Tanzania imewahi kupigana vita ya kiuchumi? Inahitaji kufanya hivyo?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Mfano. Kuna kitu kinaitwa Chicken War. Miaka hiyo ya nyuma USA walikuwa wanauza sasa kuku Ulaya na hasa Ujerumani. Kuku kutoka USA walikuwa bei rahisi kuliko wale wanaozalishwa Ujerumani. Wafuga kuku wa Ujerumani wakaanza kulia kuwa kuku wa US wanawafanya washindwe kuuza. Serikali yao ikawasikiliza. Ikaongeza ushuru kwa kuku kutoka US kiasi kwamba wakawa siyo cheap tena. US kuona hivyo akarudishia kwa kuweka Tariff kwa gari Trucks zote kutoka Ujerumani.

Miaka mingi imepita na ushuru huo waliwekeana bado upo. Matokeo yake soko la Trucks za Ujerumani US likafa, na soko la kuku wa US Ujerumani likafa. Labda wazalisha kuku wa Ujerumani walipata soko na watengeneza Trucks wa US walipata soko.
Leo hii Trump ni kama anataka kuanzisha vita ya kiuchumi na kila nchi. Nchi yetu imewahipigana vita ya kiuchumi? Kuna umuhimu wa nchi kupigana vita hizi?
 
Kwani majasusi wetu wa kiuchumi wanasemaje?
 
Yani upigane vita ya kiuchumi wakati matatizo uliyonayo ni vita kabisa?

Huna maji safi kwa kila mtu, huna elimu bora, huna huduma zenye kiwango za afya, huna umeme wa uhakika, huna internet ya uhakika mambo mengi tu unayaendesha kizamani.
IMG_20250203_153212.jpg
 
Kipindi cha Magufuli vifaranga vilidhibitiwa kutoka nje.
Maziwa ya Kenya yalipitia msukosuko kuingia nchini, magari ya mizigo yakakwama mipakani na Kenya na mahindi ya Tanzania yakadaiwa yana sumu kuvu. Kisha Kenya ikadai itatafuta mahindi kutoka soko la nje kama Mexico kukidhi mahitaji yetu kipindi ambacho tutakuwa na price control ya mazao ya chakula.

Ni majaribio ya vita ya kiuchumi.
 
Yani upigane vita ya kiuchumi wakati matatizo uliyonayo ni vita kabisa?

Huna maji safi kwa kila mtu, huna elimu bora, huna huduma zenye kiwango za afya, huna umeme wa uhakika, huna internet ya uhakika mambo mengi tu unayaendesha kizamani.View attachment 3223940
Pengine tupo hivyo sababu hatupigani "Vita za kiuchumi."
 
Back
Top Bottom