othuman dan fodio
JF-Expert Member
- Jan 2, 2018
- 6,850
- 11,033
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu mbona mvivu hivyo kupindukia? Hii ni moja ya makala fupi kabisa na nmesoma chini ya dakika 5 na nakubaliana na Mh Zitto.Jizoeshe kusoma makala ndefu ili ujifunze vitu kwa ufasaha maana makala hizi ndefu ndio huchimba mpaka ndaniNdefu nitaishoma lunch time
Dikteta huchukua hatua kadhaa kupandikiza utawala wa Imla - Zitto Kabwe
( Andiko la July, 2016 na uhariri kidogo 2018. Uhariri tena mdogo Jan, 2019 )
- Hupambana na Wafanyabiashara wakubwa ' matajiri ' ili kuweka matajiri wake wapya watakaokuwa msaada kwake. Rais Putin wa Russia alifanya hili vizuri sana alipochukua madaraka. Adolf Hitler yeye aliamua kuwaua wayahudi ( Jews ) kwani wakati huo Jews ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Ujerumani. Hapa kwetu Tanzania kwa miaka mitatu tumeshuhudia Wafanyabiashara wanakipata cha mtema kuni. Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanabambikiziwa Kodi na wakibisha wanapewa kesi zisizo na dhamana, wanatupwa jela, wananyanganywa Mali zao na wengine kufilisiwa.
- Huteua Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Watu wake wa Karibu. Rais Vladimir Putin yeye alifuta kabisa chaguzi za Magavana na akateua majenerali wa jeshi na watu wa KGB badala yake. Hapa Tanzania tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa miungu Watu wenye kufanya lolote bila kuhojiwa na yeyote. Tumeshuhudia Wakuu wa Wilaya wakifunga watu bila kufuata sheria, wakinyanganya watu mali zao na kila aina ya vituko bila kuchukuliwa hatua.
- Hudhibiti vyombo vya habari. Rais Vladimir Putin alihakikisha TV zote zinakuwa za Serikali kwa kutaifisha TV binafsi na ilikuwa marufuku DUMA ( Bunge la Urusi) kuonyeshwa na ni yeye tu ndiye mwanasiasa aliyepaswa kuonekana kwenye TV. Hapa Tanzania Bunge limezuiwa kuonyeshwa moja kwa moja Lakini shughuli zote za Rais Magufuli zinaonyeshwa hata kwa masuala yasiyopaswa kuonyeshwa kama vile kusaini mikataba au mashauriano na Viongozi wa dini. Sheria ya Huduma za Habari nchini imeviweka vyombo vya Habari hatarini Katika kuchapisha au kutangaza Habari zao. Serikali imeweka kanuni za leseni ili kudhibiti kuwepo na kufanya kwao shughuli zao. Waandishi wanatekwa na kupotezwa kwa Mfano Azory Gwanda wa Gazeti la Mwananchi.
- Hudhibiti Vyama vya Siasa. Adolf Hitler wa alifuta vyama vyote Ujerumani. Vladimir Putin alizuia mikutano ya kisiasa na kuanzisha vyama vibaraka. Hapa Tanzania, kama tulivyotabiri katika makala Hii Mwaka 2016, “ Ndio mpango utakaofanywa Tanzania kwa kuanza na kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Sheria pia itabadilishwa na kuifanya nchi ya Chama kimoja pekee, CCM”. Hili limetokea kwa tarehe 29/1/2019 Bunge kutunga sheria ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya Siasa na kumfanya Msajili wa Vyama kuwa Mdhibiti wa Vyama vya Siasa. Utekelezaji wa sheria mpya ya vyama vya siasa utapelekea ama vyama kutii maelekezo ya Serikali au kufutwa na hivyo CCM kuhodhi siasa za nchi.
Mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kupata japo muda kidogo wa kujisomea anajua nini kinaendelea. Watu wasioona ama wana maslahi au uwezo wao wa kuona ni mdogo sana. Wengine wameamua tu kuvaa miwani za mbao. Wahanga wa Demokrasia wanajua maana ya haya tunayosema. Tanzania sasa imefunga duara ( Full Circle ) kwenye hatua Muhimu za nchi kuwa ya kidikteta.
Ni dhahiri kuwa Dunia ina madikteta wengi waliowahi kuwaletea wananchi wao maendeleo. Ethiopia. Malaysia. Singapore. Hata Rwanda. Tofauti yao na Sisi ni kwamba Madikteta wao ni wanazuoni wenye uwezo wa kutumia akili na utulivu kufanya maamuzi. Madikteta wao wanasoma vitabu na majarida ya uchambuzi wa sera. Rais Paul Kagame wa Rwanda hakosi Harvard Business Review. Meles alikuwa na akili Kama mchwa mpaka wazungu walikuwa wanamwogopa na kitu cha kwanza alichoomba kupewa Kama msaada ni ' vitabu vya uchumi'. Hata hivyo tunashuhudia Ethiopia ikifuta sheria kandamizi na kuelekea kwenye barabara ya Demokrasia baada ya kuona uimla haulipi.Lee Kuan Yew wa Singapore na Mahathir Mohammed wa Malaysia ni waandishi wazuri wa vitabu. Hawa sio too technical...... Ni Intellectuals.
Pamoja na kuwa hao niliowataja wanasoma na wenye MAARIFA Mengi, Bado udikteta haukuwasaidia sana na wengi wamebadilika na kuwa wana Demokrasia.
