Tanzania imetimiza hatua zote 4 kuwa nchi ya kidikteta

Hapa kazi TU nyie endeleeni kubwabwaja lakini sisi wengine tunashuhudia MAENDELEO..tunaona miundombinu inavyojengwa usiku na mchana..hizi stori nyingine sijui za udikteta sijui za demokrasia sisi hatuna mpango nazo..tulizisoma TU shuleni huko kwa Sasa tuko busy kumsaidia Rais kujenga nchi kwa kufanya kazi tupate na hela ya kula.na inapatikana ukifanya kazi unapata hela usipofanya hupati fullstop
Leo tunanunua dola kwa 2330 tunazidi kupaa kiuchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitooooo! Tatizo lako Mh. huwa huangalii kama ufahamu wako ni wa kweli. Najua sasa hivi una presha ya uchaguzi wa mwakani na huenda ungeomba haraka ya mageuzi ili mwakani yasikukute. Tatizo uliifanya siasa kama taaluma kumbe sivyo, na sasa unaanza kuona mwisho wake. Just be calm!

Nikuulize swali la tangu zamani; Ni nchi gani iliendelea kwa sababu ya demokrasia? Nitajie moja tu, ili nasi tuone unatumia ubongo wako. Sasa angalia unatumia historia iliyopindishwa. Hitler hakuwachukia wayahudi kwa sababu ya utajili wao kama unavyodanganya. Wapi uliona uongo wa aina hiyo au unasikia hadithi za mtaani? Ipo sababu moja muhimu kabisa ya Hitler ambayo si yeye peke yake kuwahi kuitumia, ilitumika na nchi nyingi za ulaya iliyostaarabika leo hii.

Pia, elewa kwamba Vyama vingi vya siasa ni muhimu lakini siyo lazima viwepo, na kutokuwepo siyo udikteta. Au kutokuwepo siyo kwamba maendeleo hayatakuja. China kuna vyama vingapi, Mheshimiwa? Nchi gani ina uchumi unaokuwa kwa haraka kuliko China? Unaleta nadhalia ya kianazuoni wakati huiwezi. HUna uzoefu wa hoja kama hizi, braza!
Nakupigia makofi.
Tatizo la kina Zitto sababu wameona watanzania wengi wanatekwa kiurahisi na propaganda basi wamewekeza huko, wasichojua uongo una mipaka yake.

Hivi Kati ya Mbowe, Zitto na Maghufuli nani ni dikteta? Ukiwa kiongozi wa CCM ni dhahiri kuna ukomo, tena bila ubishi. Lakini jaribu kuhoji ukomo wa Mbowe au Zitto uoni cha moto!

Wnachojifanya kusahau ni kwamba Maghufuli ni chaguo la watanzania kupitia kura, ana ridhaa yetu kutuongoza. Akileta vya kuleta uchaguzi ujao tunamuondoa.

Lakini dalili za wazi zinaonyesha anatekeleza ahadi za uchaguzi. Ndiyo maana kwenye mikutano yake na wasomi wa Chuo kikuu, viongozi wa dini, wafanyabiashara, wadau wa madini inaonyesha hao wanamkubali. Sasa hilo wao wanaligeuza eti anazima sauti zao!

Mtu akionyesha kumkosoa Maghufuli wao wanaona ndiyo demokrasia!
 
Naona wewe ni wale wale, ungekuwa una muda kidogo wa kusoma madikteta wa Duniani usingeandika Hata.

Baath Party ya Iraqi uliifahami, je chama cha Hitrer unakijua kilianzaje? Je wanachama kama wewe washanhiliaji waliendelea kushangilia?

Mmezidiwa akili na mtu mmoja ambaye nahisi alitakiwa asiwazidi, sidhani kama ana IQ kubwa kuzidi wengiwenu, msichotaka kukiri ni kuwa kama tinavyo shughulikiwa sisi wapimzani nyie mmejazwa hofu, mkija kustuka ntakuwa mmechelewa hamtaweza kufanya chochote

Hata wewe ni kama Zito Kabwe much know lkn hakuna kitu mnajua, unafikiri Hitler ndiye mwanzilishi wa nazism? Au unafikiri aliyeuwa Wayahudi ni Hitler peke yake?
Nazism ni ideology ya white supremacy ambayo ilikuwepo kabla hata ya Hitler hajazaliwa, fascism ilianzia Italia hata Jengo la House of Representatives - USA, lina nembo ya fascism, nembo ambayo pia ilitumiwa na Mussolini na A.Hitler na hii ni kabla hata ya Hitler, unajua ni kwa nini?
 
