Umenichanganya mkuu! Unazitaja Greek na Roman empire kama mifano ya demokrasia na kuiweka pia uchina. Je, kwa vigezo vya leo unaweza ukasema China ina demokrasia? Ni yale yale ya akina Zitto wanayokataa kwamba TZ hakuna Demokrasia. Demokrasia ya Greek na roman haikumaanisha vyama vingi. Hii ya akina Zitto inamaanisha vyama vingi, na kama hakuna basi demokrasia hakuna. Wakigomewa mambo yao huo ni udikteta.
Back to democracy, je, unafahamu kuanguka kwa Greek na Roman empire haikutokana na u-dikteta? Ilitokana na ustaraabu (Wa wakati huo). The recent long Ottoman empire nayo hivyo hivyo. UHuru wa kiuchumi wa China siyo ingredient ya demokrasia.
btw. Ulimuelewaje Zitto bungeni kuamini kwamba umaskini TZ ulipungua wakati wa utawala wa kikwete? Indicator yake ni idadi ya watu walioingia ktk kipato kikubwa, lakini hataji walioingia ktk umaskini. He is just another stupid pretender.
Mosi, nimeiweka Uchina hapo kuaonesha kwamba hata wao wanakubali kwamba uhuru wa kiuchumi ni msingi wa maendeleo ya taifa lolote lile. Uchina ya leo ya Xi Jinping ni ya kidikteta lakini sehemu bora zaidi kuishi kuliko ile Uchina ya Mao Zedong ambayo kuwa tajiri ilikuwa ni dhambi. Kadiri siku zinavyoenda Uchina itabadilika na kuwa ni nchi inayokubaliana na mifumo ya kidemokrasia kutokana na nafasi yake kimataifa.
Pili, kwenye tafsiri ya neno demokrasia hakuna kitu kinachoitwa chama cha siasa. Kama nilivyosema kwa mdau moja hapa, Democracy is Janus Faced: It's not only a political system but also a value. Vyama vya kisiasa ni mifumo tuliyojiwekea ili kuweza kuishi kidemokrasia. Na tulifanya hivi baada ya kuona Direct Democracy haiwezekani kwa nchi kubwa za dunia ya leo, hivyo vyama vikawa kama njia mbadala wa Representative Democracy. Hivyo tusipoheshimu vyama tutakuwa hatuwapi watu sehemu ya kusemea mawazo yao.
Tatu, demokrasia ya Ugiriki na Roma hazikuwa na vyama vya siasa kutokana na mifumo yao ya uzalishaji waliyokuwa nayo kipindi hicho. Ambapo Roma walikuwa na mfumo wa Utumwa au Slavery Mode of Production na Ugiriki nao walikuwa na Slavery Mode of Production. Demokrasia ilikuwa ni kwa ajili ya watwana na siyo watumwa. Watumwa hawakuhesabiwa ka watu. Lakini katika dunia yetu ya leo ya utandawazi na ubepari ambapo suati ya kila mtu ina umuhimu, unadhani tukitoa vyama vya siasa na kukataza watu wasiseme tutaweza kweli kufika ? (Nakuanchia hili ulifikirie)
Upande mwingine nakubaliana na wewe kabisa kwamba vyama vingi haviashiriii uwepo wa demokrasia kama hivyo vyama haviwasaidii watu. Nchini Congo DRC kuna vyama vya siasa zaidi ya 20 lakini kuna vurugu kila siku. Marekani vyama vyenye nguvu ni viwili kama ilivyo nchini Uingereza lakini bado kuna demokrasia. Hivyo vyama visitupumbaze sana.
Kinadharia na tukichukua mfano wa Uchina chama kimoja ndicho mfumo bora kabisa wakuwasaidia wananchi kupata maendeleo kwasababu kwa nchi yenye chama kimoja ni rahisi sana kufanya mabadiliko ya sera na sheria kuliko nchi zenye vyama vingi. Mijadala inakuwepo mingi isiyo na maana: Angalia leo Marekani hadi wamefunga serikali yao kisa tu ugomvi wa Trump na Democrats. Kitu kama hichi uchina hakipo kabisa.
Nchini Tanzania, vyama vya siasa vimeonyesha umuhimu wake mkubwa sana. Hivi unadhani bila CHADEMA kuwepo Raisi Jakaya na genge lake la wakina Lowassa si wangekuwa washauza nchi yote hii kwa wazungu, wachina na waarabu! Leo tumejua ufisadi uliokuwepo serikalini kwasababu ya vyama vya upinzani. Nakubaliana na wewe kwamba kuna wakati hivi vyama vinavuka mipaka lakini ndiyo tutake visiwepo kabisa ?? Raisi Magufuli anataka kufanya maovu gani avichukie hivi vyama ??
Mwisho, Mimi siyo msemaji wa Zitto wala ACT wala mwanasiasa yoyote yule lakini jana bungeni nilimwelewa sana kwasababu hata Plato aliwahi kusema hivi "Human Rights are inherent entitlements which enable the development of human faculties" kwamba bila haki ya kusoma (Right to education) huwezi kufanya uvumbuzi (Innovation). Mimi narudia tena kwamba haki za binadami ni zinaendana sambamba na haki za binadamu na uhuru wa kiuchumi ni sehemu ya haki ya binadamu. Huwezi kuvitenga hivi vitu hata siku moja. Tunatafuta demokrasia ili tuweze kulinda haki zetu za kisiasa na kiuchumi. Nifahamuvyo mimi, Uhuru wa kiuchumi ni sehemu ya demokrasia.
Hayo mengine ya Zitto kuwa pretender mimi hayanihusu kabisa. I just discuss facts on the table hata kama zimetoka kwa kunguru, mwewe au nguruwe.