tunapata uhuru idadi ya magraduates tulio kuwa nao ilikuwa 571 na tulikuwa watu karibu milioni tisa.

Mwaka 1963 Kenya ilipopata uhuru miaka miwili baadaye ilikuwa na jumla ya graduates 711 kwa watu karibu milioni saba.

Mwaka 1990 idadi ya waliokuwa wanajiunga na Chuo Kikuu nchini Tanzania ilukuwa karibu 3,000 wakati Kenya ilikuwa 30,000.

Mwaka 2000 (baada ya miaka 40 ya uhuru) jumla ya magraduates wa Tanzania ilikuwa karibu 40,000 kwa watu karibu 32,000,000 - ikiwa na maana ya graduate moja kwa kila watu 1,000 !!

Huo huo mwaka 2000, Kenya walikuwa na graduates zaidi ya 200,000 kwa watu karibu milioni 30,000,000 sawa na graduates moja kwa kila watu 150 !!

Inawezekana hizi takwimu si sahihi 100% lakini zinatoa mwanga jinsi sera zetu za elimu zilivyotudumaza. Halafu bado hatuoni umuhimu wa kutafuta njia bora za kuwasomesha wanetu badala yake tunatumia FFU kuzima manung'uniko yao. Uhazili wa wanafunzi Chuo Kikuu unafanywa chini ya uangalizi wa polisi walioshika bunduki.

Hapa Afrika Mashariki tu, tunaongoza kwa ujinga - je huko kwingine ? Inahitaji moyo kujaribu kutetea hali kama hii hata kwa muumini wa utulivu na amani. Kwa kukosa elimu tumeshindwa hata kuchagua kilicho bora.

Quatitative vs Qualitative change- Ktk Machapisho ya kisayansi na vitabu ktk EA Tz tuko mbali ukilinganisha na Ug au Kenya hata Academics wa Kenya na Ug. wanajua hili. Kenya ubora zaidi ni 'good English'!

Je hii ndio kipimo cha maendeleo ktk elimu ya juu?

What do we need in Tz- Quality or Quantity? Je ni kipi bora?
 
Tanzania iko nyuma sana ya Kenya kwenye uandishi wa vitabu. Hatuna watu kama Ngugi wa Thiongo!

Quality education unayozungumzia Tanzania iko wapi? Umesahau hali halisi ya madarasa, waalimu, maktaba, maabara, etc ilivyo Tanzania? Kenya ni nafuu
 
Laiti angejua idadi ya vijana wanaoandikishwa shule na ni asilimia ngapi wanafika Chuo Kikuu - hakika angetokwa machozi.

Laiti angejua kuwa mazingira ya vyuo vyetu hayafikii hata yale ya shule za sekondari za jirani zetu - angetamani bingu zipasuke.

Laiti, laiti, laiti......lakini ndio utanzania huo. Tuna sababu za kutetea kila kitu hata vile tunavyojua wazi havihitaji utetezi wowote.
 
Maswala ya msingi kwenye hii mada ni:
(1) Kuna umuhimu wa serikali kuwapa wanafunzi mikopo kwa asilimia 100?
(2) Uwezo wa serikali kufanya hivyo upo?

Jibu la swali la kwanza linaonekana toka kwenye michango ya wengi. Katika nchi masikini na ambayo kiwango cha elimu bado kiko chini sana, ni vizuri Taifa lisomeshe vijana wote wanaochaguliwa kuingia vyuo vikuu. La sivyo watasoma watoto wa matajiri tu, na hao ni wachache mno!

Jibu la swali la pili linahitaji takwimu. Hotuba ya Bajeti ya Elimu ya 2008 - 2009 (ipo kwenye website a serikali) inatoa takwimu za vijana walioko kwenye Elimu ya Juu kama 65,966. Kurahisisha, tufanye 66,000. Ada wanayodaiwa na vyuo ni shilingi 2.7 million kila mmoja (Hiyo ni ya UDSM, na nimeweka link yake kwenye ukurasa wa 16 wa thread hii).

