Tetesi: Tanzania inalipwa mabilioni ya fedha toka nje ambazo zimefanywa siri na serikali hazina rekodi, tumenunulia ndege, na kujenga SGR na Stiegler nk

Umeandika pumba tupu na katika hilo swala la helium hujui chochote
Kwa taarifa yako tu ipo kiasi cha futi cubic 54 billion ambazo kwenye soko la dunia huo mzigo ni kama trillion 10 hivi hapo hajaingia mkataba na wamiliki wa kitalu kutoa gharama za utafutaji na uchimbaji unakuja potosha umma hapo hizi akili za nyumbu wa DJ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara umeisha ukubali huo uzushi billa kufanya utafiti zaidi na kujiridhisha?
Je kama hela hiyo wange iweka kwenye account za nje bila kutengeneza hizo miundo mbinu!
Labda wanaozitoa wanazifuatilia zinafanya nini?
 
Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha...Hii mizee yote ife “jangwani”kama Musa ndio tutafikia nchi ya maziwa na asali
 
Hili ni swali zuri sana hata kama baadhi ya yaliyoandikwa kwenye mada yanakiasi fulani cha kutoaminika. Kwa mfano, hilo la 'compensation' kupisha viwanda, ni gumu sana, hata kama sio kwamba haliwezekani.

Lakini natamani ingekuwa hivyo, mradi tusidaiwe tu hapo tutakapokuwa tayari kuvuna gesi yetu na kutunufaisha ipasavyo.

Serikali inayopenda kufanya mambo yake gizani kama hii, kila lisemwalo ni vigumu kulipuuza.
 
Lakini kama inatumika kujenga miundo mbinu kwaajili ya taifa sioni Shida. Hapa nampongeza rais mzalendo Coz Ingekuwa enzi zile hii hata kuona tusingeona. Watu wangegawana tu na 10%zao na gesi ingechimbwa bila sisi kujua. Hongera mheshimiwa rais Dr John Pombe Joseph Magufuli mzalendo namba moja kwa kufikiria taifa kwanza wakati wote.

Kulingana na mtoa mada ni kuwa gesi haijaanza kuchimbwa basi ni jambo nzuri. Haichimbwi tunakula faida. Kongole serikali ya awamu ya tano business oriented.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye mishahara haitawezekana lakini kwenye ndege imewezekana?!!!
Haya endelea na kutujuza sie tunaomba na kashata tu tunywee vizuri hii helium.
 
mkuu hakuna kitu kama hiko! hizo taarifa za kijiolojia kuhusu helium gas unazo? kwa ufupi ni kwamba ishu za uwepo wa helium gas ni nadharia na kampuni ya helium one inataka kuuaminisha umma wa kimataifa uwepo wa gas hiyo ili wapate kuuza hisa zao kwa watu binafsi na makampuni.,. nimemaliza.
lost and gone
 
Nilisema na ninaendelea kusema ya kua, mwanasiasa ni mtu mmoja mshenzi na mnafiki na hasidi , hakuna mwanasiasa yuko kwa ajili ya mwananchi, ni uongo wa kutupwa, nadhani baada ya shetani kuchomwa moto kule jehanamu,atakayefuatia ni mwanasiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, tutaongea kila kitu na kukitilia shaka lakini sio suala la uwepo wa gesi ya Helium Tanzania. Hadi sasa waliosimamisha uchimbaji sio Helium One, ni serikali. Na kumbuka taarifa kuhusu uwepo wa hiigesi sio za Helium One
 
Mbona trump anataka kutuzuia kuingia kwake wakati tuna helium
 
Kwa hiyo we unaamin dunia ina miaka hiyo? ..jua tu kwamba toka yesu asaliwe ni miaka 2020 tu
Mkuu, unataka tuongee dini? Unajichanganya sana na kutoelewa ukweli wa kisayansi juu ya Biblia. Kwani Yesu aliumbwa kwa mara ya kwanza alipozaliwa na Mariam? Yesu alikuwapo mabilioni ya miaka kabla ya kuzaliwa na Mariam hiyo miaka 2020 iliyopita unayoitaja.

Na pia tofautisha kati ya dunia kuwepo na kuumbwa kwa vitu kama wanyama na mimea na bahari nk juu ya dunia. Dunia imekuwapo kwa mabilioni ya miaka ikiwa imefunikwa na maji, kabla ya uumbaji unaoongelewa katika kitabu cha Mwanzo.

