Tanazania imejaa wapumbavu wengi sana,
Hiyo misikiti na makanisa inazuia vipi viwanda visijengwe? imemaliza ardhi yote kiasi kwamba wawekezaji wamekosa maeneo?
Hivi hayo makanisa na misikiti yamejengwa na serikali? na kama watu wameamua kujenga majengo yao ya ibada unataka serikali iwakataze? then wakuabudu wewe?
tutoke huko tuje kwa hao waarabu na na hija.
unadhani na hao waarabu wa leo walikaa kikao na kusema tujenga hili kaaba kwa ajili ya watu waje kila mwaka ili tufanye biashara ama kivutio cha utalii.
Hiyo KAABA imejengwa na Ibrahim ambaye hakua mwarabu kabisa, alitoka huko Iraq, sasa hebu tujiulize hao wa Iraq wananufaika vipi na hiyo ibada.
Hii ibada ya Hija,ni dunia nzima wanafaidika.Pale hujaji anakotoka nyumbani kwake,kwenda airport yenye ndege ya kwenda kwenye hija,atatumia Tax,bajaj mpaka kwenye stend ya Bus,kumpeleka kule ambako ndio kuna Airport ya safari ya hija,na akifika mji huo,kama anatoka mkoani,akienda Dar;atalala hotel,karibia wiki nzima,atalala hotel,atakula chakula,atatumia usafiri na mahitaji mengine,mote atatumia pesa,ambapo mzunguko wa pesa utakuwapo,na serekali hupata mapato yake.Na huduma zote hizo atazitumia bila kujali dini ya anayempa hizo huduma.
Kwa hiyo misikiti,ndio inayomuandaa huyu,anayekwenda hija,na pia kuna hija ndogo katika uislamu,inafanyika wakati wote wa mwaka,mbali ile ya hija kuu,ya mwaka mara moja.
Kwa hiyo hija ni uchumi wa dunia nzima,bila kujali dini ya mtu.Misikiti ni kiwanda tosha,cha kuwaandaa hawa,watumiaji wa ibada hiyo ya hija.Wanaoingiza mzunguko wa pesa,na kuingizia serekali mapato,maana matumizi yao,pamoja na tiketi,na malipo mengine ya uwanja wa ndege,tax,bus,mahotel,kula nk vyote vinalipiwa kodi.