Ukizidisha idadi ya wanafuzi (elfu 66) kwa kasi cha ada (2.7 mi.) zinafika 178 billion shillings. Hizo ni17.8% ya bajeti yote ya Elimu ya mwaka huu.

Swala basi ni hili: serikali ina uwezo wa kutumia 178/=bn kulipia wanafunzi wa Elimu ya Juu? Ndiyo. Hizo ni kama nusu ya fedha zinazokusanywa na TRA kwa mwezi.
 
Hesabu zako haziko sahihi.
Kiwango kinachohitajika ni sh. bilioni 1200. Bajeti ya wizara ni sh. bilioni 1080.Wewe umehesabu wanafunzi wa vyuo vya serikali tena wa ngazi ya shahada peke yao. Elimu ya juu inajumuisha stashahada pia. Halafu umeconsider wanafunzi walio nchini tu, wale wa Ukraine mliokuwa mnapiga kelele serikali iwasaidie sasa hivi unajifanya umewasahau, na si Ukraine peke yake, karibu kila nchi kuna wanafunzi wanaowezeshwa na serikali. Juzi tu mlimsikia Dr. Slaa akimwomba balozi wa Tanzania nchini Urusi ajiuzulu kwa kutokuwasaidia wanafunzi kupata mikopo yao mapema. Unafikiri asilimia 100 ya mahitaji ya mwanafunzi wa Urusi ni sawa na ya mwanafunzi wa UDSM? Leo hii mnajifanya mnatoa mahesabu hayo katika pesa zinazohitajika? kweli mna lengo zuri na taifa letu nyinyi??? Hebu elezeni vizuri, nyinyi mnaotaka asilimia 100, mnataka hizo asilimia 100 wapewe wanafunzi wote wa kitanzania au wanafunzi wote wa vyuo vya serikali? mnapaswa kuweka hili bayana maana kama hesabu mnazopiga ni za vyuo vya serikali tu mnaanza kuonyesha dalili ya kujali wanaosoma kwenye vyuo hivyo peke yao!
Jamani hakuna haja ya kufanya propaganda katika jambo ambalo linawaathiri watu moja kwa moja. Hawa vijana hawapati elimu bora kwa sababu ya hii migomo isiyo na msingi wowote. Wapeni ushauri waelewe nini wanapaswa kufanya. Msiwasukume kwenye sakata la migomo halafu mkabaki kuwaangalia kama sinema.
 
66,000. Ada wanayodaiwa na vyuo ni shilingi 2.7 million kila mmoja (Hiyo ni ya UDSM, na nimeweka link yake kwenye ukurasa wa 16 wa thread hii).

Ukizidisha idadi ya wanafuzi (elfu 66) kwa kasi cha ada (2.7 mi.) zinafika 178 billion shillings. Hizo ni17.8% ya bajeti yote ya Elimu ya mwaka huu.

Swala basi ni hili: serikali ina uwezo wa kutumia 178/=bn kulipia wanafunzi wa Elimu ya Juu? Ndiyo. Hizo ni kama nusu ya fedha zinazokusanywa na TRA kwa mwezi.

Kumbuka kuwa wanafunzi hawa hawadai asilimia 100 ya ada wanadai asilimia 100 ya mahitaji yao, ambayo ni ada, chakula, malazi, vitabu, stationary, pesa za field na special faculty requirements. Sasa kama unapiga mahesabu ya ada peke yake inaonekana unafanya makusudi kupindisha mahesabu au hujui mahitaji ya wanafunzi hawa.

