JPM alipoingia madarakani alisema ataua vyama vya upizani hawakumuelewa, wakapiga kelele bila tafakuri Kumbe JPM alimaanisha kwa utendaji wake ifikapo 2020 hakuna atakaekuwa na Sera za kueleza kwa wananchi.
Nini Matokeo yake
Mpaka unafika mwaka wa uchaguzi Si CHADEMA, ACT Wazalendo wala CUF waliokuwa wanajua nani angesimamishwa katika nafasi ya Urais kushindana na JPM, Mpaka uchaguzi umekaribia CHADEMA wakamsimamisha LISSU, ACT Wazalendo wakamsimamisha MEMBE na CUF wakamsimamisha LIPUMBA.
Katika kampeni zinazoendeleo mgombea anayefanya kampeni kwa kiasi kikubwa ni TUNDU LISSU lakini ukimsikiliza hoja anazotoa majukwaani haziakisi maisha ya mtanzania wa kawaida anayehitaji Maji safi, Huduma za Afya bora, Kilimo cha uhakika, nk badala yake anaahidi uhuru wa kuongea, kutoa mawazo na kutoa ahadi nono bila kueleze utekelezaji wake kitendo kinacosababisha zionekane ni danganya toto.
Nini Kinaendelea sasa
Baada ya Wapinzani (CHADEMA na ACT) kuona JPM atawashinda kwa urahisi wameamua kuungana na Kumsaliti MEMBE kitendo kinacholeta sintofahamu kwa wananchi na baadhi ya wanachama.
HAKIKA kinacoendelea wapinzani kusigana siku 7 kabla ya uchaguzi ni anguko la upinzani Nchini.