Well said mkuu, lakini kabla ya kufika bungeni kuna mchakato ulifanyika. Nani alitoa wazo la mswada huo? Hata hivyo bunge likipitisha sio lazima Rais asaini. Hivyo, asisaini huo mswada ili kuonyesha tatizo ni bunge sio yeye!

Kwa nini unataka Raisi anayetokana na Chama cha CCM afanye kazi ya Upinzani? Labda pia nikuulize kwa nini Upinzani hawakuuzuia Bungeni usipite?
 
Dikteta huchukua hatua kadhaa kupandikiza utawala wa Imla - Zitto Kabwe

( Andiko la July, 2016 na uhariri kidogo 2018. Uhariri tena mdogo Jan, 2019 )

  1. Hupambana na Wafanyabiashara wakubwa ' matajiri ' ili kuweka matajiri wake wapya watakaokuwa msaada kwake. Rais Putin wa Russia alifanya hili vizuri sana alipochukua madaraka. Adolf Hitler yeye aliamua kuwaua wayahudi ( Jews ) kwani wakati huo Jews ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Ujerumani. Hapa kwetu Tanzania kwa miaka mitatu tumeshuhudia Wafanyabiashara wanakipata cha mtema kuni. Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanabambikiziwa Kodi na wakibisha wanapewa kesi zisizo na dhamana, wanatupwa jela, wananyanganywa Mali zao na wengine kufilisiwa.
  2. Huteua Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Watu wake wa Karibu. Rais Vladimir Putin yeye alifuta kabisa chaguzi za Magavana na akateua majenerali wa jeshi na watu wa KGB badala yake. Hapa Tanzania tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa miungu Watu wenye kufanya lolote bila kuhojiwa na yeyote. Tumeshuhudia Wakuu wa Wilaya wakifunga watu bila kufuata sheria, wakinyanganya watu mali zao na kila aina ya vituko bila kuchukuliwa hatua.
  3. Hudhibiti vyombo vya habari. Rais Vladimir Putin alihakikisha TV zote zinakuwa za Serikali kwa kutaifisha TV binafsi na ilikuwa marufuku DUMA ( Bunge la Urusi) kuonyeshwa na ni yeye tu ndiye mwanasiasa aliyepaswa kuonekana kwenye TV. Hapa Tanzania Bunge limezuiwa kuonyeshwa moja kwa moja Lakini shughuli zote za Rais Magufuli zinaonyeshwa hata kwa masuala yasiyopaswa kuonyeshwa kama vile kusaini mikataba au mashauriano na Viongozi wa dini. Sheria ya Huduma za Habari nchini imeviweka vyombo vya Habari hatarini Katika kuchapisha au kutangaza Habari zao. Serikali imeweka kanuni za leseni ili kudhibiti kuwepo na kufanya kwao shughuli zao. Waandishi wanatekwa na kupotezwa kwa Mfano Azory Gwanda wa Gazeti la Mwananchi.
  4. Hudhibiti Vyama vya Siasa. Adolf Hitler wa alifuta vyama vyote Ujerumani. Vladimir Putin alizuia mikutano ya kisiasa na kuanzisha vyama vibaraka. Hapa Tanzania, kama tulivyotabiri katika makala Hii Mwaka 2016, “ Ndio mpango utakaofanywa Tanzania kwa kuanza na kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Sheria pia itabadilishwa na kuifanya nchi ya Chama kimoja pekee, CCM”. Hili limetokea kwa tarehe 29/1/2019 Bunge kutunga sheria ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya Siasa na kumfanya Msajili wa Vyama kuwa Mdhibiti wa Vyama vya Siasa. Utekelezaji wa sheria mpya ya vyama vya siasa utapelekea ama vyama kutii maelekezo ya Serikali au kufutwa na hivyo CCM kuhodhi siasa za nchi.

Mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kupata japo muda kidogo wa kujisomea anajua nini kinaendelea. Watu wasioona ama wana maslahi au uwezo wao wa kuona ni mdogo sana. Wengine wameamua tu kuvaa miwani za mbao. Wahanga wa Demokrasia wanajua maana ya haya tunayosema. Tanzania sasa imefunga duara ( Full Circle ) kwenye hatua Muhimu za nchi kuwa ya kidikteta.

Ni dhahiri kuwa Dunia ina madikteta wengi waliowahi kuwaletea wananchi wao maendeleo. Ethiopia. Malaysia. Singapore. Hata Rwanda. Tofauti yao na Sisi ni kwamba Madikteta wao ni wanazuoni wenye uwezo wa kutumia akili na utulivu kufanya maamuzi. Madikteta wao wanasoma vitabu na majarida ya uchambuzi wa sera. Rais Paul Kagame wa Rwanda hakosi Harvard Business Review. Meles alikuwa na akili Kama mchwa mpaka wazungu walikuwa wanamwogopa na kitu cha kwanza alichoomba kupewa Kama msaada ni ' vitabu vya uchumi'. Hata hivyo tunashuhudia Ethiopia ikifuta sheria kandamizi na kuelekea kwenye barabara ya Demokrasia baada ya kuona uimla haulipi.Lee Kuan Yew wa Singapore na Mahathir Mohammed wa Malaysia ni waandishi wazuri wa vitabu. Hawa sio too technical...... Ni Intellectuals.

Pamoja na kuwa hao niliowataja wanasoma na wenye MAARIFA Mengi, Bado udikteta haukuwasaidia sana na wengi wamebadilika na kuwa wana Demokrasia.

( last edit 30/1/2019 )
Sasa mkuu Zitto hebu tuongozeni, tunapaswa kufanya nini? Na hivi kuna dikteta asiyekuwa na military background aliyewahi kufanikiwa kweli?
 
Hata wewe ni kama Zito Kabwe much know lkn hakuna kitu mnajua, unafikiri Hitler ndiye mwanzilishi wa nazism? Au unafikiri aliyeuwa Wayahudi ni Hitler peke yake?
Nazism ni ideology ya white supremacy ambayo ilikuwepo kabla hata ya Hitler hajazaliwa, fascism ilianzia Italia hata Jengo la Senate la USA lina nembo ya fascism na hii ni kabla hata ya Hitler kuzaliwa, unajua ni kwa nini?
Sasa ndo unasema nini? Kwani aliyesema huyu dikteta wa kihutu ataua watu peke yake ni nani, si ataua kwa kusaidiana na nyinyi wapuuzi wenzake mnaomsaidia kutunga hizi sheria za kipumbavu?
 
Hii nchi ni kichekesho cha kipekee, unaanzisha uzi kuhusu udikteta na unasomwa na watu!.

Nchi za kidikteta unaweza hata kuanzisha uzi na ukapata mrejesho wa jamii?.
 
Zitooooo! Tatizo lako Mh. huwa huangalii kama ufahamu wako ni wa kweli. Najua sasa hivi una presha ya uchaguzi wa mwakani na huenda ungeomba haraka ya mageuzi ili mwakani yasikukute. Tatizo uliifanya siasa kama taaluma kumbe sivyo, na sasa unaanza kuona mwisho wake. Just be calm!

Nikuulize swali la tangu zamani; Ni nchi gani iliendelea kwa sababu ya demokrasia? Nitajie moja tu, ili nasi tuone unatumia ubongo wako. Sasa angalia unatumia historia iliyopindishwa. Hitler hakuwachukia wayahudi kwa sababu ya utajili wao kama unavyodanganya. Wapi uliona uongo wa aina hiyo au unasikia hadithi za mtaani? Ipo sababu moja muhimu kabisa ya Hitler ambayo si yeye peke yake kuwahi kuitumia, ilitumika na nchi nyingi za ulaya iliyostaarabika leo hii.