Sentensi yako kuwa mahitaji ya wanafunzi ni nusu ya makusanyo ya TRA ya mwezi siyo sahihi kama nilivyoelezea awali. Lakini hata kama ingekuwa sahihi bado ungekuwa unaclaim wanafunzi wapatiwe asilimia 4 ya mapato ya nchi ya mwaka. Hivi kweli duniani kuna nchi hata moja inazoweza kutumia asilimia 4 ya mapato yake kulipia mahitaji ya wanafunzi wa chuo kikuu peke yao? Tafadhali tafuta nchi hata moja duniani inayofanya hivyo kwenye bajeti yake.

Kumbuka kuwa mahitaji ya wanafunzi is just part of mahitaji ya wizara ya elimu. Kuna tafiti zinatakiwa kufanywa, kuna development ya new institutions and teaching programmes, kuna pesa zinazohitajika kuwasomesha walimu wao, kuna pesa zinahitajika kununua na kumaintain scietific tools etc. Labda nikuulize mashine moja ya PCR machine na other molecular genetics tools zinauzwa sh. ngapi? Hivi kweli tunataka kuwa competitive humu duniani? Kama tunataka kuwa competitive ni LAZIMA kuwe na sacrifice. Hii tabia ya kila mtu kuangalia jinsi atakavyoweza kumega kile kilichopo bila kuangalia jinsi ya kurudishia ili na wengine wapate kwa kumega haitupeleki pazuri.
 
kichwa cha habari "nchi haitakalika", mimi nadhani inabidi tuwe makini sana na nchi inavyokwenda, inchi inaonekana imeshapoteza mwelekeo katika kila kitu, ili swala la chuo kikuu si la mzaa hata kidogo, vyuo vikuu ndo siasa ya nchi inapoanzia na uongozi wa nchi unapotokea. kwa huyu bwana kama msomi na amejaribu ku analyse mambo na influence ambazo wasomi wanazo ni rahisi sana kuhubiri chochote na nchi isikalike, jamani nchi kutokalika haianzi na mambo makubwa kuna kuwa na mrundikano wa vijimambo and then kitu kidogo tu kinawasha moto mkubwa sana, angalia Greece baada ya mtoto mdogo kuuawa inchi iliingia kwenye matatizo makubwa sana watu nchi nzima walifanya fujo lakini ukiangalia hiyo haikuwa sababu ya msingi ila kilikuwa ni chanzo cha watu kuelezea matatizo yao ya kiuchumi, kilichowasaidia ni kwamba angalau wenzetu tayari wana system inayofanya kazi hivyo ikawa ni rahisi kutatua tatizo lakini hali kama hiyo ikitokea hapa TZ sijuhi itasawazishwaje?

kuhusu swala la quality ya elimu kwa mtazamo wangu Tanzania tupo juu ya Kenya, nimeishi na kufanya kazi kwenye SADC countries almost zote na hakuna Expert mwafika anae heshimika kama mtanzania, ni hapa tanzania tu kwa sababu ushauri unaokubalika serikalini ni wa kisiasa tu ndo maana unaona elimu yetu haina maana angalia uhamuzi wa mawaziri wetu wasomi (JK, MASHA, LOWASA, NK), wote utaona wanaamua kisiasa tu, LABDA SINA UHAKIKA SANA ILA NAMWONA MAGUFULI PEKEYAKE NDO ANAKUWAGA NA UHAMUZI WA KISOMI
 
