Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upuuzi mtupu.Mapungufu madogo madogo na kasoro chache zilizopo, vipo pia kila mahali inapotekelezwa demokrasia ya aina ya Tanzania, mathalani Marekani na kwingineko.
Na kwasababu hiyo uchaguzi huru na wa haki Tz upo, Tume huru ya uchaguzi Tz ipo, Utawala wa Sheria na utawala bora Tz upo, heshima kwa haki za binadamu na makundi maalumu Tz vipo, uhuru wa maoni, habari, vyombo vya habari na mawasilino Tz vipo, uwazi na uwajibikaji Tz upo, bunge na mahakama huru Tz vipo, usawa na haki ya kupata huduma za msingi Tz vipo, ulinzi na usalama wa watu, mali na makazi yao Tz vipo, uhuru wa kuabudu na kuabudiwa Tz upo, uhuru wa kutoa na kupokea sadaka na misaada Tz upo, nakadhalika nakadhali, nakadhalika, nakadhalika.....
Tunaweza kutofautiana kwa kiwango cha kuridhika cha utekelezaji wa Demokrasia hii ya vyama vingi Tanzania na ufanisi wake. Na hiyo ni haki na ni Demokrasia ya maoni, kutofautiana na kukubaliana kutofautiana.
Mathalani, wingine anaweza kusema hakuna kabisa demokrasia, mwingine akasepa ipo kidogo, mwingine akasema ipo sana, na mwingine akasema hana maoni kabisa juu ya Demokrasia Tanzania, nakadhalika, nakadhalika, nakadhalika...
Lakini, ukweli usemwe,
Amani, Utulivu na utangamano miongoni mwa waTanzania ni matokeo na matunda matamu ya utekelezaji wa Demokrasia nchini. Ni muhimu sana hali hii ya ustahimilivu na kuvumiliana kuimarishwa zaidi ndani ya mioyo ya wanasiasa na watanzani wote ile umaja wetu usitetereke.
Maendeleo ya watu na makazi yao, maendeleo ya biashara, utalii, miundombinu ya barabara, anga, maji, reli, afya elimu, michezo na vyote vinavyoonekana na visivyo onekana kisiasa, kiuchumi na kijamii ni zao la Demokrasia ya vyama vingi nchini.
Kwa kiwango kikubwa sana maendeleo yanayonekana hivi sasa yamechochewa pakubwa sana na utekelezaji wa demokrasia ya vyama vingi. Mathalani uwazi, uwajibikaji, ulinzi na usalama serikalini.
Changamoto ndogo ndogo na kasoro chache zilizopo na mara nyingi huonekana nyakati za uchaguzi, zinarekebishika na kutatulika ikiwa tu utashi wa kisiasa na dhamira ya kweli miongoni mwa wanasiasa utawekwa kwenye mizania sawa kwa maneno na matendo, kwa maslahi mapana ya umoja na mshikamano wa Tanzania.
Njia zinazotumiwa na wanasiasa kujaribu kushinikiza marekebisho ya mapungufu na kasoro za kidemokrasia nchini, zinarefusha zaidi kupata majawabu. Ushari wa maneno ya wanasiasa dhidi ya serikali, amri na matakwa ya lazima ya wanasiasa dhidi ya serikali, ubabe na utoto wa wanasiasa dhidi ya serikali, nakadhalika nakadhalika nakadhalika.....
Hakuna ungwana, ustaarbu wala utashi katika kauli na matendo miongoni mwa wanasiasa dhidi ya serikali. Ni kutunishiana misiuli kusiko koma, kutwa kucha ni kiburi na majivuno cha eti chama hiki au kile kina wafuasi wengi kuliko kingine na kwahivyo kina haki zaidi na kinaweza kufanya chochote itakacho.
Hii si sawa.
Huu ni mwanzo wa kuharibu na kumomonyoa demokrasia ambayo tayari imekomaa, imeimarika, inashamiri na kunawiri vizuri sana nchini.
