Tanzania hatuna Madaktari, tuna vishoka na makasuku

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
6,373
Reaction score
16,073
Ninaliandika hili kwa tahadhari kubwa sana, natamani hata niandike kwa wino mwekundu kisha niligongelee muhuri wa mahakama ili kutilia mkazo.

Nchi hii haina madaktari wala wanaojiita wataalamu wa afya. Hawapo kabisa, hakuna hata mmoja. Nitaeleza.

Mwaka 2020 kulizuka kitu kilichopewa jina la corona. Tukapigwa timbwili la maana tukaambiwa tujifungie uvunguni hakuna kutoa pua nje, ati la sivyo tutaangamia.

Kila mtu akabaki amejibanza kama kifaranga, hata wanaojiita wataalamu wa afya wote wakafyata mikia huku wamejicha nyuma ya milango.

Kuna rafiki yangu mmoja anajiita daktari bingwa, anafanya kazi muhimbili nikamfwata nikamuuliza hili swala limekaaje, akaniambia hata wao hawajui cha kufanya, wanasubiri NOTES (MADESA) kutoka Ulaya. Bila kupewa NOTES ZA KUSOMA kutoka Ulaya hawajui cha kufanya.

Nikagundua kumbe yote wanayoyafanya na kuyaweza ni yale tu waliyoyakariri kwenye vitabu na kwenye NOTES za TWISHENI. Nasikia kuna jamaa yao wa PCB anafundishaga TWISHENI YA UDAKTARI hapo sijui mchikichini!

Kwahiyo likitokea jambo ambalo halipo kwenye NOTES ZAO za kukariri shuleni, TWAFA! Tumekwisha!

Mimi nilijua daktari ni mtu mwenye utambuzi, mwenye elimu pevu ambaye anaweza kung'amua jambo lolote kwa kadiri ya linavyokuja. Kumbe wao wanasubiri kusoma NOTES kutoka Ulaya.

Na hivi juzi, walikuwa wanasubiri kupewa NOTES kutoka WHO ili waelezwe corona ni nini! Wenyewe kama wenyewe hawawezi kufanya lolote mpaka wasome NOTES za Ulaya. Wanakwambia "tunasubiri maelekezo kutoka China".

Bila Magufuli ndugu zangu tungeangamia! Hawa wanaojiita madokta ni watu wa kutafuna mshahara tu na kujitwika makoti makubwa ya danganya toto.

Cha kushangaza, chanjo zilivyoletwa tu, wakakurupuka kwa kasi kutoka mafichoni ati wanajidai kutoa elimu kwa umma!!! Ati wanaelimisha!
 
So sad! Hivi ni kwenye kipi tunaweza kujinadi kuwa tupo serious? Naona kila sehemu ni comedy tu!
 
kwasababu hauumwi umeshiba maharage yako unajijambia tu, unatoa ushuzi tu subiri uumwe au upate ajali utuandikie tena. Kweli we ni bwege
 
Nikafikiri una hoja kumbe takataka
 
Acha dharau mkuu.....

Siku yakikufika utawafuata hawa hawa unaowakashifu sasa hivi na kwa upole, weledi na upendo watakusaidia vizuri tu.
 
Mi mwenyewe waliniacha hoi kwenye janga la uviko. Yaani madokta wakiona mgonjwa anaingia hospitali akahisiwa kuwa na uviko wote wanatoka nduki kujificha utasema mgonjwa kaingia na vilipuzi kujitoa muhanga
 
Bichwa Komwe hujui maana ya Daktari. Daktari (MD) sio kazi yake kugundua magonjwa mapya. Inakupasa ujue fani nyingine za afya kama Virology, Molecular Biology, Immunology, etc. Na hakuna maabara Tanzania za kupima hivyo unavyotaka.

Madaktari hawapigi ramli kama unavyofanya wewe unavyopima UKIMWI kwa macho akiwa mnene ananawiri unadhani hana.
 
Mbona matusi mkuu? Kwani kadanganya? Ameongea alichoshuhudia. Pia amestaajabu ikiwa alichosikia ni kweli. Kosa lipo wapi hapo?
Daktari huyo!

Mziki wa uviko umemtoa jasho, kila akichungulia NOTES zake anakuta kitu HAIMO.

Anabaki kufoka tu, mara oohh hatuna maabara, mara sijui hatuna vifaaa!

Chaaa!!
 
Umechelewa sana kujua kwamba madaktari ni watu wa kukariri na ni wagumu kufikiri nje ya kile walichokariri ikitokea kufikiri nje ya box basi wenzie watamuona wa ajabu, ni kama watu waliyofundishwa kufikiri kwa aina moja tu. Hasa kwa afrika hali ndio mbaya zaidi bora kidogo huko kwa wazungu wapo waliyoacha kukariri na wameandika hadi vitabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…