Mkuu Ogah,
Heshima mbele kaka, na nimekusikia lakini bado ninarudia kuwa Tanzania tumekosea tena sana, ninaamini ni kutokana na kimbele mbele chetu cha siku zote kutaka kuonekana mbele ya dunia kuwa we know better, lakini Waziri wetu wa nje kwenye hili amekurupuka sana na tena ni aibu kubwa sana kwetu kama taifa kwa sababu hakuna facts wala political evidece strong enough za kuhalalisha msimamo wetu, in fact facts nyingi sana zinam-back Mugabe, isipokuwa tu tatizo ni kwamba yeye na wanajeshi wake wana-react emotional zaidi kuliko common sense, na the results ni kuishia kuharibu hata ule ukweli mzito walionao ambao bado unawapa haki wao na Mugabe, kuwa walivyo on this ishu, ingawa tunapinga kabisa kitendo cha kuwasulubu wananchi wasio na hatia,:-
1. Waziri wetu wa nje amekurupuka kwenye hili kwa sababu historia ya hii ishu haiko upande wake, according to the dataz ni kwamba hili tatizo Mugabe aliliona kwa mara ya kwanza wakiwa kwenye mkutano wa uhuru kule Lacanster, ambako yeye na Joshua Nkomo, Sithole walikwenda kwenye mkutano ule kwa kushinikizwa sana na Mwalimu.
2. More dataz ni kwamba Kwenye ule mkutano Mwalimu, aliwatuma kina Mugabe kufuatana na washauri watatu kutoka Tanzania, nao ni Dr. Salim A. Salim, Sinde Warioba, na Charles Kileo, lakini maamuzi yote mazito on Mugabe side yalikuwa yakiamuliwa Dar na Mwalimu. USA kwenye hicho kikako iliwakilishwa na Balozi Andrew Young, aliyekuwa akimuwakilisha Kissinger.
3. According to more dataz ni kuwa Mugabe, alikuwa na matatizo mawili makubwa, nayo Ardhi na kuondolewa kwa wazungu kwenye position kubwa za serikali, hizi ishu zilikuwa so difficult kuzi-solve kwamba ilifikia one point Mugabe akaamua kujitoa kwenye kiikao na kurudi porini, Mwalimu akamjia juu kuwa akijitoa atamfunga, Mugabe akabaki kwenye mkutano.
4. The dataz ni kwamba kwenye ishu ya ardhi, makubaliano yalikuwa kwamba Mugabe asubiri Uingereza itakuwa ikitoa hela kwa serikali ya Zimbabwe kwa ajili ya kununua ardhi back kutoka kwa wazungu, zoezi ambalo lilitakiwa kuchukua miaka 15-20, toka uhuru wa Zimbabwe, likiwa linafanyika pole pole, na Andrew Young, akaahidi kwa niaba ya USA kuwa wao watasaidia kuchangia zile hela kwa serikali ya Zimbabwe kununua ardhi, Kwenye ishu ya wazungu kuondoka serikalini, ikakubaliwa wapewe miaka 10, ambapo wataondoka kwa pole pole.
5. The dataz ni kwamba haya yaliyokubaliwa yalikuwa yakifanyika kama ilivyokubaliwa, mpaka mwaka 1997 kushindwa kwa serikali ya Major ndio kilichokuwa chanzo cha matatizo ya Zimbabwe, meaning kwamba ni Tony Blair ndiye aliyehusika sana na ku-instigate matatizo haya, walipoingia tu madarakani, Tony Blair alimtuma waziri wake wa Afrika, kumuandikia barua nzito sana Mugabe, barua ambayo iliwekwa sana kwenye magazeti ya Zimbabwe then, ambako Labor Party walsiema kuwa hawana mpango wa kujihusisha kabisa na maamuzi mengi yaliyofanywa na taifa lao as a Colonist na kwamba hela za land hazitakuwepo tena, na kwamba wanataka Mugabe ajibu matatizo ya uhalali wa serikali kuwepo kwenye power, hasa kutokana na malalamiko ya Commnwealth kuwa uchaguzi wake then haukuwa wa halali,
Halafu pia USA, ambao waliahidi kusadia kutoa hela za kununua ardhi kule Lancaster, hwakutoa hata senti tano toka uhuru wa Zimbabwe, mpaka kuelekea mwaka 1997 Labor Party ilipokuwa inaingia kwenye power, kwa hiyo in short hapa ni Tony Blair ndiye aliyeamua ku-change the subject kutoka kwenye makubaliano ya kununua ardhi back, na sasa kuwa Demokrasia in Zimbabwe, sasa swali langu hapa ni je Waziri Wetu wa Nje anayajua haya kweli?
