Tanzania iliwahi kuwa nchi ya tatu kwa upelelezi duniani

Tanzania iliwahi kuwa nchi ya tatu kwa upelelezi duniani

Tz sio kwamba imewai kuwa ya tatu tu hata majuzi miaka kama mitano au saba tz ilishika nafasi ya kwanza

Kumbuka ni Tz peke yake ndio iliweza kufanya RAISI wa nchi nyingine awe anabadilisha makazi ya kulala kwa miezi Sita mfululizo

kwaiyo usishangae saana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wana bodi,wakati nikiwa mdogo enzi za mwalimu kuliwahi kuwa na uvumi kuwa Tanzania ilikuwa na idara nzuri sana ya TISS hata ikawa nchi ya Tatu kwa upelelezi duniani.

Kwa upande mmoja naweza kuona ukweli wa hili nikijaribu kulinganisha TISS ya enzi za Nyerere na TISS ya ezi hizi,nakumbuka wapelelezi wa enzi hizo wengine waliweza hata kuwa kama vichaa kwa kuvaa nguo chafu ili waweze kukamilisha upelelezi na wakafanikiwa hata kuwakamata makaburu waliokuwa wanakuja nchini kutoka Afrika kusini kwa njia za pori,lakini siku hizi wasomali wanaingia nchini na kutoka wachache ndo kuwa wanakamatwa tena na polisi kwa kupewa taarifa na raia wema na sio TISS.

Naomba michango yenu wana bodi kuhusu jambo hili ukilinganisha na haya matukio yanayotokea kwa sasa.

Ni kweli
 
Kuwa ya tatu inawezekana siyo kweli ila ni kweli kuwa ofisi ya usalama wa taifa ilikuwa ikijua sana kazi yake wakati huo. Kuna mtu alikuwa akiitwa Walingozi, yule bwana alikuwa siyo mchezo katika mambo ya usalama. Ni kutokana na usalama huo kuwa ingawa Nyerere alikuwa na maadui wengi matajiri, lakini walishindwa kabisa kumgusa. Kila wakijaribu mapinduzi wanakwapuliwa kabla hawajafika popote. Kwenye ile kesi ya akina Hans Pope, mmoja wa watuhumiwa (nadhani Badru Kajaja) katika testimony yake alionyesha kufadhaishwa sana kuwa plani zao zote zilipanguliwa na jamaa wa TISS katika muda ambapo ilikuwa zianze kutekelezwa kiasi kuwa wote wakachanganyikiwa wasijue namna ya kuendelea.
Naskia walikuwa wakipata ujuzi cuba na urusi... Na hizi nchi naskia wako juu sana kwenye eneo hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri neno UZALENDO liliishia huko na enzi hizo

Sent from my SM using Tapatalk
 
Ndugu wana bodi,wakati nikiwa mdogo enzi za mwalimu kuliwahi kuwa na uvumi kuwa Tanzania ilikuwa na idara nzuri sana ya TISS hata ikawa nchi ya Tatu kwa upelelezi duniani.

Kwa upande mmoja naweza kuona ukweli wa hili nikijaribu kulinganisha TISS ya enzi za Nyerere na TISS ya ezi hizi,nakumbuka wapelelezi wa enzi hizo wengine waliweza hata kuwa kama vichaa kwa kuvaa nguo chafu ili waweze kukamilisha upelelezi na wakafanikiwa hata kuwakamata makaburu waliokuwa wanakuja nchini kutoka Afrika kusini kwa njia za pori,lakini siku hizi wasomali wanaingia nchini na kutoka wachache ndo kuwa wanakamatwa tena na polisi kwa kupewa taarifa na raia wema na sio TISS.

Naomba michango yenu wana bodi kuhusu jambo hili ukilinganisha na haya matukio yanayotokea kwa sasa.

Zamani usalama wa taifa walikuwa na siri nzito yaani unaweza kulala naye kitanda kimoja usijue kuwa umelala na mwanausalama,
Lakini wa siku hizi wanajitangaza wenyewe kwenye bar na kumbi za starehe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ndi usalama wa Taifa ambao kamwe hauwezi kufananishwa na huu usalama wa mafisadi. Madudu chungu nzima kila kukicha lakini hakuna hata mmoja anayekamatwa!!! pia wameingia katika kundi la kutengeneza ushahidi fake ili waharibu maisha ya Watanzania katika juhudi zao za kukisaliti chama cha upinzani. Wako busy kuidhibiti CDM wakati nchi inawaka moto kwa matukio mbali mbali ya kutisha ambayo yanaongezeka siku hadi siku.
Mbona kila jambo linalo husu usalama wa watanzania mnazungumzia CHADEMA? Duuh basi mtakuwa mnaweweseka usijue mkilala kuwa mnatafutwa na serikali ya Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha kuonyesha ujuha wako hadharani!! Hii post ni ya 2013. 2013 huyo dhalimu na dikteta alikuwepo madarakani? Usikurupuke vinginevyo UTAUMBUKA.

Mbona kila jambo linalo husu usalama wa watanzania mnazungumzia CHADEMA? Duuh basi mtakuwa mnaweweseka usijue mkilala kuwa mnatafutwa na serikali ya Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tiss hawalali usiku na mchana kuhakikisha Tanzania inabaki salama cha ajabu watanzania ni watu tusio na heshima kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama tunakuwa wepesi kuamaini mambo ya upotoshaji uzandiki na propaganda za watu wanaotaka kujaribu kuvunja amani yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi sana. Amani inawalemaza watu. Nafikiri watakuja juta itakapo kuja wakati wa kupigana wenyewe kwa wenyewe. Wewe subiri tu Magufuli atoke.

Wengi hawajui mda huu nafikiri tungekuwa tuko hatarini kuipoteza amani yetu.

Kama sio maamuzi mazito ya Rais Magufuli sijui hii nchi ingekuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani anaivuruga nani? Umeshawahi kuona waraka kama huu kabla ya huyo dikteta na dhalimu kuingia madarakani!

Maaskofu nao wanaokota maneno vijiweni? Acha upumbavu wako wewe!

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini - JamiiForums

Back
Top Bottom