Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,770
- 5,423
Watumishi wengi ni watu wenye maarifa na upeo mdogo sana!
Wakati tangazo la nyongeza ya mishahara linatoka mimi Fumadilu Kalimanzila niliandika humu JF nikawaeleza kuwa Tanzania haina uwezo wa kuhimili nyongeza ya mishahara ya 23.3%! Nilishambuliwa sana humu.
Leo mtu amekuta ameongezewa Tshs.8,000/= anabwatuka kama chizi na kusahau kuwa watu wenye maarifa walifanya analysis na kuwaeleza kuwa huo uwezo Tanzania hatuna!
Sababu za umasikini wa Nchi hii ni nyingi ikiwa ni pamoja na vilaza wengi walioajiriwa Serikalini kwa " connections", kufoji vyeti na wengi waliofanya vibaya darasani (fail) na watumishi wasiopenda kujiendeleza (personal development) n.k.
Watumishi wengi wa Serikali ni watu wa majungu, washirikina, wasaka posho ,wavivu na watu wasiotoa huduma bora kwa Wananchi.
Wengine ni watu waliojengeka vichwani mwao kuumiza Wananchi, vichwa vyao vimejaa mawazo ya rushwa ,kufunga biashara za watu, kufilisi watu ama kutia watu hasara za kijinga,kufuta biashara na kupiga watu fine basi.
Wengi ni watu wenye maarifa na ubunifu duni ambao hata genge la kuuza nyanya hawawezi kuendesha.
Wengi hawana tija kabisa na wanalipwa mishahara kutokana na Kodi za Wananchi kwa kukaa maeneo ya kazi na si kwa tija ya ufanisi wa kazi zao!