( last edit 30/1/2019 )
Jakaya Kikwete hii lawama itamfuata hadi kaburiniBaada ya kukamilisha kuupitisha huu mswaada naona Jiwe kaadvance kutoka dikteta uchwara kwenda dikteta kamili .
Kwamba Magufuli ni mchapa kazi na anapambana kuwainua watanzania kiuchumi.Hakika ukweli utazidi kuonekana
Bado unahangaikia hela ya kule karne hii, badala ya kuhangaikia pesa ya maendeleo? Kweli tunapishana mitazamo!Hapa kazi TU nyie endeleeni kubwabwaja lakini sisi wengine tunashuhudia MAENDELEO..tunaona miundombinu inavyojengwa usiku na mchana..hizi stori nyingine sijui za udikteta sijui za demokrasia sisi hatuna mpango nazo..tulizisoma TU shuleni huko kwa Sasa tuko busy kumsaidia Rais kujenga nchi kwa kufanya kazi tupate na hela ya kula.na inapatikana ukifanya kazi unapata hela usipofanya hupati fullstop
Nape Nnauye alikuwa na kejeli kukuzidi .Kwamba Magufuli ni mchapa kazi na anapambana kuwainua watanzania kiuchumi.
Naona wewe ni wale wale, ungekuwa una muda kidogo wa kusoma madikteta wa Duniani usingeandika Hata.Kosa kubwa mnalofanya Upinzani ni kumtenganisha Magufuli na CCM, wengine hata mnaifanyia CCM promo kwa kumsifia Kikwete kwamba alifanya mazuri TZ mnachoshindwa kuelewa ni kwamba 2020/25 Kikwete ataikampenia CCM Magufuli ataenda atakuja mwingine lkn bado atakuwa ni CCM hivyo mtarudi tena hapa kuanza moja na kumchukia pia mwishowe hakuna mahali mnaenda.
Tuliona mlimchukia Mwinyi, Mkapa, hata Kikwete na sasa Magufuli.
Hivyo mkitaka mfanikiwe ni lazima mumjue adui yenu, na Adui yenu siyo Magufuli kwani huo Mswada ungepita hata kama Raisi asingekuwa Magufuli.
Kweli kwa mujibu wa madai/maandiko yale ya Ben Saanaane,jamaa kweli ni genius.We ZZK, unapowasifu Mahathir Mohammed na Lee Kun Yew kuwa ni waandishi wa vitabu, hata wa kwetu pia ni mwandishi mzuri tuu wa thesis ya kemia Ben Saanane aliileta humu, hivyo kuwa mwandishi sii hoja.
Unapomsifu Kagame na Meles kuwa ni wasomi wazuri wa Havard Bussiness Review-Journal, hata wa kwetu ni msomi mzuri wa JF.
The truth, is JPM ni genius.
P
Well said mkuu, lakini kabla ya kufika bungeni kuna mchakato ulifanyika. Nani alitoa wazo la mswada huo? Hata hivyo bunge likipitisha sio lazima Rais asaini. Hivyo, asisaini huo mswada ili kuonyesha tatizo ni bunge sio yeye!Kosa kubwa mnalofanya Upinzani ni kumtenganisha Magufuli na CCM, wengine hata mnaifanyia CCM promo kwa kumsifia Kikwete kwamba alifanya mazuri TZ mnachoshindwa kuelewa ni kwamba 2020/25 Kikwete ataikampenia CCM Magufuli ataenda atakuja mwingine lkn bado atakuwa ni CCM hivyo mtarudi tena hapa kuanza moja na kumchukia pia mwishowe hakuna mahali mnaenda.
Tuliona mlimchukia Mwinyi, Mkapa, hata Kikwete na sasa Magufuli.
Hivyo mkitaka mfanikiwe ni lazima mumjue adui yenu, na Adui yenu siyo Magufuli kwani huo Mswada ungepita hata kama Raisi asingekuwa Magufuli.
Unataka akafanyie Chumbani kwa mama yako akiwa anamduu! Mmetufunga mikono Nyuma na Policcm na TISS yenu mnataka wakaongelee wapi na hali ninyi mnakampein kila eneo! Lakini mwisho wenu Utakuwa Mbaya!Siasa za mtandaoni zimeshakuchanganya.
Hapa kazi TU nyie endeleeni kubwabwaja lakini sisi wengine tunashuhudia MAENDELEO..tunaona miundombinu inavyojengwa usiku na mchana..hizi stori nyingine sijui za udikteta sijui za demokrasia sisi hatuna mpango nazo..tulizisoma TU shuleni huko kwa Sasa tuko busy kumsaidia Rais kujenga nchi kwa kufanya kazi tupate na hela ya kula.na inapatikana ukifanya kazi unapata hela usipofanya hupati fullstop
Hivi uyu ni mwenyekiti katika kamati yoyote ya bunge kwenye utawala JPM?Zito ulizoea awamu ya nne kupewa hela za burebure na mashirika, sasa zimekata unahangaika. You are facing the reality, na 2025 ubunge hutoupata tena. Tuache JPM anatenda kazi kwa kasi kwa faida ya watanzania. Nakushauri tubu urudi nyumbani , PAMENOGA. Watanzania wazalendo tupo na Mhe. Rais, Tanzania yenye neema inakuja.