Pia, elewa kwamba Vyama vingi vya siasa ni muhimu lakini siyo lazima viwepo, na kutokuwepo siyo udikteta. Au kutokuwepo siyo kwamba maendeleo hayatakuja. China kuna vyama vingapi, Mheshimiwa? Nchi gani ina uchumi unaokuwa kwa haraka kuliko China? Unaleta nadhalia ya kianazuoni wakati huiwezi. HUna uzoefu wa hoja kama hizi, braza!
Mkuu Patriot, zipo zile akili ambazo siku nyingi zimesalimu amri kwa matakwa ya wenye kututawala kiuchumi.

Pia zipo akili zenye kujitegemea bila ya kujali wale wanaotutawala wanawaza nini. Tofauti kwa maoni yangu ipo hapo.
 
Hizi ngonjera tumezoea kuziskia kila awamu ya uongozi,uliokuwepo madarakani.
Hata sasa hakuna jpya,tulianza kwa tundu lisu akidai Rais n dictecta,kwa sasa yy ndo anataka urais na ww unakuja na ngojnera zilezile,tutaskia ukitangaza nia kutaka urais.

Siasa mchezo mchafu.
Kuutaka urais kuna uhusiano gani na kupinga udikteta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimiwa umeelezea mada yako kwa kina, na kama kawaida wapo wanaokuunga mkono na wapo pia wanaokupinga kwa hoja na hata pia kwa vijembe na kejeli za kila aina!

Ombi langu kwako; ungemalizia mada yako kwa kutoa na hitimisho. Nini kifanyike kwa mwananchi wa kawaida na Taifa kwa ujumla kwa hayo yote uliyoeleza? Kinyume na hapo wadau wengine wasiogemea upande wowote tutaona ni mwendelezo tu wa siasa na wale wa upande pendwa wataona ni kelele tu za chura!
Kwani siasa haziruhusu kutoa maoni na mapendekezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wewe ni kama Zito Kabwe much know lkn hakuna kitu mnajua, unafikiri Hitler ndiye mwanzilishi wa nazism? Au unafikiri aliyeuwa Wayahudi ni Hitler peke yake?
Nazism ni ideology ya white supremacy ambayo ilikuwepo kabla hata ya Hitler hajazaliwa, fascism ilianzia Italia hata Jengo la Senate la USA lina nembo ya fascism na hii ni kabla hata ya Hitler kuzaliwa, unajua ni kwa nini?
Stick kwenye realism sio theories, unajua Hitler alishindikana kudhibitiwa kwa sababu ya waimba mapambio kama wewe?

Call a spade spade ndugu, muda ni mwalimu nzuri, hebu hifadhi hii post yangu then kabla ya miaka miwili utaelewa ninachokueleza maana kitakuwa dhahili
 
Zitto Kabwe, kuna mambo mengi hayajui sababu ya uchanga:-
(i). Inapaswa afahamu kwamba wakati wa shida nyingi ndio wakati wa kujenga misingi imara kwa ajili ya kizazi kijacho; (Kama USA kusingekuwapo na mitafaruku kati ya watu weupe na weusi - leo hii sijui USA ingekuwaje - Hivyo migogoro baina ya White vs Black people ulikuwa ufunguo wa misingi imara ya kidemokrasia USA - Swali muhimu ni njia ipi inapaswa kutumiwa na Watanzania ili kumaliza migogoro hiyo ya kivyama);

(ii). Uhakika na Usahihi wa njia za kupata suluhu:- hapa lazima taasisi zinazoona kwamba zinaonewa zifahamu njia sahihi za muda wa kati za kupata suluhu katika maeneo yote yenye shida - kama kunakuwa na mwanya wa mazungumzo basi utumiwe kwa hali na mali kufikia muafaka wa mivutano - iwapo hakuna njia hii ya mazungumzo itashindikana basi alikeni viongozi wawakilishi wa kimataifa kusaidia kupata suluhu ( )
 
Stick kwenye realism sio theories, unajua Hitler alishindikana kudhibitiwa kwa sababu ya waimba mapambio kama wewe?

