Tanzania imetimiza hatua zote 4 kuwa nchi ya kidikteta

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,888
Dikteta huchukua hatua kadhaa kupandikiza utawala wa Imla - Zitto Kabwe

(Andiko la July, 2016 na uhariri kidogo 2018. Uhariri tena mdogo Jan, 2019 )

  1. Hupambana na Wafanyabiashara wakubwa ' matajiri ' ili kuweka matajiri wake wapya watakaokuwa msaada kwake. Rais Putin wa Russia alifanya hili vizuri sana alipochukua madaraka. Adolf Hitler yeye aliamua kuwaua wayahudi (Jews) kwani wakati huo Jews ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Ujerumani. Hapa kwetu Tanzania kwa miaka mitatu tumeshuhudia Wafanyabiashara wanakipata cha mtema kuni. Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanabambikiziwa Kodi na wakibisha wanapewa kesi zisizo na dhamana, wanatupwa jela, wananyanganywa Mali zao na wengine kufilisiwa.
  2. Huteua Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Watu wake wa Karibu. Rais Vladimir Putin yeye alifuta kabisa chaguzi za Magavana na akateua majenerali wa jeshi na watu wa KGB badala yake. Hapa Tanzania tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa miungu Watu wenye kufanya lolote bila kuhojiwa na yeyote. Tumeshuhudia Wakuu wa Wilaya wakifunga watu bila kufuata sheria, wakinyang'anya watu mali zao na kila aina ya vituko bila kuchukuliwa hatua.
  3. Hudhibiti vyombo vya habari. Rais Vladimir Putin alihakikisha TV zote zinakuwa za Serikali kwa kutaifisha TV binafsi na ilikuwa marufuku DUMA (Bunge la Urusi) kuonyeshwa na ni yeye tu ndiye mwanasiasa aliyepaswa kuonekana kwenye TV. Hapa Tanzania Bunge limezuiwa kuonyeshwa moja kwa moja Lakini shughuli zote za Rais Magufuli zinaonyeshwa hata kwa masuala yasiyopaswa kuonyeshwa kama vile kusaini mikataba au mashauriano na Viongozi wa dini. Sheria ya Huduma za Habari nchini imeviweka vyombo vya Habari hatarini Katika kuchapisha au kutangaza Habari zao. Serikali imeweka kanuni za leseni ili kudhibiti kuwepo na kufanya kwao shughuli zao. Waandishi wanatekwa na kupotezwa kwa Mfano Azory Gwanda wa Gazeti la Mwananchi.
  4. Hudhibiti Vyama vya Siasa. Adolf Hitler wa alifuta vyama vyote Ujerumani. Vladimir Putin alizuia mikutano ya kisiasa na kuanzisha vyama vibaraka. Hapa Tanzania, kama tulivyotabiri katika makala Hii Mwaka 2016, “ Ndio mpango utakaofanywa Tanzania kwa kuanza na kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Sheria pia itabadilishwa na kuifanya nchi ya Chama kimoja pekee, CCM”. Hili limetokea kwa tarehe 29/1/2019 Bunge kutunga sheria ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya Siasa na kumfanya Msajili wa Vyama kuwa Mdhibiti wa Vyama vya Siasa. Utekelezaji wa sheria mpya ya vyama vya siasa utapelekea ama vyama kutii maelekezo ya Serikali au kufutwa na hivyo CCM kuhodhi siasa za nchi.
Mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kupata japo muda kidogo wa kujisomea anajua nini kinaendelea. Watu wasioona ama wana maslahi au uwezo wao wa kuona ni mdogo sana. Wengine wameamua tu kuvaa miwani za mbao. Wahanga wa Demokrasia wanajua maana ya haya tunayosema. Tanzania sasa imefunga duara ( Full Circle ) kwenye hatua Muhimu za nchi kuwa ya kidikteta.

