Tanzania hatuna Madaktari, tuna vishoka na makasuku

Tanzania hatuna Madaktari, tuna vishoka na makasuku

Mi mwenyewe waliniacha hoi kwenye janga la uviko. Yaani madokta wakiona mgonjwa anaingia hospitali akahisiwa kuwa na uviko wote wanatoka nduki kujificha utasema mgonjwa kaingia na vilipuzi kujitoa muhanga
Jamaa chenga sana hawa!

Hizi shule zetu tuziangalie vizuri kwa jicho la tatu!

Full ukanjanja na maigizo yaani!
 
Bichwa Komwe hujui maana ya Daktari. Daktari (MD) sio kazi yake kugundua magonjwa mapya. Inakupasa ujue fani nyingine za afya kama Virology, Molecular Biology, Immunology, etc. Na hakuna maabara Tanzania za kupima hivyo unavyotaka.

Madaktari hawapigi ramli kama unavyofanya wewe unavyopima UKIMWI kwa macho akiwa mnene ananawiri unadhani hana.
Nimeandika MADAKTARI nikimaanisha hao wote uliowataja.

Wape jina lolote unalopenda, lakini ndio hao.

Nesi, MD, virologist sijui nani, wote hao. Kwenye COVID wote walitoka nduki.
 
Daaa

Umechelewa sana kujua kwamba madaktari ni watu wa kukariri na ni wagumu kufikiri nje ya kile walichokariri ikitokea kufikiri nje ya box basi wenzie watamuona wa ajabu, ni kama watu waliyofundishwa kufikiri kwa aina moja tu. Hasa kwa afrika hali ndio mbaya zaidi bora kidogo huko kwa wazungu wapo waliyoacha kukariri na wameandika hadi vitabu.
Shida ipo.
 
Sema ndio hivyo madaktari ni kama wamepewa umungu mtu kutokana na umuhimu wao na watu kudhani jamaa wanauelewa saana, nakumbuka siku Daktari anamruhusu mgonjwa wangu arudi nyumbani et atakuwa sawa tu kwa tiba aliyompa yeye tena huku ananihakikishia kabisa kuwa baada ya muda atakuwa sawa, kama si kujiongeza na kutochukulia daktari mungu mtu basi pengine yangekuwa maafa nyumbani ila nikampeleka Amana mgonjwa akalazwa.

Wanaokoa maisha ya watu hilo halipingiki ila kuna wakati wanacheza sana uhai wa watu.
 
Ninaliandika hili kwa tahadhari kubwa sana, natamani hata niandike kwa wino mwekundu kisha niligongelee muhuri wa mahakama ili kutilia mkazo.

Nchi hii haina madaktari wala wanaojiita wataalamu wa afya. Hawapo kabisa, hakuna hata mmoja. Nitaeleza.

Mwaka 2020 kulizuka kitu kilichopewa jina la corona. Tukapigwa timbwili la maana tukaambiwa tujifungie uvunguni hakuna kutoa pua nje, ati la sivyo tutaangamia.

Kila mtu akabaki amejibanza kama kifaranga, hata wanaojiita wataalamu wa afya wote wakafyata mikia huku wamejicha nyuma ya milango.

Kuna rafiki yangu mmoja anajiita daktari bingwa, anafanya kazi muhimbili nikamfwata nikamuuliza hili swala limekaaje, akaniambia hata wao hawajui cha kufanya, wanasubiri NOTES (MADESA) kutoka Ulaya. Bila kupewa NOTES ZA KUSOMA kutoka Ulaya hawajui cha kufanya.

Nikagundua kumbe yote wanayoyafanya na kuyaweza ni yale tu waliyoyakariri kwenye vitabu na kwenye NOTES za TWISHENI. Nasikia kuna jamaa yao wa PCB anafundishaga TWISHENI YA UDAKTARI hapo sijui mchikichini!

Kwahiyo likitokea jambo ambalo halipo kwenye NOTES ZAO za kukariri shuleni, TWAFA! Tumekwisha!

Mimi nilijua daktari ni mtu mwenye utambuzi, mwenye elimu pevu ambaye anaweza kung'amua jambo lolote kwa kadiri ya linavyokuja. Kumbe wao wanasubiri kusoma NOTES kutoka Ulaya.

Na hivi juzi, walikuwa wanasubiri kupewa NOTES kutoka WHO ili waelezwe corona ni nini! Wenyewe kama wenyewe hawawezi kufanya lolote mpaka wasome NOTES za Ulaya. Wanakwambia "tunasubiri maelekezo kutoka China".

Bila Magufuli ndugu zangu tungeangamia! Hawa wanaojiita madokta ni watu wa kutafuna mshahara tu na kujitwika makoti makubwa ya danganya toto.

Cha kushangaza, chanjo zilivyoletwa tu, wakakurupuka kwa kasi kutoka mafichoni ati wanajidai kutoa elimu kwa umma!!! Ati wanaelimisha!
Aah!bichwa komwe!
 
JF mada za kuwakandia madaktari na watu wote wa taaluma za afya zinapata airtime ya kutosha sana siku hizi.

Siku hizi imekua mtu akitaka thread yake itembee lazima alete hizo mada. Kama ndugu yangu Mpwayungu Village na walimu.

Endeleeni kuponda lakini nyie na ndugu zenu mkiugua ndio hawa hawa wataalamu wa afya mnaowaponda ndio mtakaowakimbilia wawatibu. Ni asilimia chache sana kati yenu mnaoweza afford matibabu nje ya nchi, hata Kenya tu hapo.
 
