Tanzania imekuwa nchi ya matukio; hongera CCM kwa kufaulu kujenga Taifa la namna hii

Tanzania imekuwa nchi ya matukio; hongera CCM kwa kufaulu kujenga Taifa la namna hii

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Wiki chache zilizopita tulishuhudia mjadala mkali kuhusu bandari, baadaye kukaibuka tetesi za rupia kupenyezwa kwa baadhi ya wakazi wa Ufipa ili wajiondoe katika mjadala huu.

Dkt. Slaa, Dkt. Nshallah, Mwabukusi, Tundu Lissu, TEC na wananchi wengine wakaendelea kutoa elimu kuhusiana na kile kilicho sainiwa.

Way forward:
Kujadili bila kuchukua hatua ni kupoteza muda, akina Dr Slaa wakaja na wazo la maandamano yasiyo na kikomo mpaka serikali itakapofuta mkataba wa awali na kuandaa solution yenye tija.

Jana Dkt. Slaa amesikika akisema kuwa wanajaribu kuwapigia simu CHADEMA ili kuratibu hili suala lakini viongozi hawapokei simu.

Haifahamiki ni kwasababu wameweka simu silent au hawaungi mkono maandamano, kama hawaungi mkono maandamano ni vyema ila wangepokea washauri wanafikiri njia gani inafaa zaidi.

Kwa ninavyoijua hii nchi, mjadala huu umefungwa, ule wa Ngorongoro pia umefungwa, sasa tunasubiri mjadala wa wanyama kusafirishwa wakiwa hai kupelekwa Dubai ili watu wa Dubai wakawaangalie kisha warejeshwe ili kutangaza utalii kwa vitendo.

Utakapoiva tutajadili kisha tuhamie kwenye uendelezaji wa misitu yote baada ya huo 2025 itakuwa imefika, CCM ishinde kwa kishindo.
 
Mjadala wa wa Bandari umefungwa aje?

Walisikika chawa wakisema Dp World wataanza KAZI Octoba mwishoni, baadae wamesogeza mbele Hadi November mwishoni,

Mjadala wa BANDARI umemalizwa na Tamko la TEC,

Tusubiri.
 
Slaa ameanza fitina zake viongozi wetu wote hawawezi kuzima simu.

✌️
 
Zile zilikuwa kelele za vichaa tu wenye njaa.

Tulisema humu hakuna hata mtu mmoja mwenye hoja ya msingi kwenye hilo lililoitwa sakata la bandari tukaonekana wabaya! Haya sasa kiko wapi?
 
Zile zilikuwa kelele za vichaa tu wenye njaa.

Tulisema humu hakuna hata mtu mmoja mwenye hoja ya msingi kwenye hilo lililoitwa sakata la bandari tukaonekana wabaya! Haya sasa kiko wapi?
Hoja zipo sana tena hazijapata majibu lakini sisiemu wamekuwa wakifanikiwa kuzima hoja kwa kupenyeza rupia mfukoni au kupenyeza risasi mwilini
 
Back
Top Bottom