Ni dhahiri kuwa Dunia ina madikteta wengi waliowahi kuwaletea wananchi wao maendeleo. Ethiopia. Malaysia. Singapore. Hata Rwanda. Tofauti yao na Sisi ni kwamba Madikteta wao ni wanazuoni wenye uwezo wa kutumia akili na utulivu kufanya maamuzi. Madikteta wao wanasoma vitabu na majarida ya uchambuzi wa sera. Rais Paul Kagame wa Rwanda hakosi Harvard Business Review. Meles alikuwa na akili Kama mchwa mpaka wazungu walikuwa wanamwogopa na kitu cha kwanza alichoomba kupewa Kama msaada ni ' vitabu vya uchumi'. Hata hivyo tunashuhudia Ethiopia ikifuta sheria kandamizi na kuelekea kwenye barabara ya Demokrasia baada ya kuona uimla haulipi.Lee Kuan Yew wa Singapore na Mahathir Mohammed wa Malaysia ni waandishi wazuri wa vitabu. Hawa sio too technical...... Ni Intellectuals.

Pamoja na kuwa hao niliowataja wanasoma na wenye MAARIFA Mengi, Bado udikteta haukuwasaidia sana na wengi wamebadilika na kuwa wana Demokrasia.

( last edit 30/1/2019 )
 
Kosa kubwa mnalofanya Upinzani ni kumtenganisha Magufuli na CCM, wengine hata mnaifanyia CCM promo kwa kumsifia Kikwete kwamba alifanya mazuri TZ mnachoshindwa kuelewa ni kwamba 2020/25 Kikwete ataikampenia CCM Magufuli ataenda atakuja mwingine lkn bado atakuwa ni CCM hivyo mtarudi tena hapa kuanza moja na kumchukia pia mwishowe hakuna mahali mnaenda.

Tuliona mlimchukia Mwinyi, Mkapa, hata Kikwete na sasa Magufuli.

Hivyo mkitaka mfanikiwe ni lazima mumjue adui yenu, na Adui yenu siyo Magufuli kwani huo Mswada ungepita hata kama Raisi asingekuwa Magufuli.
 
Udikteta ni relative.

Kuna wengine wanaweza kusema hata wewe ni dikteta ndani ya ACT-Wazalendo kwa sababu cheo chako hakina tofauti na Supreme Leader of Iran. Sayyid Ali Hosseini Khamenei

Acheni kulisha wananchi matango ya kisiasa.

Udikteta upi unaosema katika mazingira ya kuweza kusema serikali ya sasa inaongozwa na dikteta!
 
Hapa kazi TU nyie endeleeni kubwabwaja lakini sisi wengine tunashuhudia MAENDELEO..tunaona miundombinu inavyojengwa usiku na mchana..hizi stori nyingine sijui za udikteta sijui za demokrasia sisi hatuna mpango nazo..tulizisoma TU shuleni huko kwa Sasa tuko busy kumsaidia Rais kujenga nchi kwa kufanya kazi tupate na hela ya kula.na inapatikana ukifanya kazi unapata hela usipofanya hupati fullstop
 
Dikteta huchukua hatua kadhaa kupandikiza utawala wa Imla - Zitto Kabwe

( Andiko la July, 2016 na uhariri kidogo 2018. Uhariri tena mdogo Jan, 2019 )

  1. Hupambana na Wafanyabiashara wakubwa ' matajiri ' ili kuweka matajiri wake wapya watakaokuwa msaada kwake. Rais Putin wa Russia alifanya hili vizuri sana alipochukua madaraka. Adolf Hitler yeye aliamua kuwaua wayahudi ( Jews ) kwani wakati huo Jews ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Ujerumani. Hapa kwetu Tanzania kwa miaka mitatu tumeshuhudia Wafanyabiashara wanakipata cha mtema kuni. Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanabambikiziwa Kodi na wakibisha wanapewa kesi zisizo na dhamana, wanatupwa jela, wananyanganywa Mali zao na wengine kufilisiwa.
  2. Huteua Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Watu wake wa Karibu. Rais Vladimir Putin yeye alifuta kabisa chaguzi za Magavana na akateua majenerali wa jeshi na watu wa KGB badala yake. Hapa Tanzania tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa miungu Watu wenye kufanya lolote bila kuhojiwa na yeyote. Tumeshuhudia Wakuu wa Wilaya wakifunga watu bila kufuata sheria, wakinyanganya watu mali zao na kila aina ya vituko bila kuchukuliwa hatua.
  3. Hudhibiti vyombo vya habari. Rais Vladimir Putin alihakikisha TV zote zinakuwa za Serikali kwa kutaifisha TV binafsi na ilikuwa marufuku DUMA ( Bunge la Urusi) kuonyeshwa na ni yeye tu ndiye mwanasiasa aliyepaswa kuonekana kwenye TV. Hapa Tanzania Bunge limezuiwa kuonyeshwa moja kwa moja Lakini shughuli zote za Rais Magufuli zinaonyeshwa hata kwa masuala yasiyopaswa kuonyeshwa kama vile kusaini mikataba au mashauriano na Viongozi wa dini. Sheria ya Huduma za Habari nchini imeviweka vyombo vya Habari hatarini Katika kuchapisha au kutangaza Habari zao. Serikali imeweka kanuni za leseni ili kudhibiti kuwepo na kufanya kwao shughuli zao. Waandishi wanatekwa na kupotezwa kwa Mfano Azory Gwanda wa Gazeti la Mwananchi.

