Kama hili ni kweli basi wamrudishe nyumbani balozi wetu Zimbabwe na pia wamuombe wa Zimbabwe arudi kwao.
Bubu wa Zimbabwe alisharudi Zimbabwe.
Labda kama karudi tena Dar-es-Salaam.
Hukusikia kokote kwa sababu Tanzania hakuna press.
sijui kama wakuu wamelitazama hili. unapokuwa humtambui rais wa nchi na serikali yake inamaana hatua ambayo inafuata ni kuvunja uhusiano wa kibalozi au "kumuita balozi wenu nyumbani kwa mashauriano." sasa kama ndio mmeishaitiana mabalozi wenu kwa mashauriano sijui huko sadc kutakaaje.
Kwa maana hiyo unanambia niliyemuona anatangaza hakuwa mkuu wa usimamizi wa uchaguzi wa SADC bali alikuwa Tony Blair???
Mimi nina akili timamu za kutambua propaganda na ukweli, kilichotokea Zimbabwe ni ukweli tupui suala ni kuwa vilipewa kipaumbele saana katika TV yao.
Unaposema uchaguzi ulikuwa free unamaanisha nini? Mamilioni ya Wazimbabwe waliokimbilia SA na msituni na walichomwa moto matakoni na sehemu zingine za mwili hawakupata hiyo freedom unayoisema
Kuna press lakini ni corrupt!
Press siyo source of information..Wao wanaripoti tu baada ya ku gather information.
Hata hivyo kama walivyofanya kwenye hiyo issue ya Balozi..Waliamua kui ignore source hiyo ya information kuhusu mabalozi hao!
Na saa nyingine hata wakiamuwa kuto kuignore na kuwa wakweli kama wako hao wakweli...Then tunarudi back kwenye tatizo...SOURCE...UNAKUMBUKA MWENYEWE NI KAULI NGAPI KINZANI ZA SERIKALI ZILIZOWAHI KUTOLEWA KUTOKA KWA MEMBE,MKULLO,NA SALVA !
You are so incoherent.
Unasema press ipo lakini ni corrupt.
Unasema press ipo lakini ina ignore information za Kidiplomasia kuhusu moja ya ishu kubwa kuliko zote kwenye press duniani sasa hivi.
Unasema kuna press wakati hapo hapo una doubt kama wapo waandishi wakweli.
So incoherent. Almost ridiculous.
Unatanisamehe, lakini ni kituko, tena karibia na utupu, kukubali yote hayo juu halafu kunikatalia kwamba hakuna press.
So incoherent.
Nyangumi,
Nafikiri huyafahamu ya huko kusini ndio maana unasema kuwa wa Zimbabwe walioko SA walimkimbia Mugabe. Sijui na wa TZ, waMozambique, Nigeria, Kenya n.k. walioko huko wote pia wamekimbia maraisi wao?
Uchaguzi Zimbabwe umekuwa wa mtu mmoja kwa vile Tsvangirai aliamua kujitoa dakika ya 90 kinyume na sheria maana pengine alihisi kushindwa, who knows. Awamu ya kwanza matokeo yalikuwa 47% MDC, 42% Mugabe, niambie hata kama ni wewe tena baada ya kukimbilia SA utakuwa na uhakika kweli wa kushind re-run?
Ni kweli vurugu zilikuwepo hapa na pale na waliokumbwa nazo hata elfu hawafiki, hii ni kwa taarifa ya MDC. Wewe umeng'ang'ania na picha za propaganda za kwenye net, mbona hazikuonyeshwa kwa maelfu kama ilivyokuwa vurugu za SA, au kuonyeshwa video, zaidi ya ile ya wale vijana wanaokimbizana waliovaa vilemba vya ZANU-PF??
Swali kwenye free election ni kuwa je watu walishindwa kupiga kura ingawa walitaka kufanya hivyo? Ukweli ni kuwa hata baada ya Morgan Tsvangirai kuwataka watu wakae nyumbani, bado wengi walijitokeza kwenda kumpigia Tsvangirai kura au kuziharibu. Hii inaonyesha dhahiri kuwa access ya kupiga kura ilikuwapo na ndio maana nasema uchaguzi ulikuwa FREE, lakini kuwa FAIR kunaweza kuwa discussed kutokana na vurugu za awali.
Tuachane na kudance hizi ngoma tunazopigiwa kwa vile sauti zao ni kubwa. Mambo Zim ni kweli hayaendi sawia, lakini tusijiunge tu na kwaya hii inayotuambia kuwa sababu tu ni Mugabe, kwa vile wao wana vita naye basi na sisi tujiingize. Historia itatuadhibu kama hatuisomi ipasavyo hivi sasa. Zidumu fikira za Mwalimu.
Mi nadhani ni dhahiri kuwa there was intimidation, maiming and killing during the election, eti kusema kuna watu walijitokeza kumpigia kura Tsvangirai is a delusional claim, maana wengi hivi sasa ni refugees at the US embassy, wengine wamekuwa viwete na wanaugulia hospitali. Usichanganye pan Africanism na uhuni wa Mugabe. Mwalimu Nyerere kama angekuwa hai asingeweza kusapoti uhuni, ubabe na mauaji ya Mugabe in the name of Pan Africanism. Mugabe has to go!!!!!
Kubwajinga;
BBC, CNN, na most of western journalists hawaruhusiwi kukanyaga Zimbabwe. Zile picha unazoziona ni zile tu ambazo zinapigwa na freelance photographers (at their own risks). Hata NGO zimepigwa marufuku, utapataje news? Au wewe unategemea ile Herald (Uhuru version of Zimbabwe)? Acha siasa za kizamani hizo!
Mkuu Nyangumi,
Ningekushauri tu kuwa BBC iwe sehemu yako ya mwisho kupatia habari za Zimbabwe hasa zinapokosekana mahali pengine popote.
Kisheria, kitu ambacho ndio pekeyake alichokitaka Mugabe, uchaguzi wa Zimbabwe umetimiza vipengele vyote vinavyotakiwa. Was it FREE, absolutely YES. Was it FAIR probably NOT. How was the elections in TZ, Uganda, Kenya, Ethiopia, Nigeria n.k.? FREE but not FAIR, and no one listened to the opositions. Why is Zim so special?. How on earth should Kikwete say Mugabe is not a president but Karume is?
Mr Zero issue ya Zanzibar na ya MUGABE ni tofauti kabisa!Labda ya Zanzibar inafanana na ile ya Kenya!
Tofauti ni kwamba ZIMBAMBWE MUGABE kagombea peke yake na khali Morgani naye alitakiwa agombee!hapa issue ni MORGAN na MUGABE waingie kwenye ulingo!ili ukweli ujulikane je ni MUGABE AU MORGAN!
tatizo linakuja serikali yetu inaangalia sana nje na ilifanikiwa kusaidia maelewano kenya na khali hapa kwetu the same tatizo kama la kenya limetushinda hadi leo
Mr Zero issue ya Zanzibar na ya MUGABE ni tofauti kabisa!Labda ya Zanzibar inafanana na ile ya Kenya!Tofauti ni kwamba ZIMBAMBWE MUGABE kagombea peke yake na khali Morgani naye alitakiwa agombee!hapa issue ni MORGAN na MUGABE waingie kwenye ulingo!ili ukweli ujulikane je ni MUGABE AU MORGAN!tatizo linakuja serikali yetu inaangalia sana nje na ilifanikiwa kusaidia maelewano kenya na khali hapa kwetu the same tatizo kama la kenya limetushinda hadi leo