Tanzania ina Serikali Korofi, Onevu kwa wananchi wake. Wanaaongea wao tu

Tanzania ina Serikali Korofi, Onevu kwa wananchi wake. Wanaaongea wao tu

Mhaini

Member
Joined
Apr 8, 2024
Posts
70
Reaction score
101
Tanzania ina Serikali Korofi, Onevu kwa wananchi wake. Wanaaongea wao tu. Sisi tukiongea hatua kali zinachukuliwa. Mtaua wangapi?

Watawala wanataka waongee wao tu. Mwanchi akiongea anatafutwa alipo ili wamuue.

Msikilize huyu bibi hapa kwenye Video

Wananchi wote wale watapewa hela walete vurugu? Halafu mnakuta mnazungumza Jabadi za vurugu tu jinsi walivyo uaawa hamtaki kuzungumzia.

Yakija mashirika mengine yakitoa ukweli kwamba mliua wananchi wenu mnasema ni waongo na hamtaki kuwaona kwenye nchi.

Sasa mnataka nini? Mnatuzuia kuongea kwamba ukionekana umeongea basi hatuwa kali zitachukuliwa. Sisi tutakaa kwenye kibano mpaka lini?Mtaua wangapi?

Nini wenye mnaongea, Hakuna anaewazuia. Lakini wengine wakiongea, sheria kali zitachukuliwa.

Niliona baba moja wa kisilamu hapa wakizungumza kwamba siku ya maandamano wataingia, mtaani watakatana vichwa. Watakatana vichwa. Kwani hayo maandamano yalikuwa ya kikristo? Yalikuwa ya kikristo hayo maandamano au ni ya wananchi kudai haki zao?

Lakini angekwa ni Mkristo amesema kile kitu,hatua zingechukuliwa kwa mara moja. Lakini kwa sababu ni muisilamu na Mnawagopa waislam kwa sababu mnajua walivyyo. Na ndio mana hamtaki kusema chochote.

Kwa hiyo, tumechoka, tumechoka, tumechoka, na hatutaki kufumbwa vinywa. Tuacheni tuseme. Kwa sababu, tunapokaa na maneno mioyoni ni kama mnatuumiza tu.

Mnaishia kutuumiza. Na sisi tulishaumia mpaka tumechoka. Kwasababu Haki ya maandamano ipo. Kila wakipeleka polisi kwamba tunataka kufanya maandamano siku flani polisi wanasemsla hakuna kibali. Sasa mnataka wafanya nini wananchi?

Mnataka wananchi wafanya nini? Ninyi ndo mnao wanyima kibali na ndo mnaoleta vurugu. Wakitoka kwa nguvu mnasema kwamba wamevunja sheria. Wana leta vurugu. Hapana waleta vurugu ni ninyi na si wananchi.

Mkiambiwa ukweli, mnatafuta kwamba waliongelea wapi, mtakamata wangapi? mtatuua bure mtatumaliza. Wengine damu zetu mkituua, yani ndio hivyo.

nyee mtuue tu kisa tumesema.

Masheria chungu nzima, mara ooh sheria za mawasiriano, ukiongea chochote kile, hatua kali zinachukuliwa. Sasa hatua kali mnataka mtufumbe vinywa sisi, tusisemi.hapana.

Huo sio utawala, huo ni uonevu wa hali ya juu, ni uonevu, Serikali korofi uonevu kwa wananchi wake.

Au mnaona nyie mna silaha, sisi hatuna silaha. Lakini unakuta tukisema, tayari, tumeshadakwa. Manake nini sasa?

Msitufumbe vinywa na kuhusu kuzungumza, tutaongea.
 
Back
Top Bottom