Hon Zito , here are somemore characteristics:
10 Ways to Tell if Your President Is a Dictator

BY STEPHEN M. WALT

1. Systematic efforts to intimidate the media.

2. Building an official pro-President media network eg Musiba, Tanzanite kijarida etc

3. Politicizing the civil service, military, National Guard, or the domestic security agencies.

4. Using government surveillance against domestic political opponents.

5. Using state power to reward corporate backers and punish opponents.

6. Stacking the juduciary.

7. Enforcing the law for only one side.

8. Really rigging the system.

9. Fear mongering.

10. Demonizing the opposition.

We need your presentation on this!
 
Kosa kubwa mnalofanya Upinzani ni kumtenganisha Magufuli na CCM, wengine hata mnaifanyia CCM promo kwa kumsifia Kikwete kwamba alifanya mazuri TZ mnachoshindwa kuelewa ni kwamba 2020/25 Kikwete ataikampenia CCM Magufuli ataenda atakuja mwingine lkn bado atakuwa ni CCM hivyo mtarudi tena hapa kuanza moja na kumchukia pia mwishowe hakuna mahali mnaenda.

Tuliona mlimchukia Mwinyi, Mkapa, hata Kikwete na sasa Magufuli.

Hivyo mkitaka mfanikiwe ni lazima mumjue adui yenu, na Adui yenu siyo Magufuli kwani huo Mswada ungepita hata kama Raisi asingekuwa Magufuli.
Ubaya huu ushauri umetoka Nazareti na kwavile wapo waliokariri kuwa jambo jema haliwezi kutoka Nazareti watakupuuza .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dikteta huchukua hatua kadhaa kupandikiza utawala wa Imla - Zitto Kabwe

( Andiko la July, 2016 na uhariri kidogo 2018. Uhariri tena mdogo Jan, 2019 )

  1. Hupambana na Wafanyabiashara wakubwa ' matajiri ' ili kuweka matajiri wake wapya watakaokuwa msaada kwake. Rais Putin wa Russia alifanya hili vizuri sana alipochukua madaraka. Adolf Hitler yeye aliamua kuwaua wayahudi ( Jews ) kwani wakati huo Jews ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Ujerumani. Hapa kwetu Tanzania kwa miaka mitatu tumeshuhudia Wafanyabiashara wanakipata cha mtema kuni. Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanabambikiziwa Kodi na wakibisha wanapewa kesi zisizo na dhamana, wanatupwa jela, wananyanganywa Mali zao na wengine kufilisiwa.
  2. Huteua Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Watu wake wa Karibu. Rais Vladimir Putin yeye alifuta kabisa chaguzi za Magavana na akateua majenerali wa jeshi na watu wa KGB badala yake. Hapa Tanzania tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa miungu Watu wenye kufanya lolote bila kuhojiwa na yeyote. Tumeshuhudia Wakuu wa Wilaya wakifunga watu bila kufuata sheria, wakinyanganya watu mali zao na kila aina ya vituko bila kuchukuliwa hatua.
  3. Hudhibiti vyombo vya habari. Rais Vladimir Putin alihakikisha TV zote zinakuwa za Serikali kwa kutaifisha TV binafsi na ilikuwa marufuku DUMA ( Bunge la Urusi) kuonyeshwa na ni yeye tu ndiye mwanasiasa aliyepaswa kuonekana kwenye TV. Hapa Tanzania Bunge limezuiwa kuonyeshwa moja kwa moja Lakini shughuli zote za Rais Magufuli zinaonyeshwa hata kwa masuala yasiyopaswa kuonyeshwa kama vile kusaini mikataba au mashauriano na Viongozi wa dini. Sheria ya Huduma za Habari nchini imeviweka vyombo vya Habari hatarini Katika kuchapisha au kutangaza Habari zao. Serikali imeweka kanuni za leseni ili kudhibiti kuwepo na kufanya kwao shughuli zao. Waandishi wanatekwa na kupotezwa kwa Mfano Azory Gwanda wa Gazeti la Mwananchi.
  4. Hudhibiti Vyama vya Siasa. Adolf Hitler wa alifuta vyama vyote Ujerumani. Vladimir Putin alizuia mikutano ya kisiasa na kuanzisha vyama vibaraka. Hapa Tanzania, kama tulivyotabiri katika makala Hii Mwaka 2016, “ Ndio mpango utakaofanywa Tanzania kwa kuanza na kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Sheria pia itabadilishwa na kuifanya nchi ya Chama kimoja pekee, CCM”. Hili limetokea kwa tarehe 29/1/2019 Bunge kutunga sheria ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya Siasa na kumfanya Msajili wa Vyama kuwa Mdhibiti wa Vyama vya Siasa. Utekelezaji wa sheria mpya ya vyama vya siasa utapelekea ama vyama kutii maelekezo ya Serikali au kufutwa na hivyo CCM kuhodhi siasa za nchi.

Mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kupata japo muda kidogo wa kujisomea anajua nini kinaendelea. Watu wasioona ama wana maslahi au uwezo wao wa kuona ni mdogo sana. Wengine wameamua tu kuvaa miwani za mbao. Wahanga wa Demokrasia wanajua maana ya haya tunayosema. Tanzania sasa imefunga duara ( Full Circle ) kwenye hatua Muhimu za nchi kuwa ya kidikteta.

Ni dhahiri kuwa Dunia ina madikteta wengi waliowahi kuwaletea wananchi wao maendeleo. Ethiopia. Malaysia. Singapore. Hata Rwanda. Tofauti yao na Sisi ni kwamba Madikteta wao ni wanazuoni wenye uwezo wa kutumia akili na utulivu kufanya maamuzi. Madikteta wao wanasoma vitabu na majarida ya uchambuzi wa sera. Rais Paul Kagame wa Rwanda hakosi Harvard Business Review. Meles alikuwa na akili Kama mchwa mpaka wazungu walikuwa wanamwogopa na kitu cha kwanza alichoomba kupewa Kama msaada ni ' vitabu vya uchumi'. Hata hivyo tunashuhudia Ethiopia ikifuta sheria kandamizi na kuelekea kwenye barabara ya Demokrasia baada ya kuona uimla haulipi.Lee Kuan Yew wa Singapore na Mahathir Mohammed wa Malaysia ni waandishi wazuri wa vitabu. Hawa sio too technical...... Ni Intellectuals.

Pamoja na kuwa hao niliowataja wanasoma na wenye MAARIFA Mengi, Bado udikteta haukuwasaidia sana na wengi wamebadilika na kuwa wana Demokrasia.

( last edit 30/1/2019 )
Zitooooo! Tatizo lako Mh. huwa huangalii kama ufahamu wako ni wa kweli. Najua sasa hivi una presha ya uchaguzi wa mwakani na huenda ungeomba haraka ya mageuzi ili mwakani yasikukute. Tatizo uliifanya siasa kama taaluma kumbe sivyo, na sasa unaanza kuona mwisho wake. Just be calm!

Nikuulize swali la tangu zamani; Ni nchi gani iliendelea kwa sababu ya demokrasia? Nitajie moja tu, ili nasi tuone unatumia ubongo wako. Sasa angalia unatumia historia iliyopindishwa. Hitler hakuwachukia wayahudi kwa sababu ya utajili wao kama unavyodanganya. Wapi uliona uongo wa aina hiyo au unasikia hadithi za mtaani? Ipo sababu moja muhimu kabisa ya Hitler ambayo si yeye peke yake kuwahi kuitumia, ilitumika na nchi nyingi za ulaya iliyostaarabika leo hii.

Pia, elewa kwamba Vyama vingi vya siasa ni muhimu lakini siyo lazima viwepo, na kutokuwepo siyo udikteta. Au kutokuwepo siyo kwamba maendeleo hayatakuja. China kuna vyama vingapi, Mheshimiwa? Nchi gani ina uchumi unaokuwa kwa haraka kuliko China? Unaleta nadhalia ya kianazuoni wakati huiwezi. Huna uzoefu wa hoja kama hizi, braza!
 
