Tanzania imetimiza hatua zote 4 kuwa nchi ya kidikteta



OK basi sana, naona umekuwa emotional sana!
 
So what? Hivi unadhani udikteta una madhara kwa chadema tu, nani kakudanganya? Katika mfumo wa udikteta hata wewe hauko salama , ndugu zako hawako salama.
Iko siku utayakumbuka haya maneno. Hoja hapa siyo kwamba udikteta unafanywa na nani , ni chama kizima au mtu mmoja , hoja hapa ni kwamba udikteta haufai mahali popote duniani bila kujali nani anaufanya.

Narudia tena mkuu wala usishangilie hili kwani hauko salama hata kidogo. Siku zinakuja tena kwa kasi ya mwanga utakuja kuona madhara ya huu mfumo ambao Leo unaushabikia.

Naomba niwaambie wasomaji humu Leo , katika vitu ambavyo havipaswi kufanyiwa ushabiki na mtu yeyote yule mwenye akili timamu labda kichaa ni udikteta.

Udikteta unaumiza , unatesa, unaleta ukiwa , udikteta huleta umasikini , na matatizo makubwa ya uchumi katika jamii. Jamii husinyaa na kuwa kama maua yaliyokosa maji na mwanga wa jua.

Mungu wa mbinguni atusadie tuione kweli na hiyo kweli ituweke huru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unafanya exaggeration, usiwe muoga. Hakuna mtu anayefungwa kwa kusema eti kipaumbele ni ndege, sio kweli.

Wanaofungwa au kukamatwa ni wale wanaojisahau na kumtusi matusi ya nguoni mheshimiwa rais kwenye facebook au twitter. Ukweli anaambiwa ila tatizo tunataka tuwe huru mno wakati wa kuusema huo ukweli kiasi cha kuuchanganya na matusi au kejeli.
 

Mosi, nimeiweka Uchina hapo kuaonesha kwamba hata wao wanakubali kwamba uhuru wa kiuchumi ni msingi wa maendeleo ya taifa lolote lile. Uchina ya leo ya Xi Jinping ni ya kidikteta lakini sehemu bora zaidi kuishi kuliko ile Uchina ya Mao Zedong ambayo kuwa tajiri ilikuwa ni dhambi. Kadiri siku zinavyoenda Uchina itabadilika na kuwa ni nchi inayokubaliana na mifumo ya kidemokrasia kutokana na nafasi yake kimataifa.

Pili, kwenye tafsiri ya neno demokrasia hakuna kitu kinachoitwa chama cha siasa. Kama nilivyosema kwa mdau moja hapa, Democracy is Janus Faced: It's not only a political system but also a value. Vyama vya kisiasa ni mifumo tuliyojiwekea ili kuweza kuishi kidemokrasia. Na tulifanya hivi baada ya kuona Direct Democracy haiwezekani kwa nchi kubwa za dunia ya leo, hivyo vyama vikawa kama njia mbadala wa Representative Democracy. Hivyo tusipoheshimu vyama tutakuwa hatuwapi watu sehemu ya kusemea mawazo yao.

Tatu, demokrasia ya Ugiriki na Roma hazikuwa na vyama vya siasa kutokana na mifumo yao ya uzalishaji waliyokuwa nayo kipindi hicho. Ambapo Roma walikuwa na mfumo wa Utumwa au Slavery Mode of Production na Ugiriki nao walikuwa na Slavery Mode of Production. Demokrasia ilikuwa ni kwa ajili ya watwana na siyo watumwa. Watumwa hawakuhesabiwa ka watu. Lakini katika dunia yetu ya leo ya utandawazi na ubepari ambapo suati ya kila mtu ina umuhimu, unadhani tukitoa vyama vya siasa na kukataza watu wasiseme tutaweza kweli kufika ? (Nakuanchia hili ulifikirie)

Upande mwingine nakubaliana na wewe kabisa kwamba vyama vingi haviashiriii uwepo wa demokrasia kama hivyo vyama haviwasaidii watu. Nchini Congo DRC kuna vyama vya siasa zaidi ya 20 lakini kuna vurugu kila siku. Marekani vyama vyenye nguvu ni viwili kama ilivyo nchini Uingereza lakini bado kuna demokrasia. Hivyo vyama visitupumbaze sana.

Kinadharia na tukichukua mfano wa Uchina chama kimoja ndicho mfumo bora kabisa wakuwasaidia wananchi kupata maendeleo kwasababu kwa nchi yenye chama kimoja ni rahisi sana kufanya mabadiliko ya sera na sheria kuliko nchi zenye vyama vingi. Mijadala inakuwepo mingi isiyo na maana: Angalia leo Marekani hadi wamefunga serikali yao kisa tu ugomvi wa Trump na Democrats. Kitu kama hichi uchina hakipo kabisa.