Kama raia wa Tanzania navisihi vyama vya siasa na wanasiasa, vyama vya kiraia, taasisi za dini na makundi mbalimbali ya kutetea haki nchini,
fanyieni vyovyote mfanyavyo kwa mujibu wa sheria.
Lakini chondechonde, matokeo ya hayo yote muyafanyayo iwe ni Amani, Amani, Amani, ya huyu Mama Yetu Tanzania.
wasaalam.....
shukrani sana kiongozi.Kwa mujibu wa tafiti za wataalamu wa mambo ya siasa Tanzania ni nchi ya tano duniani kwa utawala bora unaozingatia haki na misingi ya kidemokrasia , utafiti huo umeonyesha nchi ya Guatemala, Honduri na Malta kushika nafasi tatu boraš
mgombe mwenza nae anapeleka wawakilishi/mawakala tatzo lipo wap?Ha
Hakuna usawa hapo.
Mtu wa chama fulani anateua msimamizi wa uchaguzi ambao anashiriki..š¤£š¤£
ndio ule ushari unaochelewesha na kurefusha muda wa kupatikana majawabau ya dosari na kasoro chache zilizopo kwenye demokrasia.Matatizo ya kukulia husweken huko ndaani ndani maporini ndio haya. Siku MTU akija Dar anaona CCM. Imefanya makubwa. Hivi nimuulize, wakati wa chaguzi za 2019/2020 ulikua bado uko porini unakula mizizi na asali au ulishatokeza kwenye mwanga?
una hoja muhimu sana ndugu. na ni kweli kabisa hamna haya ya kuvuruga amani. Ni ungwana tu.HAMNA HAJA YA HAYO. NCHI INATAKIWE IWE NA AMANI.
TATIZO NI KATIBA::
MMOJA ANAMTEUA MSIMAMIZI KUAMUA JAMBO AMBALO NAE ANALITAKA
Kwamba huwa hatuoni hujuma na upuuzi unaofanywa kwa mawakala wa upinzani ama?mgombe mwenza nae anapeleka wawakilishi/mawakala tatzo lipo wap?
Kawaida yako , au ni ID yako nyingine maana ni akili kama zako tuNaunga mkono andiko lako na sina nyongeza.
ukiona hvyo ndyo culture ya muafrika,sisi bado hatujafka kutaka pure democracy na ikifika tutaipata,kwa sasa msilete fujoKwamba huwa hatuoni hujuma na upuuzi unaofanywa kwa mawakala wa upinzani ama?
Mapungufu madogo madogo na kasoro chache zilizopo, vipo pia kila mahali inapotekelezwa demokrasia ya aina ya Tanzania, mathalani Marekani na kwingineko.
Na kwasababu hiyo uchaguzi huru na wa haki Tz upo, Tume huru ya uchaguzi Tz ipo, Utawala wa Sheria na utawala bora Tz upo, heshima kwa haki za binadamu na makundi maalumu Tz vipo, uhuru wa maoni, habari, vyombo vya habari na mawasilino Tz vipo, uwazi na uwajibikaji Tz upo, bunge na mahakama huru Tz vipo, usawa na haki ya kupata huduma za msingi Tz vipo, ulinzi na usalama wa watu, mali na makazi yao Tz vipo, uhuru wa kuabudu na kuabudiwa Tz upo, uhuru wa kutoa na kupokea sadaka na misaada Tz upo, nakadhalika nakadhali, nakadhalika, nakadhalika.....
Tunaweza kutofautiana kwa kiwango cha kuridhika cha utekelezaji wa Demokrasia hii ya vyama vingi Tanzania na ufanisi wake. Na hiyo ni haki na ni Demokrasia ya maoni, kutofautiana na kukubaliana kutofautiana.
Mathalani, wingine anaweza kusema hakuna kabisa demokrasia, mwingine akasepa ipo kidogo, mwingine akasema ipo sana, na mwingine akasema hana maoni kabisa juu ya Demokrasia Tanzania, nakadhalika, nakadhalika, nakadhalika...
