Mimi ni mpenda comedy sana hasa za nje. Awali nilikuwa nikizitazama hizi za Bongo za kina Kingwendu, Majuto n.k lakini sasa natazama za nje za kina Charlie Chaplin, Buster Keaton na wengine walio hai.
Ukitazama comedy ya MC Pilipili utagundua kuwa uropokaji ndio aliojaaliwa. Akina Kingwendu pia ndo walewale maneno mengi.
Comedy za bongo hovyo sana, wengi hawana vipaji na kazi zao hazina hata uwezo wa kushindana na soko la miaka hata 25 tu ya mbele.
Akina Tiny white, Erick, Kitale, Ringo hamna kitu.
Maufundi unakuja vizuri.