Kuna vijana Libya walikuwa front line kuhakikisha Gaddafi anaondolewa Libya bila ya kujua kuwa nyuma yao kuna nguvu ovu inawasukuma. Vijana wengi wa Libya walipambana na serikali yao wakijidhani wamevaa vazi la uzalendo kumbe ni mipango iliyosukwa kwa ustadi na waroho wa rasilimali za Libya.
The same Tanzania, vijana wengi waliingia barabarani tarehe 29 September kwa mwavuli wa Uzalendo kumbe wenzao wachache wanaishi ughaibuni kwa kutegemea hizo vurugu. Rais Samia juzi kasema sasa kinachofuata ni maridhiano then kwa haraka katiba mpya itakuja.
Katiba mpya ni kilio cha upinzani kwa miaka mingi lakini pamoja na kuambiwa katiba mpya inakuja muda si mwingi lakini hakuna mchochezi hata mmoja aliyeunga mkono hiyo issue ya katiba mpya, so far hata wapinzani wenyewe hawajatoa kauli ya kuwaambia vijana wavumilie maana katiba mpya ambayo ndani yake ina mabando ya majibu yote.
Hii maana yake nini?
Hii maana yake ni kwamba shari na vurugu kwa baadhhi ya watu ni muhimu kuliko katiba mpya waliyokuwa wakiidai. Nawaambia kuwa hakuna kijana mchochezi au atahusika kupanga vurugu asifikiwe. Kila mtu atafikiwa tu. Polisi kila siku itaendelea kuwadaka na kuwaweka ndani wote wanaopanga uovu.
Hii ni Tanzania sio Kongo. Kama umekubali kuwa dekio la Wazungu ni vyema harakati zako kafanyie ukiwa nje huko. Tarehe 9 ukitoka tu kushindana na serikali wazazi wako watalia sana. Kuna mashine mpya za kisasa zimeingia kwa wingi sana.
Nchi itakuwa ya amani.
Hutaki hama nchi