Tanzania inahitaji Rais anayejiamini na mwenye uhakika wa Jambo lake na Maamuzi yake

Tanzania inahitaji Rais anayejiamini na mwenye uhakika wa Jambo lake na Maamuzi yake

hata mm naumia kisawa sawa, siamini yatokeayo kweli tumefiwa na baba jembe. Swala la tutaleta majibu hapo baadae ni hatari...angeshauriana na wasaidizi angekuwa anamaliza mchezo palepale kama baba alivyokuwa anafanya. Pia hii ya kutengua wala sioni umuhimu..maana baba akimtengua mtu anamwambia kabisa nimekutengua sababu yake ni hii na ile, hata sisi wananchi tunapata mwanga na kuridhika na uteuzi mpya. kwasasa hata hatujui wanatenguliwa kwasababu ipi?..au ndio yale yale ya ccm ya kale ya kufichiana uozo imerudi kwa kasi. Watakaokuja kuja kugombea nafasi hii ya juu nami naunga mkono hoja wawe ni WANAUME JASIRI, WAWAZI, WAKWELI, WACHAPA KAZI, WASIOOGOPA, WENYE KUFANYA MAAMUZI YA KISHUJAA ili kulikomboa taifa letu zuri
 
Kama mwendazake ndiye alikuwa na sifa ambazo mama hana. Ni kheri mno mama azikose kabisa.

Mama akaze uzi hapo hapo tayari dawa inapenya.
Akaze uzi gani, wa kutokuwa makini kupitia sifa za viongozi kabla ya kuwateua?
 
Kuna boss wangu mmoja aliwahi kuniambia - 'Theodora you can make as many mistakes as you want BUT never repeat the same mistake twice'. Inamaana ukirudia kosa lile lile ni kwamba hujajifunza. Na katika career, politics na hata maisha ya kawaida kwenye familia its unacceptable.

Labda ushauri kwa Madame President SSH - she has to take her time. Maana uteuzi siyo riadha na yeye ana mamlaka ya kuteua basi asiharakishwe. Bado naamini there are great women who can be great leaders....
Unaweza tokea msituni ukawa Rais bora, lakini unaweza utoke darasani ukawa Rais wa ajabu. Urais Ni Taasisi imara Basi!
 
Umeongea point kabisa kiukweli hata mm binafsi ningependa kumuona Rais Samia akifanikiwa na mafanikio yake ndiyo mafanikio ya Tanzania tatizo linakuja anapokubali kushikiwa kalamu kwenye kuandika anatakiwa asiendekeze urafiki kwenye mamlaka aliyonayo ni makubwa mnoo inabidi awe na utulivu wa hali ya juu sana katika kufanya maamuzi akiendekeza undugu na urafiki safari kwake itakuwa ngumu ayavae mamlaka ya Urais awe na mipaka atengeneze mazingira ya kutozoeleka zoeleka
Ukizoea maisha ya kiswahili huwezi kuwa na utulivu...asilani
Ukiruhusu hisia kutawala akili kwa kuwa tu anaekupa muongozo ndio alikutoa kisiasa umeotea ...JPM kuna wakati aliwaambia wazee watulie wanawashwa sana.
Ila mwanamke ambae ulimvu..pichu lazima afuate kilausemalo kwa kuzingatia anaamini we ndo umefikisha alipo.
Mama yetu hakuwahi jiandaa kuwa Presedaa kamwe ni zali tu.. aliridhika kutumwa kuelekezwa cha kufanya sio kutoa maamuzi ya mwisho.
Sasa msela wangu kwa vile bado anatamani sana kuongoza akiongozwa na wivu wakiswahili ...kwamba mshamba fulani alikuja kumfunika kimaamuzi na kuona matokeo basi moyo ulikuwa unamuuma mpaka kukonda ila kwa sasa anaraha balaa na shavu limerejea maana anaongoza kwa kivuli.
Kumtaka mama kukaa nae kando hilo sahau ..endelea kuumia taratibu mpaka kwenye sanduku la kura ndio utafuta machozi.

Kuna mengi sana kachemsha kisa ushikaji...Tume ya madini kamweka shoga yake wa kitambo ex Barrick employee kuongoza unatarajia nini hapo.
Sukuma gang, Mataga na wafuasi wajiwe ambao ki uhalisia ndio wenye uchungu na hii nchi ni kundi lililopozwa kwenye mitandao lakini mitaani wanapenda kuona mama anabaki nje ya awamu ya nne ili waende sawa.
 
Kwa maoni yangu nadhani ni kuwa rais ameanza kwa kupanga na kupangua kikosi kazi kwaajili ya kuendana na misimamo yake.

Yani ni kama kocha mpya akichukua team lazima kuna panga pangua huwa zinatokea kwenye kikosi ikiwamo na sajili mpya na kutemwa baadhi ya wachezaji ili kocha abaki na wale ambao wata fit kwenye mfumo wake.