Mkuu tangu niambiwe Nazi na maembe vimepimwa na kukutwa na virus vya korono nimekuwa nikijifunza Utabibu huko mjini youtube,sahizi mebakiza tu kununua koti jeupe na miwani nianze kazi.
 
Ninaliandika hili kwa tahadhari kubwa sana, natamani hata niandike kwa wino mwekundu kisha niligongelee muhuri wa mahakama ili kutilia mkazo.

Nchi hii haina madaktari wala wanaojiita wataalamu wa afya. Hawapo kabisa, hakuna hata mmoja. Nitaeleza.

Mwaka 2020 kulizuka kitu kilichopewa jina la corona. Tukapigwa timbwili la maana tukaambiwa tujifungie uvunguni hakuna kutoa pua nje, ati la sivyo tutaangamia.

Kila mtu akabaki amejibanza kama kifaranga, hata wanaojiita wataalamu wa afya wote wakafyata mikia huku wamejicha nyuma ya milango.

Kuna rafiki yangu mmoja anajiita daktari bingwa, anafanya kazi muhimbili nikamfwata nikamuuliza hili swala limekaaje, akaniambia hata wao hawajui cha kufanya, wanasubiri NOTES (MADESA) kutoka Ulaya. Bila kupewa NOTES ZA KUSOMA kutoka Ulaya hawajui cha kufanya.

Nikagundua kumbe yote wanayoyafanya na kuyaweza ni yale tu waliyoyakariri kwenye vitabu na kwenye NOTES za TWISHENI. Nasikia kuna jamaa yao wa PCB anafundishaga TWISHENI YA UDAKTARI hapo sijui mchikichini!

Kwahiyo likitokea jambo ambalo halipo kwenye NOTES ZAO za kukariri shuleni, TWAFA! Tumekwisha!

Mimi nilijua daktari ni mtu mwenye utambuzi, mwenye elimu pevu ambaye anaweza kung'amua jambo lolote kwa kadiri ya linavyokuja. Kumbe wao wanasubiri kusoma NOTES kutoka Ulaya.

Na hivi juzi, walikuwa wanasubiri kupewa NOTES kutoka WHO ili waelezwe corona ni nini! Wenyewe kama wenyewe hawawezi kufanya lolote mpaka wasome NOTES za Ulaya. Wanakwambia "tunasubiri maelekezo kutoka China".

Bila Magufuli ndugu zangu tungeangamia! Hawa wanaojiita madokta ni watu wa kutafuna mshahara tu na kujitwika makoti makubwa ya danganya toto.

Cha kushangaza, chanjo zilivyoletwa tu, wakakurupuka kwa kasi kutoka mafichoni ati wanajidai kutoa elimu kwa umma!!! Ati wanaelimisha!
Ukitaka kuamini kuwa madakitali Tanzania wapo siku ukiugua au kuuguza weka hela mezani watakuzunguka kitandani kwako kama walivyo mzunguka nyerere kama huna hela watakuhudumia wanao jifunza udakitari
 
JF mada za kuwakandia madaktari na watu wote wa taaluma za afya zinapata airtime ya kutosha sana siku hizi.

Siku hizi imekua mtu akitaka thread yake itembee lazima alete hizo mada. Kama ndugu yangu Mpwayungu Village na walimu.

Endeleeni kuponda lakini nyie na ndugu zenu mkiugua ndio hawa hawa wataalamu wa afya mnaowaponda ndio mtakaowakimbilia wawatibu. Ni asilimia chache sana kati yenu mnaoweza afford matibabu nje ya nchi, hata Kenya tu hapo.
Kwanini mlijificha wakati wa corona?

Nyinyi sio wanataaluma huru, mnakopi na kupesti!

Mambo ya TWISHENI.
 
Ukitaka kuamini kuwa madakitali Tanzania wapo siku ukiugua au kuuguza weka hela mezani watakuzunguka kitandani kwako kama walivyo mzunguka nyerere kama huna hela watakuhudumia wanao jifunza udakitari
😂😂😂😂😂😂
 
Kuishi kwenye hii dunia kwataka kuwa na akili za ziada kung'amua mambo, dunia ina uongo mwingi sana yumkini hata kuwadanganya wasomi. Wengine tuna elimu ndogo lakini suala la corona tuliliona ni upuuzi tu na lingepita ki aina. Watu wangewekwa karantini wangeumia zaidi kwa kukosa chakula kwani hakuna drone za kutosha kudondosha chakula. Chakula chenyewe kingekuwa chepesi tu cha kulambalamba na ambacho hakishibishi. Watu wengi wangepata utapiamlo kwa kukosa lishe bora ambayo hupatikana kila siku masokoni. Cha ajabu upuuzi huu uliingia mpaka nyumba za kuabudia. Pumbavu sana nisingehangaika kwenda kusali kama kungekuwa na masharti yale ya kuvaa barakoa na kukaa mbali na wenzangu hiyo isingekuwa ibada bali ni mkusanyiko wa watu wenye hofu ya kufa na Mungu hayupo hapo kamwe. Wahuni wa dunia wanaweza wakazusha hofu tena duniani wakiamua kufanya hivyo
 
Bila NOTES ZA ULAYA hutoboi wewe! I am telling you!

NOTES ndo kila kitu kwako! Kichwa kimejaa MADESA YA KIZUNGU.

Mambo ya TWISHENI
yakheee!
Sawa Kuna ukweli ila sio Kwa madaktari tu inaonekana karibia Kila sehemu yenye utaalamu tupo hivi ila serikali yetu inawawezesha kufanya tafiti hao madaktari?

Maana ni gharama kufanya tafiti ata Kwa wahandisi pia hela ya kununulia vifaa ni kubwa
 
Back
Top Bottom