Na kama putin ni dikteta ambaye amemudu ushindani dhidi ya Marekani na Urusi iko juu kiteknolojia, bora na sisi tuwe na dikteta kuliko kuruhu kelele kila siku kwa kisingizio cha demokrasia.

Urusi ilipoteza ushawishi kipindi cha Mikhail Gorbachev ambaye alikuwa pandikizi la USA, ila baada ya hapo Putini ameisimamisha tena Nguvu ya Urusi duniani.

Hatutaki demokrasia za kila siku mikutano kulaghai wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kazi TU nyie endeleeni kubwabwaja lakini sisi wengine tunashuhudia MAENDELEO..tunaona miundombinu inavyojengwa usiku na mchana..hizi stori nyingine sijui za udikteta sijui za demokrasia sisi hatuna mpango nazo..tulizisoma TU shuleni huko kwa Sasa tuko busy kumsaidia Rais kujenga nchi kwa kufanya kazi tupate na hela ya kula.na inapatikana ukifanya kazi unapata hela usipofanya hupati fullstop

Hizo shule zinazofundisha ujinga angali top 10 ya shule bora kama kuna shule ya bure pale
Tanzania safari ya maendeleo utachukua karne nyingi kukiwa na watu sampuli yako
Shame on you!
 
Kosa kubwa mnalofanya Upinzani ni kumtenganisha Magufuli na CCM, wengine hata mnaifanyia CCM promo kwa kumsifia Kikwete kwamba alifanya mazuri TZ mnachoshindwa kuelewa ni kwamba 2020/25 Kikwete ataikampenia CCM Magufuli ataenda atakuja mwingine lkn bado atakuwa ni CCM hivyo mtarudi tena hapa kuanza moja na kumchukia pia mwishowe hakuna mahali mnaenda.

Tuliona mlimchukia Mwinyi, Mkapa, hata Kikwete na sasa Magufuli.

Hivyo mkitaka mfanikiwe ni lazima mumjue adui yenu, na Adui yenu siyo Magufuli kwani huo Mswada ungepita hata kama Raisi asingekuwa Magufuli.

Hilo baadhi yetu tumeshawaambia sana lakini wapi! Watu wenyewe hawajielewi.
 
Kosa kubwa mnalofanya Upinzani ni kumtenganisha Magufuli na CCM, wengine hata mnaifanyia CCM promo kwa kumsifia Kikwete kwamba alifanya mazuri TZ mnachoshindwa kuelewa ni kwamba 2020/25 Kikwete ataikampenia CCM Magufuli ataenda atakuja mwingine lkn bado atakuwa ni CCM hivyo mtarudi tena hapa kuanza moja na kumchukia pia mwishowe hakuna mahali mnaenda.

Tuliona mlimchukia Mwinyi, Mkapa, hata Kikwete na sasa Magufuli.

Hivyo mkitaka mfanikiwe ni lazima mumjue adui yenu, na Adui yenu siyo Magufuli kwani huo Mswada ungepita hata kama Raisi asingekuwa Magufuli.
Afadhali umesaidia watu kumjua adui wa Tanzania kuwa ni CCM.
 
Zito ulizoea awamu ya nne kupewa hela za burebure na mashirika, sasa zimekata unahangaika. You are facing the reality, na 2025 ubunge hutoupata tena. Tuache JPM anatenda kazi kwa kasi kwa faida ya watanzania. Nakushauri tubu urudi nyumbani , PAMENOGA. Watanzania wazalendo tupo na Mhe. Rais, Tanzania yenye neema inakuja.
 
Fanyaa
Udikteta ni relative.

Kuna wengine wanaweza kusema hata wewe ni dikteta ndani ya ACT-Wazalendo kwa sababu cheo chako hakina tofauti na Supreme Leader of Iran. Sayyid Ali Hosseini Khamenei

Acheni kulisha wananchi matango ya kisiasa.

Udikteta upi unaosema katika mazingira ya kuweza kusema serikali ya sasa inaongozwa na dikteta!

Fanya kwanza wema nyumbani kwako kabla ya kwenda kwa jirani!
 
Back
Top Bottom