Hesabu zako haziko sahihi.
Kiwango kinachohitajika ni sh. bilioni 1200. Bajeti ya wizara ni sh. bilioni 1080.Wewe umehesabu wanafunzi wa vyuo vya serikali tena wa ngazi ya shahada peke yao. Elimu ya juu inajumuisha stashahada pia. Halafu umeconsider wanafunzi walio nchini tu, wale wa Ukraine mliokuwa mnapiga kelele serikali iwasaidie sasa hivi unajifanya umewasahau, na si Ukraine peke yake, karibu kila nchi kuna wanafunzi wanaowezeshwa na serikali. Juzi tu mlimsikia Dr. Slaa akimwomba balozi wa Tanzania nchini Urusi ajiuzulu kwa kutokuwasaidia wanafunzi kupata mikopo yao mapema. Unafikiri asilimia 100 ya mahitaji ya mwanafunzi wa Urusi ni sawa na ya mwanafunzi wa UDSM? Leo hii mnajifanya mnatoa mahesabu hayo katika pesa zinazohitajika? kweli mna lengo zuri na taifa letu nyinyi??? Hebu elezeni vizuri, nyinyi mnaotaka asilimia 100, mnataka hizo asilimia 100 wapewe wanafunzi wote wa kitanzania au wanafunzi wote wa vyuo vya serikali? mnapaswa kuweka hili bayana maana kama hesabu mnazopiga ni za vyuo vya serikali tu mnaanza kuonyesha dalili ya kujali wanaosoma kwenye vyuo hivyo peke yao!
Jamani hakuna haja ya kufanya propaganda katika jambo ambalo linawaathiri watu moja kwa moja. Hawa vijana hawapati elimu bora kwa sababu ya hii migomo isiyo na msingi wowote. Wapeni ushauri waelewe nini wanapaswa kufanya. Msiwasukume kwenye sakata la migomo halafu mkabaki kuwaangalia kama sinema.

Mkuu hii hesabu ya kwamba zinahitajika Ths Bilioni 1200 unaweza kusubstantiate or else kuelezea source maana sijawahi kuisikia mahali pengine. Halafu kwa ushauri tu, jaribu kutokuwa personal unapowakilisha hoja zako. Inapunguza nguvu ya hoja and sometimes kuifanya hoja kuonekana childish!!!!!!!!!!!!
 
Quote:
"Kwa wanafunzi, kama wewe wajiona huna uwezo wa kupata 20% percent ya ada yako usichangue kazi. Fanya, by the way kazi ni kazi. Hii tabia ya ubrazamen au usisita duu si nzuri. Ni ujinga kukataa kazi ya kusafisha eti kisa wewe ni mwanafunzi. Not good at all."

Mkuu hii point ni ya ukweli kabisa, tatizo la wanachuo wa bongo ni kujiona wao wako juu
sana kufanya shughuli za aina fulani. Wanaogopa kuchekwa so to speak. Wengi waliosoma nje wengine wakiwa na ofisi zao za heshima bongo, wamepiga kazi za "hovyo" sana, tena kwenye mazingira magumu ya barafu ikianguka.

Lakini mwanafunzi wa chuo bongo ukimwambia labda aanzishe "Kasalon" kunyoa(kichwa 1000-2000), au kuosha magari(gari moja 1000- 3000) au kupika chipsi au mama lishe(plate 300 -1000), watakwambia kazi za "kichovu" university student hawezi kufanya... ulaya ni kawaida kukuta mature wanafunzi wa Phd wakifanya odd jobs, let alone hawa mostly youth students.

Mwanafunzi wa bongo hajiulizi "why not me" ili AFANYE such kazi, bali hujiuliza "why me" ili ASIFANYE hizo kazi. Umwinyi at its best. TUBADILIKE...Kuanzia kwenye MINDSET.

Na kwa nchi kama yetu ukishaanza kujiuliza "why me" ili USIFANYE kitu, majibu yatakua meeengi na analysis zitakua ndeefu ili kujustify umwinyi. Coz its the easier thing to do. Wabongo siku zote hatukosi "good reasons" kujustify short cuts, kutokujituma au kutokuwajibika...

Tunailaumu serikali ndio, na naunga mkono hili, lakini ni vizuri tukajiangalia na sisi wenyewe.
 
Swali la kizushi:

Hivi kuna nchi gani INAYOENDELEA(meaning Least Developed Countries) yenye population ya ZAIDI ya milioni 30, inayowapa wanachuo wake WOTE grant ya 100%?

Tukishaijua, tutaweza kujifunza a thing or two kutoka kwao.
 
