Nyangumi,
Nafikiri huyafahamu ya huko kusini ndio maana unasema kuwa wa Zimbabwe walioko SA walimkimbia Mugabe. Sijui na wa TZ, waMozambique, Nigeria, Kenya n.k. walioko huko wote pia wamekimbia maraisi wao?
Uchaguzi Zimbabwe umekuwa wa mtu mmoja kwa vile Tsvangirai aliamua kujitoa dakika ya 90 kinyume na sheria maana pengine alihisi kushindwa, who knows. Awamu ya kwanza matokeo yalikuwa 47% MDC, 42% Mugabe, niambie hata kama ni wewe tena baada ya kukimbilia SA utakuwa na uhakika kweli wa kushind re-run?
Ni kweli vurugu zilikuwepo hapa na pale na waliokumbwa nazo hata elfu hawafiki, hii ni kwa taarifa ya MDC. Wewe umeng'ang'ania na picha za propaganda za kwenye net, mbona hazikuonyeshwa kwa maelfu kama ilivyokuwa vurugu za SA, au kuonyeshwa video, zaidi ya ile ya wale vijana wanaokimbizana waliovaa vilemba vya ZANU-PF??
Swali kwenye free election ni kuwa je watu walishindwa kupiga kura ingawa walitaka kufanya hivyo? Ukweli ni kuwa hata baada ya Morgan Tsvangirai kuwataka watu wakae nyumbani, bado wengi walijitokeza kwenda kumpigia Tsvangirai kura au kuziharibu. Hii inaonyesha dhahiri kuwa access ya kupiga kura ilikuwapo na ndio maana nasema uchaguzi ulikuwa FREE, lakini kuwa FAIR kunaweza kuwa discussed kutokana na vurugu za awali.
Tuachane na kudance hizi ngoma tunazopigiwa kwa vile sauti zao ni kubwa. Mambo Zim ni kweli hayaendi sawia, lakini tusijiunge tu na kwaya hii inayotuambia kuwa sababu tu ni Mugabe, kwa vile wao wana vita naye basi na sisi tujiingize. Historia itatuadhibu kama hatuisomi ipasavyo hivi sasa. Zidumu fikira za Mwalimu.