Baada ya siku 100 madarakani kama hizi panga pangua hazijaisha basi nami nitakuunga mkono mleta mada.

Mada yako ina hoja nzito lakini.
Dah....panga pangua ya nini tena....Sera ni zilezile....tena alisema mwenyewe kuwa yeye na JPM ni kitu kimoja....anyway tuendelee kumpa Mama muda [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2960]
 
Tuna Rais ambae anasahau hata majina ya aliowateua na mikoa aliyowapa[emoji3][emoji3][emoji3]
Mungu tunusuru
 
Mtaanza sasa Kutulazimisha kuamini kuwa Watu wa Jinsia fulani si ' Competent ' kwa nafasi ya ' Head of State ' na akina GENTAMYCINE tukiamini hivyo msituchukie au msianze ' Kutubatiza ' Jina lenu la SUKUMA GANG mkimaanisha ni Wapinzani ' Tukuka ' wa Utawala huu wa Rais ( Mama ) Samia Suluhu Hassan.

Tanzania ya sasa inahitaji Rais ambaye haishii tu kuwa Mchapakazi bali pia mwenye uwezo wa Kufuatilia Jambo, Kusoma sana, Kujiridhisha na kuwa na Timu ya Wasaidizi ( Washauri ) wenye Akili hasa na siyo Wapumbavu wenye ' Uchawa ' mwingi.

Kibinadamu Tukio moja linasameheka kwani hata Mimi GENTAMYCINE na hata Wewe ' Member ' pia huwa tunakosea ila Mtu huyo huyo akilirudia tena Tukio ( Kosa ) hilo hilo anaanza kututia Mashaka na kuanza kutupa Mtihani mzito wa Kumjibia kutoka kwa wale wasiomkubali.

Nina mengi Moyoni na Rohoni ila kabla tu Hasira zangu hazijanipanda zaidi kwa Upuuzi unaoanza Kuzoeleka natoa Ushauri wa bure kwa wale Watanzania ambao watagombea Urais miaka ijayo GENTAMYCINE nawaombeni teueni Makamu wa Rais Vijana ( Damu Changa ) na pia wawe ' very intelligent ' ili hata ikitokea Mmekufa ( Mmefariki ) watakaotwaa Madaraka ' Kikatiba ' wawe ni Watu ambao hawatotupa Mashaka Mashaka katika Kuwaamini kama ninavyoanza kupata Mashaka hayo sasa.

Najua kwa Uzi huu leo nami nitabatizwa kuwa natokea SUKUMA GANG hivyo nikiitwa hivyo kwa kusema huu Ukweli wangu nitalipokea hilo Jina ila pamoja na kwamba Hayati Rais Dkt. Magufuli alikuwa na ' Mapungufu ' yake ila nilikuwa nikimpenda zaidi katika tabia yake ya kupenda Kujiridhisha, Kudadisi, Kufuatilia Jambo na kufanya Maamuzi ya uhakika ambayo huenda yakachelewa ila hayatotupa Mashaka na kuanza Kutusababishia tuwe na Maswali mengi.

Mlio karibu na Mheshimiwa Rais nanyi pia ni sehemu ya tatizo kwani hamumsaidii hadi Mama kila mara anatoa ' Maboko ' yake tu ya ' Kuteua Kutengua ' au yawezekana pia mkawa katika Mpango ' Maalum ' wa Kumpigisha Shoti ( Kumuhujumu Mama ) ili aharibikiwe na achekwe Yeye na tuchekwe pia Sisi wana CCM wote.

Mwisho namalizia kwa Mama ( Mheshimiwa Rais ) hebu punguza sana kuwa karibu kwa 99% na Rais Mstaafu Kikwete ( hasa Kiushauri ) kwani Kitendo hiki ' Kinawakera ' baadhi ya Watendaji wako ( tena Waandamizi kabisa ) na usipokuwa nacho makini kitakuja Kukugharimu na utakuja Kunikumbuka GENTAMYCINE niliyenyimwa Utajiri na Nguvu ila niliyepewa Fikra na Maono na Mwenyezi Mungu.

Sisemi usimsikilize Mzee Kikwete bali acha Kumfanya ndiyo kila Kitu Kwako Kiushauri bali Shirikisho pia na Watu ( Wastaafu ) wengine lakini pia Waamini na hao Watendaji wako ulionao sasa Serikalini kwani huenda na Wao wakawa na Mawazo Cbanya Kwako Kimaendeleo na Kiuongozi hata kuliko hayo unayoyapata kwa Mzee Kikwete.