Lakini, ukweli usemwe,
Amani, Utulivu na utangamano miongoni mwa waTanzania ni matokeo na matunda matamu ya utekelezaji wa Demokrasia nchini. Ni muhimu sana hali hii ya ustahimilivu na kuvumiliana kuimarishwa zaidi ndani ya mioyo ya wanasiasa na watanzani wote ile umaja wetu usitetereke.
Maendeleo ya watu na makazi yao, maendeleo ya biashara, utalii, miundombinu ya barabara, anga, maji, reli, afya elimu, michezo na vyote vinavyoonekana na visivyo onekana kisiasa, kiuchumi na kijamii ni zao la Demokrasia ya vyama vingi nchini.
Kwa kiwango kikubwa sana maendeleo yanayonekana hivi sasa yamechochewa pakubwa sana na utekelezaji wa demokrasia ya vyama vingi. Mathalani uwazi, uwajibikaji, ulinzi na usalama serikalini.
Changamoto ndogo ndogo na kasoro chache zilizopo na mara nyingi huonekana nyakati za uchaguzi, zinarekebishika na kutatulika ikiwa tu utashi wa kisiasa na dhamira ya kweli miongoni mwa wanasiasa utawekwa kwenye mizania sawa kwa maneno na matendo, kwa maslahi mapana ya umoja na mshikamano wa Tanzania.
Njia zinazotumiwa na wanasiasa kujaribu kushinikiza marekebisho ya mapungufu na kasoro za kidemokrasia nchini, zinarefusha zaidi kupata majawabu. Ushari wa maneno ya wanasiasa dhidi ya serikali, amri na matakwa ya lazima ya wanasiasa dhidi ya serikali, ubabe na utoto wa wanasiasa dhidi ya serikali, nakadhalika nakadhalika nakadhalika.....
Hakuna ungwana, ustaarbu wala utashi katika kauli na matendo miongoni mwa wanasiasa dhidi ya serikali. Ni kutunishiana misiuli kusiko koma, kutwa kucha ni kiburi na majivuno cha eti chama hiki au kile kina wafuasi wengi kuliko kingine na kwahivyo kina haki zaidi na kinaweza kufanya chochote itakacho.
Hii si sawa.
Huu ni mwanzo wa kuharibu na kumomonyoa demokrasia ambayo tayari imekomaa, imeimarika, inashamiri na kunawiri vizuri sana nchini.
Kama raia wa Tanzania navisihi vyama vya siasa na wanasiasa, vyama vya kiraia, taasisi za dini na makundi mbalimbali ya kutetea haki nchini,
fanyieni vyovyote mfanyavyo kwa mujibu wa sheria.
Lakini chondechonde, matokeo ya hayo yote muyafanyayo iwe
Sio kweli, kubalini tu kuwa mmefikia mwisho wa ushawishi wenu kwa umma. Sio kutaka kucheza na maneno.ukiona hvyo ndyo culture ya muafrika,sisi bado hatujafka kutaka pure democracy na ikifika tutaipata,kwa sasa msilete fujo
ni vizuri kubainisha dosari na kasoro zote kwa makini, kisha kwa ungwana wa kiwango wasilisha mapendekezo mujarabu kiungwana pia panapohusika.Demokrasia ya kupitishana bila kupingwa inapatikana Tanzania tu tume huru ya kuengua wapinzani peke yake ipo Tanzania tu,tume huru ya kujaza kura fake kuibeba CCM ipo Tanzania tu,tume huru inayofanyia kazi maelekezo ya kuibeba CCM ipo Tanzania tu,tume huru ambayo wapinzani pekee ndio hawajui kujaza form za uchaguzi inapatikana Tanzania tu,demokrasia ambayo intelejensia yao inaonyesha uvunjifu wa amani ya nchi ni kwa wapinzani peke yao inapatikana Tanzania tu,tume huru ambayo wapinzani ndio wanaotekwa na kuporwa form za uchaguzi na haikemei matukio hayo inapatikana Tanzania tu.