Last edited:
kwanza hilo suala cost sharing linakuja vipi hapo ikiwa utakopa 60% and the rest 40% unazilipa bila kukopa kwenye bodi.Sasa hapo si tayari mtu amelipa 100% bila share from gvnt?
 
Swali la kizushi:

Hivi kuna nchi gani INAYOENDELEA(meaning Least Developed Countries) yenye population ya ZAIDI ya milioni 30, inayowapa wanachuo wake WOTE grant ya 100%?

Tukishaijua, tutaweza kujifunza a thing or two kutoka kwao.

Cuba ina some 12 million na elimu ya juu ni bure, well let us assume hiyo ni 1/3 ya milioni 30. Basi na sisi tutoe elimu bure kwa idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu equivalent na one third ya Cuba in that perspective au tujifunzie hiyo 1/3 yao kwamba inawezekanaje
 
Please tusome hii!!!!!!!!!

Cuba's population is 11.39 million. Life expectancy is 77 years, the same as that in the US (Unesco data 2005)

The island's literacy rate is 99.8 per cent

In 2006, the country's GDP - purchasing power parity adjusted - was £20 billion, or £2,000 per person a year

The University of Havana, founded in 1728, is the oldest institution of higher education on the island and one of the oldest in the Americas

Some 44 per cent of students completing first-degree programmes in Cuba studied education, 21 per cent health and welfare and 19 per cent social sciences, business and law

The gross completion ratio for first-degree studies (the proportion of the overall population at a typical age of graduation that completes a first degree) was 14.2 per cent in Cuba in 2005 against 40 per cent in the UK for the same year, according to Unesco

The number of students enrolled in tertiary education per 100,000 inhabitants in Cuba in 2005 was 4,196, compared with 3,846 in the UK and 5,847 in the US, according to Unesco figures
 
Na hii halafu linganisha na statistics za bongo.

According to the Unesco Institute for Statistics, Cuba's gross enrolment for tertiary education of the relevant age cohort was 61.5 per cent in 2005 against 53.6 per cent in 2004. The equivalent 2005 figure for the UK was 59.7 per cent and 82.7 per cent for the US
 
Suala tuition hilo,ni watanzania wangapi watakaofundisha tuition? Hapa itakuja kuwafanya hata watu ambao hawana uwezo wa kufundisha tuition kuingia kwenye game na kuwaharibia madogo future.Maanake hii ndiyo kazi ambayo form six leaver anaeza kujiajiri

Si utani,hata mimi nimendusha Advanced Chemistry Pale YWCA Moshi na Mzumbe center.Kwa kweli unaweza kutengeneza hela nyingi na kama wewe ni mwanafunzi tuseme wa UDSM ratiba zao ni ishu kuweza kufanya kazi upate hela nyingi at the same time upandishe madude yako fresh darasani,sana sana unaweza kuwalostisha madogo bure kwa uroho wa hela nyingi
 
Mkuu Nyambala,
Statistics za cuba on social services are highly impressive, no doubt!... sasa kama population yao 2008 ndio wako milioni 11.4, sijui huko 1970 or 1980 walikua wangapi.
Im am not trying to take anything away from sera nzuri zenye results walizonazo. Na naamini there are man things za kujifunza kutoka kwao, no doubt. Ila numbers do matter... Pamoja na kuitwa developing country lakini Cuba GDP per capita yao ni USD 12,700 wakati ya kwetu ni 1,300, that is ten times ile ya kwetu. Halafu wakati wao wapo watu 11.4m sisi tupo 40m, yaani 1/4 au robo yetu (CIA world fact book).

I am not sure kama huu ni mfano comparable na sisi. But thanks for the informative and awe inspiring posts on cuba.
 
