Tanzania inafuata misingi yote ya Demokrasia ya vyama vingi

Kwa mujibu wa tafiti za wataalamu wa mambo ya siasa Tanzania ni nchi ya tano duniani kwa utawala bora unaozingatia haki na misingi ya kidemokrasia , utafiti huo umeonyesha nchi ya Guatemala, Honduri na Malta kushika nafasi tatu bora🐒
 
Upuuzi mtupu.
 
Kwa mujibu wa tafiti za wataalamu wa mambo ya siasa Tanzania ni nchi ya tano duniani kwa utawala bora unaozingatia haki na misingi ya kidemokrasia , utafiti huo umeonyesha nchi ya Guatemala, Honduri na Malta kushika nafasi tatu bora🐒
shukrani sana kiongozi.
 
Matatizo ya kukulia husweken huko ndaani ndani maporini ndio haya. Siku MTU akija Dar anaona CCM. Imefanya makubwa. Hivi nimuulize, wakati wa chaguzi za 2019/2020 ulikua bado uko porini unakula mizizi na asali au ulishatokeza kwenye mwanga?
 
Matatizo ya kukulia husweken huko ndaani ndani maporini ndio haya. Siku MTU akija Dar anaona CCM. Imefanya makubwa. Hivi nimuulize, wakati wa chaguzi za 2019/2020 ulikua bado uko porini unakula mizizi na asali au ulishatokeza kwenye mwanga?
ndio ule ushari unaochelewesha na kurefusha muda wa kupatikana majawabau ya dosari na kasoro chache zilizopo kwenye demokrasia.
ungwana umekua shari.
 
HAMNA HAJA YA HAYO. NCHI INATAKIWE IWE NA AMANI.
TATIZO NI KATIBA::
MMOJA ANAMTEUA MSIMAMIZI KUAMUA JAMBO AMBALO NAE ANALITAKA
una hoja muhimu sana ndugu. na ni kweli kabisa hamna haya ya kuvuruga amani. Ni ungwana tu.

kinachotokea na kuonekana kinasikitisha sana, yaani uwasilishwaji wa hoja na malalamiko panapo husika unafanywa na mwanadamu na unakua katika hali ya ushari mno na wa kulazimisha.
sasa na mpokea hoja na malalamiko pia ni mwanadamu, Sasa wanadamu tulivyo nae anavimba. Hakubali kulazimishwa.

kinachotokea ni kuvimbiana na mambo yanagoma kwenda kabsaa. inakua ni kulalama kutwa kucha
 
Kwamba huwa hatuoni hujuma na upuuzi unaofanywa kwa mawakala wa upinzani ama?
ukiona hvyo ndyo culture ya muafrika,sisi bado hatujafka kutaka pure democracy na ikifika tutaipata,kwa sasa msilete fujo
 
Tanzania imekubali kuwa na mfumo wa vyama vingi,imekataa demokrasia.
 
Demokrasia gani katika Uchaguzi Mkuu 2020 Mkuu wa Polisi alitumia muda mwingi kumfuatilia mgombea mmoja wa upinzani. Huyo Mkuu hata akajisahau akaelekeza mgombea huyo popote alipo ajisalimishe Polisi. Tume ya Uchaguzi ikaagiza tuhuma husika ni wajibu wa Tume sio Polisi.
Mahakama Kuu ilitoa uamuzi katika kesi ya wanaharakati kuwa si sahihi Wakurugenzi wa Wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi. Uamuzi huo ulitupiliwa mbali, Wakurugenzi wakahakikisha wagombea Uchaguzi Mkuu wa 2020 toka vyama vya upinzani wanawekewa vikwazo kila hatua ya mchakato wa kujisajili hadi kutangaza matokeo. Kilichotokea ni BUNGE la chama kimoja lililokorogewa Covid 19. Katika mfumo huo maendeleo kwa uma wa Watanzania itabaki kuwa sarabi ("mirage").
 
ukiona hvyo ndyo culture ya muafrika,sisi bado hatujafka kutaka pure democracy na ikifika tutaipata,kwa sasa msilete fujo
Sio kweli, kubalini tu kuwa mmefikia mwisho wa ushawishi wenu kwa umma. Sio kutaka kucheza na maneno.
 
Kwenye demokrasia halisi hakuna mgombea anayeenguliwa bila amri ya mahakama.
 
Tanzania ina mengi mazuri kwa upande wa utawala wa kidemocrasia ila yafuatayo bado yanahitaji kuboreshwa:
1. Tume ya Uchaguzi - iwe huru kweli
2. Mahakama - ziwe mbali na siasa na rushwa
3. Polisi wawe mbali na siasa lakini watekeleze kazi yao ya kuhakikisha nchi ni salama na tulivu
4. CCM wakubali kua kuna siku inabidi ipishe wengine.
5. Mali za CCM walizovuna kabla ya mfumo wa vyama vingi irudishwe serikakini sababu wananchi wote walichangia na zinawapa CCM uwezo kandamizi kwa wapinzani.
6. Wapinzani wajiimarishe na kubainisha kua wanaweza kuaminiwa na watanzania kuunda serikali. Mpaka sasa haioneshi wana huo uwezo.
7. Siasa za visasi ziepukike kabisa. Atakea chukua utawala ajikite kwenye maendeleo na umoja wa taifa.

Mimi naona bora kwa miaka kama 20 ijayo kuchukua mfumo wa serikali ya mseto au maridhiano kufuatana na idadi ya kura vyama vilivopata. Hii itawezeshe kujenga imani na na utamaduni wa kufanya kazi kwa umoja hata baadae tukirudia mfumo wa chama kimoja kilicho shinda uchaguzi kutawala pekee.
 
ni vizuri kubainisha dosari na kasoro zote kwa makini, kisha kwa ungwana wa kiwango wasilisha mapendekezo mujarabu kiungwana pia panapohusika.

lawama na ghadhabu dhidi ya udhaifu wa demokrasia nchini, si suluhu hata kidogo.
Malalamiko yatakuepo tu, miaka nenda miaka rudi ,
walalamikaji nnje, walalamikiwa ndani na hakuna kitakachofanyika na mambo yateendelea kama yalivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…