Call a spade spade ndugu, muda ni mwalimu nzuri, hebu hifadhi hii post yangu then kabla ya miaka miwili utaelewa ninachokueleza maana kitakuwa dhahili

Hitler alishindikana kudhibitiwa na nani?
 
Hata wewe ni kama Zito Kabwe much know lkn hakuna kitu mnajua, unafikiri Hitler ndiye mwanzilishi wa nazism? Au unafikiri aliyeuwa Wayahudi ni Hitler peke yake?
Nazism ni ideology ya white supremacy ambayo ilikuwepo kabla hata ya Hitler hajazaliwa, fascism ilianzia Italia hata Jengo la Senate la USA lina nembo ya fascism na hii ni kabla hata ya Hitler kuzaliwa, unajua ni kwa nini?
Isikilize Hitler's starngrad speech utaelewa nani alianzisha Nazism.
 
Dikteta huchukua hatua kadhaa kupandikiza utawala wa Imla - Zitto Kabwe

( Andiko la July, 2016 na uhariri kidogo 2018. Uhariri tena mdogo Jan, 2019 )

  1. Hupambana na Wafanyabiashara wakubwa ' matajiri ' ili kuweka matajiri wake wapya watakaokuwa msaada kwake. Rais Putin wa Russia alifanya hili vizuri sana alipochukua madaraka. Adolf Hitler yeye aliamua kuwaua wayahudi ( Jews ) kwani wakati huo Jews ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Ujerumani. Hapa kwetu Tanzania kwa miaka mitatu tumeshuhudia Wafanyabiashara wanakipata cha mtema kuni. Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanabambikiziwa Kodi na wakibisha wanapewa kesi zisizo na dhamana, wanatupwa jela, wananyanganywa Mali zao na wengine kufilisiwa.
  2. Huteua Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Watu wake wa Karibu. Rais Vladimir Putin yeye alifuta kabisa chaguzi za Magavana na akateua majenerali wa jeshi na watu wa KGB badala yake. Hapa Tanzania tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa miungu Watu wenye kufanya lolote bila kuhojiwa na yeyote. Tumeshuhudia Wakuu wa Wilaya wakifunga watu bila kufuata sheria, wakinyanganya watu mali zao na kila aina ya vituko bila kuchukuliwa hatua.
  3. Hudhibiti vyombo vya habari. Rais Vladimir Putin alihakikisha TV zote zinakuwa za Serikali kwa kutaifisha TV binafsi na ilikuwa marufuku DUMA ( Bunge la Urusi) kuonyeshwa na ni yeye tu ndiye mwanasiasa aliyepaswa kuonekana kwenye TV. Hapa Tanzania Bunge limezuiwa kuonyeshwa moja kwa moja Lakini shughuli zote za Rais Magufuli zinaonyeshwa hata kwa masuala yasiyopaswa kuonyeshwa kama vile kusaini mikataba au mashauriano na Viongozi wa dini. Sheria ya Huduma za Habari nchini imeviweka vyombo vya Habari hatarini Katika kuchapisha au kutangaza Habari zao. Serikali imeweka kanuni za leseni ili kudhibiti kuwepo na kufanya kwao shughuli zao. Waandishi wanatekwa na kupotezwa kwa Mfano Azory Gwanda wa Gazeti la Mwananchi.
  4. Hudhibiti Vyama vya Siasa. Adolf Hitler wa alifuta vyama vyote Ujerumani. Vladimir Putin alizuia mikutano ya kisiasa na kuanzisha vyama vibaraka. Hapa Tanzania, kama tulivyotabiri katika makala Hii Mwaka 2016, “ Ndio mpango utakaofanywa Tanzania kwa kuanza na kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Sheria pia itabadilishwa na kuifanya nchi ya Chama kimoja pekee, CCM”. Hili limetokea kwa tarehe 29/1/2019 Bunge kutunga sheria ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya Siasa na kumfanya Msajili wa Vyama kuwa Mdhibiti wa Vyama vya Siasa. Utekelezaji wa sheria mpya ya vyama vya siasa utapelekea ama vyama kutii maelekezo ya Serikali au kufutwa na hivyo CCM kuhodhi siasa za nchi.

Mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kupata japo muda kidogo wa kujisomea anajua nini kinaendelea. Watu wasioona ama wana maslahi au uwezo wao wa kuona ni mdogo sana. Wengine wameamua tu kuvaa miwani za mbao. Wahanga wa Demokrasia wanajua maana ya haya tunayosema. Tanzania sasa imefunga duara ( Full Circle ) kwenye hatua Muhimu za nchi kuwa ya kidikteta.

Ni dhahiri kuwa Dunia ina madikteta wengi waliowahi kuwaletea wananchi wao maendeleo. Ethiopia. Malaysia. Singapore. Hata Rwanda. Tofauti yao na Sisi ni kwamba Madikteta wao ni wanazuoni wenye uwezo wa kutumia akili na utulivu kufanya maamuzi. Madikteta wao wanasoma vitabu na majarida ya uchambuzi wa sera. Rais Paul Kagame wa Rwanda hakosi Harvard Business Review. Meles alikuwa na akili Kama mchwa mpaka wazungu walikuwa wanamwogopa na kitu cha kwanza alichoomba kupewa Kama msaada ni ' vitabu vya uchumi'. Hata hivyo tunashuhudia Ethiopia ikifuta sheria kandamizi na kuelekea kwenye barabara ya Demokrasia baada ya kuona uimla haulipi.Lee Kuan Yew wa Singapore na Mahathir Mohammed wa Malaysia ni waandishi wazuri wa vitabu. Hawa sio too technical...... Ni Intellectuals.

Pamoja na kuwa hao niliowataja wanasoma na wenye MAARIFA Mengi, Bado udikteta haukuwasaidia sana na wengi wamebadilika na kuwa wana Demokrasia.

( last edit 30/1/2019 )
ZZK: Ifike wakati mkajifunza kuwa wakweli.
Tanzania hakujawa na huo udikteta unaotaka kutuaminisha.

Siku chache zilizopita Tanganyka Law Society ilikuwa na mkutano kujadili mswaada mpya wa vyama vya siasa. Kama kungekuwa na udikteta unaousema, mkutano ule usingefanyika.

Mara kadhaa tunaona watu wa civil society na vyama vya siasa vikiwa na mikutano ya vyombo vya habari (press conference), tungekuwa ni nchi ya kidikteta, yote hayo yasingafanyika.

Mara ngapi, watu wengi wanamkosoa Rais kupitia majarida na machapisho mbali mbali na hawabughudhiwi. Isipokuwa wale tu ambao wanadhalilisha taasisi ya Urais, sheria imekuwa ikichukua mkondo wake. Hayo yamekuwepo hata enzi za JK.

Ni wakati umefika, ZZK na wenzako mjipambanue kama wanasiasa wenye kupigania maslahi mapana ya Taifa na sio "kunenepesha wallet" zenu.

JPM anatupeleka katika viwango sahihi. Ikiweza kufuata nyayo za akina Lew Kuan Yew wa Singapore na Mahathir Mohamed wa Malyasia, kwa rasimali ambazo Tanzania inazo, tunaweza kupaa kiuchumi na kuwa nchi ya dunia ya kwanza.

Kufikia kiwango cha dunia ya kwanza kitawezekana kwani Rais wetu (JPM) yuko focused. Akina ZZK wana lengo mahsusi ya kutengeneza distraction kupitia porojo nyepesi. The good thing JPM is very intellectual, strategic and tactical skills to ensure his mission to take Tanzanianis to the promise land is realized.
 
Na taifa zima la ujerumani plus acomplises plus his own party.

Unafahamu kwamba A. Hitler alishinda Uchaguzi Ujerumani? Unafahamu kwamba the rise of A.Hitler kulisaidiwa na USA akiwemo baba yake HW Bush aliyeitwa Prescot Bush? Unafahamu Ulaya yote pamoja na English monarchy walisapoti nazism?

Unafahamu apartheid AK ni ideology ya nazism na ilisapotiwa na Muzungu wote USA na Ulaya? Unafahamu Mandela alikuwa kwenye orodha ya terrorist USA?
Unafikiri ni kwa nini Mandela alitambulika kama terrorist na USA?
 
Back
Top Bottom