Last edited:
Mkuu Nyambala,
Statistics za cuba on social services are highly impressive, no doubt!... sasa kama population yao 2008 ndio wako milioni 11.8, sijui huko 1970 or 1980 walikua wangapi.
Im am not trying to take anything away from sera nzuri zenye results walizonazo. Na naamini there are man things za kujifunza kutoka kwao, no doubt. Ila numbers do matter... Pamoja na kuitwa least developed lakini Cuba GDP per capita yao ni USD 12,700 wakati ya kwetu ni 1,300(CIA world fact book), that is ten times ile ya kwetu.

I am not sure kama huu ni mfano comparable na sisi. But thanks for the informative and awe inspiring posts on cuba.

Big up mkuu, well tukisema tutafute nchi zenye ezactly GDP per capita kama yetu unaweza kukuta tena kiuhalisi haatufanani maana I am one of those wanaoona hii data kwa TZ imepikwa. Well all in all nilichojaribu kukonvey hapo ni kwamba it is possible kusomesha vijana wetu ikiezekn hata wote. Tatizo naloliona hapa ni kwamba hii ishu imekuwa politicized to an extent inaonekana kama shida ni hhela tu wakati infact it is not.
 
Mkuu Nyambala,
Statistics za cuba on social services are highly impressive, no doubt!... sasa kama population yao 2008 ndio wako milioni 11.8, sijui huko 1970 or 1980 walikua wangapi.
Im am not trying to take anything away from sera nzuri zenye results walizonazo. Na naamini there are man things za kujifunza kutoka kwao, no doubt. Ila numbers do matter... Pamoja na kuitwa least developed lakini Cuba GDP per capita yao ni USD 12,700 wakati ya kwetu ni 1,300(CIA world fact book), that is ten times ile ya kwetu.

I am not sure kama huu ni mfano comparable na sisi. But thanks for the informative and awe inspiring posts on cuba.

Ni vizuri kujilinganisha na wengine kwa nia nzuri ili nawe uweze kupata mafanikio zaidi; lakini pia hili lina matatizo yake iwapo mtu atataka kuyafikia hayo mafanikio kwa haraka sana bila utaratibu maalum na kuzingatia mambo yote muhimu katika kufanya hivyo. Na ndiyo maana sasa hivi tunaongelea "Mafisadi" ...

Lakini pia tukirudi nyuma, nadhani Mwalimu Nyerere alianza vizuri kwa kuanzisha viwanda vyetu wenyewe ili tuzalishe vitu vyetu vya ndani na hata kuuza nje ... havipo tena, ama vilihujumiwa, sijui ... Lakini hii kitu ndiyo ingekuwa mkombozi wetu kwa maana ya uzalishaji ... sasa hivi sisi ni walaji tu, na tunakula vilivyozalishwa na wengine (imported) hadi chakula (kilimo) ... kuna watu eti wana njaa ... na hakuna ukame ... something is WRONG with us!!

Nimefurahishwa na hii hapa: "The University of Havana, founded in 1728, is the oldest institution of higher education on the island and one of the oldest in the Americas"

How many universities did we have in 1728, if at all kulikuwa na Tanzania/Tanganyika?
 
hilo la kuchangia elimu kwa kweli aliwezi kupingika na hakuna anayelipinga lakini lazima uwepo usawa katika hilo,
kwanza lazima kuwe na mfumo wa kuwajua raia wote na vipato vyao(national database), kwa hiyo basi mwanafunzi anapoingia chuo kikuu anajulikana asaidwe asilimia ngapi na sio lazima iwe 60 by 40, inaweza ikawa 1,2 au hata 100 kutegemeana na kipato cha familia husika, lakini ukitegemea wanafunzi ndio wakuletee data zao, wote watakuwa hawana uwezo na mwisho wa yote watoto wa wakubwa ndo watazaminiwa tu, hapa panahitaji hekima sana, lakini kwa kufuta mfumo huu wasomi wazuri wenye vipaji wataachwa tu porini wakichunga ngombe na kuvua samaki maziwani
 
Back
Top Bottom