Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,956
Mi nadhani ni dhahiri kuwa there was intimidation, maiming and killing during the election, eti kusema kuna watu walijitokeza kumpigia kura Tsvangirai is a delusional claim, maana wengi hivi sasa ni refugees at the US embassy, wengine wamekuwa viwete na wanaugulia hospitali. Usichanganye pan Africanism na uhuni wa Mugabe. Mwalimu Nyerere kama angekuwa hai asingeweza kusapoti uhuni, ubabe na mauaji ya Mugabe in the name of Pan Africanism. Mugabe has to go!!!!!
Yaani unajua nikisoma post za KubwaJInga nachanginyikiwa kabisa. Yaani haoni hata aibu kusema uchaguzi ule ulikuwa huru, akisema haya hapohapo anakiri kwamba kuna watu walichomwa visu na moto matako lakini sio wengi! Halafu anadiriki kusema kwamba MDC walijitoa kwa sababu waliogopa kushindwa, na hapo hapo anatoa statistics zinazonyesha kwamba MDC walishinda katika uchaguzi wa awali, sasa unajiuliza huyu mtu anatumia vigezo gani katika kujenga hoja zake ambazo zinajichanganya kiasi hiki!? Nafikiri tunachotofautiana hapa sio kwamba urais wa Mugabe ni halali au la, bali ni kwamba kuna baadhi yetu wanatumia hisia (gut feelings) kutoa maoni yao wakati wengine tunatumia uhalisia wa mambo (evidence).
Ni aibu zaidi kusema kwamba nchi yetu ikae kimya au Mugabe aachwe na uharamia wake kwa sababu tu nasi tulivuruga uchaguzi huko Zanzibar. Kwa hiyo mnataka tukubaliane kwamba sisi ndivo tulivyo na hatuna haja kubadilika? The argument couldn't be weaker and any more ludicrous!