Nchini Tanzania, vyama vya siasa vimeonyesha umuhimu wake mkubwa sana. Hivi unadhani bila CHADEMA kuwepo Raisi Jakaya na genge lake la wakina Lowassa si wangekuwa washauza nchi yote hii kwa wazungu, wachina na waarabu! Leo tumejua ufisadi uliokuwepo serikalini kwasababu ya vyama vya upinzani. Nakubaliana na wewe kwamba kuna wakati hivi vyama vinavuka mipaka lakini ndiyo tutake visiwepo kabisa ?? Raisi Magufuli anataka kufanya maovu gani avichukie hivi vyama ??

Mwisho, Mimi siyo msemaji wa Zitto wala ACT wala mwanasiasa yoyote yule lakini jana bungeni nilimwelewa sana kwasababu hata Plato aliwahi kusema hivi "Human Rights are inherent entitlements which enable the development of human faculties" kwamba bila haki ya kusoma (Right to education) huwezi kufanya uvumbuzi (Innovation). Mimi narudia tena kwamba haki za binadami ni zinaendana sambamba na haki za binadamu na uhuru wa kiuchumi ni sehemu ya haki ya binadamu. Huwezi kuvitenga hivi vitu hata siku moja. Tunatafuta demokrasia ili tuweze kulinda haki zetu za kisiasa na kiuchumi. Nifahamuvyo mimi, Uhuru wa kiuchumi ni sehemu ya demokrasia.

Hayo mengine ya Zitto kuwa pretender mimi hayanihusu kabisa. I just discuss facts on the table hata kama zimetoka kwa kunguru, mwewe au nguruwe.
 
Basi kama ni hivyo kulikuwa na haja gani ya kukataza tusitazame shughuli zote za bunge letu ?? Kulikuwa na haja gani ya kupitisha ule muswada ambao unamfanya Msajili wa vyama vya siasa kuingilia shughuli za siasa moja kwa moja with impunity without any sense of responsibility ?? Hadi kufika kumtishia CAG kwa kufanya kazi yake kisheria, haya yanatoka wapi ??
 
CAG hajatishwa, yeye mwenyewe alichemka kule USA kwa kuongea jambo bila ya kujua kuwa kinga ina mipaka yake.

Bunge kuonyeshwa live au kutoonyeshwa ina impact gani katika utendaji wa kazi wa mbunge mmoja mmoja?.

Msajili kuingilia shughuli za siasa ni baada ya kuona uhuru mkubwa wa vyama vya siasa unatengeneza wapigaji wa ruzuku na madikteta ambao wakija JF wanaongelea udikteta wa chama kingine yaani yale yale ya nyani kutoona sehemu zake zile za nyuma.
 

Mosi, Spika hana mamlaka ya kumpa subpoena CAG. Hajawahi kuwa nayo, hana na wala haji kuwa nayo: Kusema utakuja kwa pingu ule ulikuwa ni upumbavu na ukosefu wa hekima kwa mtu mwenye nafasi kama spika.

Pili, kuhusu Bunge live mimi ninaongela haki ya wananchi kupata taarifa kuhusu utendaji wa Serikali yao na siongelei swala la utendaji wa mbunge moja moja. Ni haki yangu mimi kama mwananchi wa kawaida kuona nini kichoendelea bungeni. Pesa yangu inatumika kufanya serikali iwepo.

Tatu, narudia tena kusema hivi, kisheria na kisiasa udikteta upo kwenye ngazi ya kitaifa pekee na siyo kichama: Kichama hakuwezi kuwepo na udikteta wakati mtu anakuwa na uhuru wa kuendelea kuwepo au kutokuwepo ndani ya chama ambacho anakipenda au hakipendi. Kitaifa udikteta upo kwasababu hata kama hukubaliani na Serikali wewe bado uko nayo tu 27/7/365.
 
Mkuu ukiwa mfuata sheria pasipo shuruti hakuna udikteta. Hakuna nchi inayoweza kupiga hatua ya kimaendeleo pasipo nidhamu.

Wewe kulipa kodi sio kigezo cha kuiamulia serikali irushe matangazo ya bunge au la. Kila mlipa akiwa anaamua nini cha kuonyesha kwenye runinga hakuna sababu ya kuwa na wakurugenzi wa mashirika ya runinga.

CAG hakuwa na sababu ya kusema bunge dhaifu nje ya bunge, alishindwa nini kuutamka udhaifu huo ndani ya bunge ili ufanyiwe kazi?.
 
Katika yote uliyoyasema, na single out kitu muhimu cha kuomba. Lazima kuwe na chama cha siasa chenye nguvu ili CCM iwe na adabu. Dunia hii hakuna mtu mwema bila kuwa na woga wa kilicho juu yake. Hakika CCM ingebaki bila upinzani, tungekoma. Hii ni kwa sababu CCM haijawahi kuwa na watu bora kiasi hicho na imeendelea kuwa na watu wa ubora duni kwa muda mrefu. Central system yake alikaliwa na wanenguaji badala ya thinkers. That's fine! Lakini upinzamni tulionao sasa hivi umehama.

