Huo ujinga atauondoa nani?.Bila kuondoa huo mfumo ulioweka nakulea huo ujinga kamwe usitegemee mfumo uliopo sasa utauondoa.
That is beside my point.
OP (TSC) - Naona mabadiliko makubwa Tanzania.
Kiranga - Mabadiliko makubwa hayawezekani bila kuondoa ujinga mkubwa wa watu wengi, hapo hakuna shortcut.
Gigabyte - Huo ujinga atauondoa nani? Bila kuondoa huo mfumo uliopo sasa...
That is beside my point, my point ni kwamba usitegemee mabadiliko makubwa bila kuondoa ujinga.
Hayo masuala la ujinga atauondoa nani, na tutauondoa vipi ni masuala tofauti na angalizo langu.
Yani kuna nyumba ina geti, halafu ina mlango wa mbele umefungwa.
OP (TSC) anakuja anasema naona tutapata ufunguo wa geti sasa hivi. Tutaingia ndani ya nyumba hii.
Mimi namkumbusha tu, asifikiri kwamba tukipata ufunguo wa geti ndiyo tumemaliza mchezo, bado kuna mlango wa mbele hatujaweza kuufungua.
Wewe unaniambia ni muhimu kufungua geti kwanza, bila kufungua geti hatutafika hata hapo kwenye huo mlango wa mbele.
Obviously you are right, lakini hilo haliondoi point yangu kwamba bado kuna mlango wa mbele, tusiusahau na kufikiri kwamba tukifungua geti ndiyo tumemaliza matatizo.