Hii ' Teua Tengua ' iwe mwisho Mama!!!!
Well saidi; rais anayetegemea sana ushauri siyo competent. Anatakiwa aweze kutoa uamauzi hata bila kupata ushauri, na akipata ushauri anaupima kwanza kabla ya kutoa uamuzi, kwani siyo lazima akubaliane na kila ushauri. Watamwita kuwa hashauriki, lakini yeye asisyumbishwe na mano hayo.
 
Wabongo mna vipaji vya kulalamika , kulaum na unafiki.

Mama wewe chapa kazi ukiona Shida mahali itatue papo hapo.

Ulidhani mama anashindwa kuwaacha hao walioteuliwa bahati mbaya waendelee kuchapa kazi mpaka baadae kabisa Kama wakina Kitwangwa?

Anachokifanya Rai's anakifanya Kwa nia njema kabisa.
Hawa ndio wabongo. Uzuri wa Mama yetu kipenzi Samia Suluhu Hassan ni kwamba hasikilizi wasema ovyo.

Mama anajua jukumu lake ni kuwatumikia Watanzania, full stop!
 
Siku zote marais wastaafu wanakuwa ni sehemu ya washauri wa marais waliopo madarakani. Hii ipo dunia nzima. Mzee Biden pamoja na kuwa anamzidi Obama miaka 19 lakini kwa Obama kumtangulia kuwa rais tayari ni sehemu ya washauri wake muhimu na wa karibu.

Urais ni cheo kikubwa sana, na Mzee Kikwete ni mwanadiplomasia mzoefu, hivyo kwa Rais Samia kumkwepa ni suala lisilowezekana. Kikwete ni muhimu kwa Samia kwa sasa kuliko wakati wowote ule.

Rais wa sasa ni mwanamke wa kwanza kuongoza Tanzania, hawezi kufanya baadhi ya maamuzi kama ambayo yangefanywa na rais mwanaume. Ni kumvumilia na kumtia moyo.
Hizi chuki zao na husda zao kwa mzee wa Msoga hata sijui zimesababishwa na nini.

Eti mama asimsikilize Mzee kikwete mtu alielitumikia taifa hili katika nyadhifa mbali mbali nyeto kabisa ambazo asilimia 98 ya members wote humu mtaota tu kuzipata amsikilize eti gentamycine.

Hivi hawa watu wanakula MAVI??? Mbona akili zao mbovu hivi???
 
Tatizo liko wapi? si ametengua kabla hajaapa? Na inawezekana hata anaweza akawa badilisha hata kabla hawaja apishwa SHIDA IKO WAPI Mkuu.
Sifa ya Magufuli alikuwa anatengua na anatoa sababu za kutengua hata miezi minne hajaisha tayari waliokuwa wanafurahia kifo chake sasa wameanza kuomboleza kwa uchungu kuliko hata sisi tuliolia sikuza msiba.Tutaelewana tu kwamba hakunaga kama JPM
 
"Hayati Rais Dkt. Magufuli alikuwa na ' Mapungufu ' yake ila nilikuwa nikimpenda zaidi katika tabia yake ya kupenda Kujiridhisha, Kudadisi, Kufuatilia Jambo na kufanya Maamuzi ya uhakika ambayo huenda yakachelewa ila hayatotupa Mashaka na kuanza Kutusababishia tuwe na Maswali mengi."

Hayo maneno yako ndio Usukuma Gang wenyewe. JPM huyu huyu aliyemini Kabudi Nguli wa sheria anafaa Mambo ya nje na Mahiga Nguli wa diplomasia anafaa sheria?

Pia tambua kwamba hakuna haja ya kutoa mfananisho wa Samia mtoto Pwani , mtoto wa mjini na JPM aliyekulia porini akichunga ng'ombe akaishia kuwa mshamba wa madaraka.

Umakini wa Kiongozi ni kuchukua hatua papo hapo ili mradi anafanya hivyo Kwa nia njema.
Well said.

Yaani eti Leo Hayati Magufuli alikuwa bora. MAVI yao hawa Sukuma gang.

Na kwa taarifa tu, sisi Watanzania tumedhamiria kumuomba Mama agombee mwaka 2025 maana miaka 4 ni michache sana kuleta mabadiliko ya kweli na kuondoa majeraha na sononeko zilizosababishwa na hawa washamba
 
Rais ana majukumu mengi hivyo kutimiza yote bila kuwa na wasaidizi wenye weredi kutakuwa hakuna tija ndio maana teuzi zipo na zinazingatia sheria zote

Kitendo cha kumsema mzee JK kuwa ndo anashika kalamu bila ushaidi huu ni uzandiki mkuu mbona kipindi Mzee JPM alipokuwa karibu sana na hayati BWM hukuja na uzi wa kumshauri? Leo Mama pia kafanya lile lile kama la JPM kuwa karibu na BWM yeye kawa karibu na Jk sasa ndo imekuwa udwazi?
Tena alivyo mpuuzi eti mama asimsikilize JK, askilizwe nani sasa??
 
Back
Top Bottom