Genesis 1:1-2: In the beginning God created the heavens and the earth. Now the earth was formless and void, and darkness was over the surface of the deep. And the Spirit of God was hovering over the surface of the waters.

Mwanzo 1:1-2 sio day 1 ya uumbaji, ni mabilioni ya miaka kabla ya day 1 ya uumbaji. Sasa baada ya mabilioni ya miaka katika status hiyo ya Mwanzo 1:1-2, ndipo Mungu siku moja akasema; “Let there be light,”a and there was light. And God saw that the light was good, and He separated the light from the darkness. God called the light “day,” and the darkness He called “night.” And there was evening, and there was morning—the first day (Genesis 1:3-5).

Tatizo mnaenda kanisani kuimba mapambio na kuambiwa uzinzi na kuiba ni dhambi na mnaridhika na hayo mambo madogo bila kuwa watafiti. Na mkikutana na watu wanaojua dini wakakitaka kuwaelimisha zaidi mnakuwa na shingo ngumu.
 
Mkuu, kama ungesoma mambo ya business hili la compensation lingekuwa rahisi sana kwako kuelewa.

Fikiria hili. Tuseme una kiwanda cha kutengeneza chupa za chai, na inakugharibu shilingi elfu moja kutengeneza chupa moja ya chai na unaiuza kwa shilingi 1500 ukipata faida ya Shs 500 kwa kila chupa. Na wewe ndio mtu pekee mwenye kiwanda cha chupa za chai duniani.

Sasa anakuja mtu anakuambia, nimegundua njia ya kutengeneza chupa bora zaidi na moja nitaitengeneza kwa shilingi 500 badala ya 1000 kama wewe, na nitakapoanza kuzitengeneza nitaziuza kwa shilingi 1000 badala ya 1500 kama wewe.

Utafanya nini? Kumbuka huyo mtu akianza kuuza chupa moja kwa shilingi 1000 basi wewe itabidi ufunge kiwanda chako, maana watu hawatakubali kununuia chupa zako kwa shilingi 1500 wakati zipo ambazo ni bora zaidi na zinauzwa kwa shilingi 1000 kila moja.

Una mamwili ya kufanya. Itabidi ujitahidi sana upunguze gharama yako ya uzalishaji kutoka shilingi 1000 hadi 500 ili na wewe upunguze bei hadi shilingi 1000 au hata 900 ili kuendelea na biashara. Labda hilo halitawezekana.

Njia ya pili ni kumwambia (au kumlazimisha ukiweza) yule jamaa aliyegundua njia bora na rahisi ya kutengeneza chupa, kwamba sikiliza, katika kila faida ya Shs 500 ninayopta kwa kuuza chupa zangu, nitakupa shs 250 ili usianze kutengeneza chupa zako hadi nitakapofunga kiwanda changu baada ya miaka 10. Nakupa hiyo shs 250 bure bila wewe kufanya kazi na huku rasilimali yako ya kutengeneza chupa za chai ikiendelea kuwapo na utaanza kuitumia siku mie nikiacha. Nipe hiyo mika 10 nijiandae kufunga kiwanda changu bila hasara.

Kumbuka hata ukimpa shs 250 katika faida yako, bado utapata faida, japo itakuwa imepungua, tofauti na hasara ya kufunga kabisa kiwanda chako.

Kuna wakati Bill Gates wa Microsoft aliambiwa aruhusu ushindani katika soko la operating system kwenye computer ili wateja wawe na uhuru wa kutumia operating system zaidi ya Microsoft Windows, la sivyo atapigwa faini ya mamilioni ya dola kila mwaka. Bill Gates alipiga hesabu akakuta hata akipigwa fine bado atapata faida, akaendelea na ukiritimba!

Mfano rahisi ni hivi, nikikwambia nipo hapa Moshi nakusubiri na ukiweza kufika na gari yako kutoka Dar ndani ya masaa matano nitakulipa Tshs 3M, je utajali kupigwa tochi na trafiki? Wakikupiga tochi si utakuwa unawaambia hebu niandikieni faini haraka nina haraka!

Sasa hvyo ndivyo biashara ya kimataifa inavyofanyika. Na kama umenielewa hapo juu utaelewa kwa nini kuna tetesi Tanzania inalipwa kuchelewesha uzalishaji wa Helium, na nani watakuwa wanatoa hela za kuilipa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…