6. Tha dataz ni kwamba haikuchukua muda mrefu since then NGO moja kali sana kule UK iliyokuwa ikifadhiliwa na serikali pamoja na chama cha Tony Blair, physically ikaanzisha chama cha siasa cha upinzani zimbabwe, kinachoitwa MDC, NGO hiyo ambayo kwa jina inaitwa West-Minister Foundation, ndiyo iliyo andika hata katiba ya chama hicho yaani MDC, kikiwa pia kikipewa misaada ya hela toka serikali ya US, chama ambacho hatimaye walim-hand pick Tshangarai kuwa mwenyekiti wake, ambaye majuzi aligombea tena urais. Pia walianzisha gazeti na kutaka pia kuanzisha Radio na TV, station lakini Mugabe akagoma kwa hiyo wakaenda kunzisha Radio na TV Botswana. Na hata hivi karibuni kulipotokea matatizo makubwa ndani ya MDC, sio siri kuwa balozi wa US kule aliwaita viongozi wa MDC na kuwapa US Dollars 1,000,000 ili waelewane, na ndio maana Tshangarai akakimbilia ubalozi wa Dutch kwa kushauriwa na balozi wa US kwamba angekimbilia kwao hizi habari zingetoka nje!
7. Ni hapa sasa ndipo wanajeshi wa Mugabe waliopigania uhuru wa nchi hiyo, walipoamua kuanza ku-react emotionally, badala ya kutumia diplomasia au political wisdom kwa sababu walijua wazi kuwa kama ni The West, hakuna wa kumuamini tena, na ndio maana Mugabe hawezi kuwasikiliza viongozi wa Afrika ambao either hawaelewei kitu on fact na history, au wanafanya makusudi, Mugabe hawezi kuwasikiliza Botswana kwa sababu kwanza wanatumiwa na UK, halafu hata rais wao Botswana ni mtoto aliyezaliwa na mwanamke wa kiingereza inamfanya Mugabe kukasirishwa sana nao, na pia by the fact of the dataz kwamba sasa hivi US wanajenga base yao Botswana sasa should Mugabe litsen to Botswana? Ninasema hapana tena a big no!
Kwa kumaliza ninarudia tena kuwa Waziri wetu wa Nje amekurupuka na Tanzania tunapaswa kuwa ashamed, kwa sababu tulipaswa kujua haya yote niliyoyatoa hapa kutoka kwenye dataz zangu, sasa tumegeuka kichekesho mbele ya mataifa yaliyokuwa yakituheshimu sana zamani,
sisi Tanzania ni wanachama wa Security Council ya SADC, ambayo inajumuisha Angola(Chairmarn), Lesotho na South Afrika, kwenye hicho kikao muhimu South Africa hawakwenda wala Angola, tulihudhuria sisi tu na Lesotho, lakini ni maajabu makubwa kwamba Tanzania tukaamua maamuzi ambayo baadaye tukaya-forward mbele kwa AU kama ni maaamuzi ya serikali zote nne za ile Securty Council ya SADC, marokeo yake ikawa aibu kule Egypt kwa sababu South Afrika na Angola zikaja juu kuwa hazikushiriki kutoa huo uamuzi nasikia tukaabika sana mbele ya chi zingine za Afrika,
Look, majuzi mkutano ulipokuwa unaanza Gordon Brown na Condi Rice, waliwatumia ujumbe mzito viongozi wote kule Egypt kuwa Mugabe, asikubaliwe kabisa kutambuliwa kama rais, na kweli viongozi wetu wengi wa AU wakaitikia wito huo wa wazungu, ninaomba kumuuliza Waziri wetu wa Nje kwamba ni lini sisi waa-Afrika tuliwahi kuwapa ushauri viongozi wa EU na US wanapokutana nini cha kujadili? Si majuzi tu Rais Bush alijaribu kuwashinikiza kuwa EU wawakubali Turkey kwenye jumuiya yao, hivi kweli tunajua majibu aliyopewa na viongozi wa EU? aliambiwa akae mbali sana na ishu za EU hazimuhusu, sasa sisi ni kwa nini wao wanatumabia na tunafuata tu kama wajinga?
Waziri wetu wa nje anapaswa kujua kuwa sasa tunachekesaha sana nje, na tayari nchi nyingi zimeshashituyka kuwa tunatumiwa na mkono mmoja mzito kutoka nje, ambao sasa hivi unatushinikiza kutoa haya maamuzi ikiwa ni kujiweka sawa na mkutano ujao utakaofanyika Japan hivi karibuni, according to the dataz ni kwamba tumeahidiwa misaada mingi kupitishwa huko na huo mkono kwa ajili ya kutusaidia Tanzania, that is pathetic forign policy!
Tanzania tuliowahi kuwasidia Zimbabwe kwa hali na mali kupata uhuru wao, tulipaswa kuwa makini badala ya kuanza kuwa "malaya" wa siasa, kwa sababu hapa we are about kugombana na ndugu zetu wenyewe kwa sababu tu ya vipande vichache vya silver, with all his problems France, EU wala US haikuwahi hata siku moja kusiadia kumuondoa Mobutu, lakini hao hao leo wanatumabia kuwa tumkamne Mugabe, na here we are kama kondooo na the sd thing ni pale hata wananchi wenzetu wanaposhangilia huu uamuzi, tunajua kuwa kuna wale ambao pia wanafaidika na ile misaada ya West-minister NGO, maana wale wapo kila kona za upinzani Afrika, lakini Afrika haiwezi kuamuliwa na wazungu what to do!
Waziri wetu wa Nje amechemsha na niko radhi kumpa darasa zito on this ishu kwa sababu I got all the dataz, na ni lazima atuheshumu wananchi wa Tanzania kbala ya kutoa maamuzi mzito kama haya bila ukweli!
Ahsante Wakuu!