Sina hakika kwamba kweli Rais anataka kuondoa upinzani, na siamini pia kwamba upinzani huu ndo ule nilioushuhudia ukiongozwa na Slaa? Maturity imeondoka kabisa na nionacho ni frustrations. Kwa akili ya kawaida kabisa usingetegemea chama kama CHADEMA kiwe na viongozi wa maono ya kiwango kile kwa sasa. Wanasingizia kununuliwa lakini anayenunuliwa atakuwa na kiwango cha chini tangu mwanzo.

Sasa angalia mwanzo wa thrd hii, argument za Zito anakodhani ni kuonyesha muelekeo wa siasa za TZ. Mifano anayoitoa ni ya kizembe na haiwezi ku-apply TZ. Huo ndo mwanzo wa mchango wangu na hasa anapoingiza na mambo ya uongo ya akina Hitler na wayahudi. Hitler alishakuwa kama ndo mfano wa failure lakini ukweli aliyoyafanya, nchi nyingi za ulaya pia ziliyafanya!
 
ZITO KAA DAWATI LA MBELE UISOME NAMBA VIZURI.
JPM WANYOOSHE HATA KWA MIJELEDI.
Tena nataka nikagombee uenyekiti ACT Wazalendo. Wenyewe wanaendesha vyama hivi vya upinzani kidikiteta wengine mpaka vinawafia mkononi ....Siasa sisi bado sana [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Tatizo langu juu ya mamlaka ya Bunge imekuwa ni pale ambapo Bunge linaisimamia serikali na kuikosoa lakini, haliko tayari kusimamiwa na kuosolewa na mwananchi. Linajipa madaraka ya kukuita na kukupiga pingu. Kwa sasa ilivyo, kama mwananchi yeyote anavyoitwa na spika kufika kujieleza, hata CAG hana kinga hiyo. CAG amekingwa akiwa ktk utendaji wake lakini siyo anapokuwa mitaani Kariakoo au New York. Hapo alichemka kwa kuwa uwezo wa kukosoa utendaji wa Bunge anao na angeweza kuuweka katika ripoti yake ili Bunge lijirekebishe.

Alichokifanya ni kulikosoa bunge juu ya linavyoifanyiakazi ripoti yake. Hiyo haikubaliki hata tumtetee namna gani!
 
Swali dogo kwako mhe zito

Nini kifanyike kunusuru hali hii? Maana muda si mrefu utasikia katiba inabadilishwa kipengere cha ukomo wa rais, which can be taken as the measures?
Muulize commando kilichompata ZNZ ..acheni uoga atafyekelewa mbali.
Tanzania sio vinchi vya pembezoni Rwanda ,Uganda na Burundi
 
Na bado unaandika mambo kama haya katika nchi ya Kidikteta.
 

Leo umezungumza (andika) kichwa na akili vikiwa upright...

Sijawahi kukupa LIKE, kwa comment hii nimekupa na ofcoz nakubaliana na wewe ingalau kwa hili....

Nahisisi mara nyingine uamkapo akili zako huwa unaziacha juu ya godoro kitandani na kutoka na mwili tu na safari hii, umejisahau, umeamka na vyote.....

Shikamoo, and welcome to the world....!!!
 
Hama nchi Zitto kama unaona nchi ni ya kidikteta. Kwani lazima uishi kwenye nchi hii.
 
Kwamba macho huna ?! Hata masikio nayo hayafanyi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Udikteta ni time bomb. Likilipuka nchi husika huishia kuwa kifusi na mizoga. Tatizo akili ya mtu mweusi inatia mashaka sana. Kuna baadhi ya watu wakipewa mamlaka hujiona kama wao ni miungu. Hawa ndio watakaoweka doa la milele kwa watu wengine. Sishangai reference za umaskini, marathi na ujinga ni kwa watu weusi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili za simbachawene hizi dunia ina nchi 200+ ila mfano ni nchi 1 china.
Nchi 200+! Hongera. wewe toa mifano hiyo achana na mifano ya mwingine. Sema nchi ipi imeendelea kwa vyama vingi. Singapore ya Lee Kuan ilikuwa na vyama vingapi?
 
Tatizo siyo CCM bali kiongozi. Ndiyo maana kila akija kiongozi mpya anakuja na mambo yake mapya. Off corse kuna baadhi watasurvive kutoka awamu moja kwenda nyingine. Ila causalities wanakuwepo kila awamu. Na awamu hii ni wengi sana ila watu wanaogopa mkono wa chuma!! Kuna wengi tu mwisho wao wa kuwa wana CCM ni 2020 ..............!!

Huo Mswada usingekuja kama asingekuwa Magufuli ............!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…