Dikteta huchukua hatua kadhaa kupandikiza utawala wa Imla - Zitto Kabwe
( Andiko la July, 2016 na uhariri kidogo 2018. Uhariri tena mdogo Jan, 2019 )
- Hupambana na Wafanyabiashara wakubwa ' matajiri ' ili kuweka matajiri wake wapya watakaokuwa msaada kwake. Rais Putin wa Russia alifanya hili vizuri sana alipochukua madaraka. Adolf Hitler yeye aliamua kuwaua wayahudi ( Jews ) kwani wakati huo Jews ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Ujerumani. Hapa kwetu Tanzania kwa miaka mitatu tumeshuhudia Wafanyabiashara wanakipata cha mtema kuni. Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanabambikiziwa Kodi na wakibisha wanapewa kesi zisizo na dhamana, wanatupwa jela, wananyanganywa Mali zao na wengine kufilisiwa.
- Huteua Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Watu wake wa Karibu. Rais Vladimir Putin yeye alifuta kabisa chaguzi za Magavana na akateua majenerali wa jeshi na watu wa KGB badala yake. Hapa Tanzania tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa miungu Watu wenye kufanya lolote bila kuhojiwa na yeyote. Tumeshuhudia Wakuu wa Wilaya wakifunga watu bila kufuata sheria, wakinyanganya watu mali zao na kila aina ya vituko bila kuchukuliwa hatua.
- Hudhibiti vyombo vya habari. Rais Vladimir Putin alihakikisha TV zote zinakuwa za Serikali kwa kutaifisha TV binafsi na ilikuwa marufuku DUMA ( Bunge la Urusi) kuonyeshwa na ni yeye tu ndiye mwanasiasa aliyepaswa kuonekana kwenye TV. Hapa Tanzania Bunge limezuiwa kuonyeshwa moja kwa moja Lakini shughuli zote za Rais Magufuli zinaonyeshwa hata kwa masuala yasiyopaswa kuonyeshwa kama vile kusaini mikataba au mashauriano na Viongozi wa dini. Sheria ya Huduma za Habari nchini imeviweka vyombo vya Habari hatarini Katika kuchapisha au kutangaza Habari zao. Serikali imeweka kanuni za leseni ili kudhibiti kuwepo na kufanya kwao shughuli zao. Waandishi wanatekwa na kupotezwa kwa Mfano Azory Gwanda wa Gazeti la Mwananchi.
- Hudhibiti Vyama vya Siasa. Adolf Hitler wa alifuta vyama vyote Ujerumani. Vladimir Putin alizuia mikutano ya kisiasa na kuanzisha vyama vibaraka. Hapa Tanzania, kama tulivyotabiri katika makala Hii Mwaka 2016, “ Ndio mpango utakaofanywa Tanzania kwa kuanza na kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Sheria pia itabadilishwa na kuifanya nchi ya Chama kimoja pekee, CCM”. Hili limetokea kwa tarehe 29/1/2019 Bunge kutunga sheria ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya Siasa na kumfanya Msajili wa Vyama kuwa Mdhibiti wa Vyama vya Siasa. Utekelezaji wa sheria mpya ya vyama vya siasa utapelekea ama vyama kutii maelekezo ya Serikali au kufutwa na hivyo CCM kuhodhi siasa za nchi.
Mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kupata japo muda kidogo wa kujisomea anajua nini kinaendelea. Watu wasioona ama wana maslahi au uwezo wao wa kuona ni mdogo sana. Wengine wameamua tu kuvaa miwani za mbao. Wahanga wa Demokrasia wanajua maana ya haya tunayosema. Tanzania sasa imefunga duara ( Full Circle ) kwenye hatua Muhimu za nchi kuwa ya kidikteta.
Ni dhahiri kuwa Dunia ina madikteta wengi waliowahi kuwaletea wananchi wao maendeleo. Ethiopia. Malaysia. Singapore. Hata Rwanda. Tofauti yao na Sisi ni kwamba Madikteta wao ni wanazuoni wenye uwezo wa kutumia akili na utulivu kufanya maamuzi. Madikteta wao wanasoma vitabu na majarida ya uchambuzi wa sera. Rais Paul Kagame wa Rwanda hakosi Harvard Business Review. Meles alikuwa na akili Kama mchwa mpaka wazungu walikuwa wanamwogopa na kitu cha kwanza alichoomba kupewa Kama msaada ni ' vitabu vya uchumi'. Hata hivyo tunashuhudia Ethiopia ikifuta sheria kandamizi na kuelekea kwenye barabara ya Demokrasia baada ya kuona uimla haulipi.Lee Kuan Yew wa Singapore na Mahathir Mohammed wa Malaysia ni waandishi wazuri wa vitabu. Hawa sio too technical...... Ni Intellectuals.
Pamoja na kuwa hao niliowataja wanasoma na wenye MAARIFA Mengi, Bado udikteta haukuwasaidia sana na wengi wamebadilika na kuwa wana Demokrasia.
( last edit 30/1/2019 )
ZZK: Ifike wakati mkajifunza kuwa wakweli.
Tanzania hakujawa na huo udikteta unaotaka kutuaminisha.
Siku chache zilizopita Tanganyka Law Society ilikuwa na mkutano kujadili mswaada mpya wa vyama vya siasa. Kama kungekuwa na udikteta unaousema, mkutano ule usingefanyika.
Mara kadhaa tunaona watu wa civil society na vyama vya siasa vikiwa na mikutano ya vyombo vya habari (press conference), tungekuwa ni nchi ya kidikteta, yote hayo yasingafanyika.
Mara ngapi, watu wengi wanamkosoa Rais kupitia majarida na machapisho mbali mbali na hawabughudhiwi. Isipokuwa wale tu ambao wanadhalilisha taasisi ya Urais, sheria imekuwa ikichukua mkondo wake. Hayo yamekuwepo hata enzi za JK.
Ni wakati umefika, ZZK na wenzako mjipambanue kama wanasiasa wenye kupigania maslahi mapana ya Taifa na sio "kunenepesha wallet" zenu.
JPM anatupeleka katika viwango sahihi. Ikiweza kufuata nyayo za akina Lew Kuan Yew wa Singapore na Mahathir Mohamed wa Malyasia, kwa rasimali ambazo Tanzania inazo, tunaweza kupaa kiuchumi na kuwa nchi ya dunia ya kwanza.
Kufikia kiwango cha dunia ya kwanza kitawezekana kwani Rais wetu (JPM) yuko focused. Akina ZZK wana lengo mahsusi ya kutengeneza distraction kupitia porojo nyepesi. The good thing JPM is very intellectual, strategic and tactical skills to ensure his mission to take Tanzanianis to the promise land is realized.