Tetesi: Tanzania inalipwa mabilioni ya fedha toka nje ambazo zimefanywa siri na serikali hazina rekodi, tumenunulia ndege, na kujenga SGR na Stiegler nk

Tetesi: Tanzania inalipwa mabilioni ya fedha toka nje ambazo zimefanywa siri na serikali hazina rekodi, tumenunulia ndege, na kujenga SGR na Stiegler nk

Hapana Mkuu. Ila nawashangaa hawa wanaosema kama tulanlipwa na fedha zinatumika kujenga miundo mbinu basi sio tatizo. Suala ni kwamba, kama kweli tunalipwa, hizo fedha zinatumika zote kwa miundo mbinu? Na kwa nini zifanywe siri na kuishia huko huko nje?

Hata hivyo, labda haya ni mambo ya kawaida. Katika mambo ya uzalishaji mafuta, kuna kitu kinaitwa "signature bonus" ambayo huwa haiandikwi kwenye mkataba ni kiasi gani kinalipwa. Sasa serikali nyingi za Afrika huwa zinaamua zitakavyoitumia bila kuiingiza kwenye mifumo ya fedha za serikali. Mara nyingine inafunguliwa akounti ya nje. Na hiki ndicho chanzo cha maraisi wa nchi zenye mafuta, kama Abacha wa Nigeria, kujitajirisha sana.

Inawezekana Tanzania imefanya kitu kama hiki, kama ni kweli tunalipwa.
Oh ok sawa.

Nimekuelewa now mwanzo nilijua na wewe unajua kiasi gani tunapata basi ngoja tuite tetesi na uzushi tu.
 
Disagree.

TRA wasingetukaba hivi kama kuna chanzo kingine kikubwa cha kugharamia miradi ya kimkakati
Nakubaliana nawe mkuu Ndachuwa

Hivi tungekiwa kwenye neema hiyo, ni kwanini wafanyakazi wa umma wa nchi hii hawajaongezwa mishahara yao, ambapo ni kwa mujibu wa sheria, kwa miaka 4 mfululizo?
 
Highly unlikely, kama ni injection ya pesa nje , ahueni ingekuwa kubwa zaidi.
 
Tanzania,tualipwa ili tusiichimbe gesi yetu. Mbona hadhithi ya Abunuwasi/Alflelah Ulelah.Mtoa UZI Angalia usibadili gea bila Klachi,hiyo gari sio "Automatic gear"

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni wazi huna elimu ya kutosha kuelewa hilo ndio maana unaona kama hadithi ya Abunuwasi. Umewahi kusikia Microsoft wanafanya kosa makusudi katika monopoly ya operating systems ili walipe faini? Najua huwezi kuelewa.
 
Kasome taarifa ya ongezeko la deni la Taifa kwa kipindi cha miezi 6 ya mwisho ya mwaka 2019 hafu ndo utuambie hizo pesa za mikopo zimeenda kufanya nn.
NI wazi hazjaenda kununua Dreamliner, Airbus, Bombardier na kujenga SGR na Stiegler

Umewahi kujiuliza kwa nini serikal haina wasiwasi na ongezeko kubwa la deni la taifa? Kuna nini inachojua ambacho wananchi wala wapinzani hawajui kuhusu kuliona deni hilo ni tatizo la muda mfupi?
 
uzushi uzushi uzushi ... yaani mawazo yako unaamua kuyafanya kuwa habari ... this does not warrant my thinking
Like you said, it is your thinking....which is not necessarily the thinking of someone with common sense, right?
 
Kwa hili ni uongo,
kinywa cha JPM hakiwezi kuacha kuropoka hata kwa bahati mbaya!!
Uongo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hewaaa! Sasa jiulize. Kwanza ni kweli kwamba Tanzania imekuwa nchi pekee duniani kuwa na Helium inayoptaikana ardhini kwa wingi na ambayo itatuingizia fedha kama vile tu tumegundua mafuta.

Sasa kwa nini kinywa cha JPM ambacho unasema hakiwezi kuacha kuropoka hata kwa bahati mbaya kimekaa kimya juu ya hilo? Inawezekana hatulipwi, lakini je kuwa na Helium nyingi nazo ni porojo? Umesikia lini serikali ikiongea kwa shamra shamra juu ya Helium yetu? Kwa nini wako kimya juu ya utajiri huu?

Jiulize kwa nini ni vyombo vya nje tu ndio ninaonekama kuwa na mchecheto na Helium yetu na serikali yetu imekaa kimya kabisa juu ya hilo? Angalia hapa chini;

1579762826854.png
 
Sio jambo la kuchekelea hili.

Hawa mabbeberu wakituchoka watapandikiza watu tupigane sisi kwa sisi ili tu waje kuvuna hii gesi yetu.

Wamevuna mafuta nchi za ghuba leo hii wanajidai " sisi marekani ni njchi ya kwanza kwa uzalishaji na akiba kubwa ya mafuta" Pumbavu! sana hawa watu, waliyatoa wapi? walipiganisha nchi za kiarabu wakati wakipigana wao walikuwa wakisafirisha mafuta eti kugharamia vita.

Unafikiri Mmarekani yupo Saudia miaka na miaka kuulinda ufalme wa saudia kwa malipo gani?.

Tayari wana mafuta ya kutosha miaka 100 ijayo, bado hawana hii gasi.
 
Sio jambo la kuchekelea hili.

Hawa mabbeberu wakituchoka watapandikiza watu tupigane sisi kwa sisi ili tu waje kuvuna hii gesi yetu.

Wamevuna mafuta nchi za ghuba leo hii wanajidai " sisi marekani ni njchi ya kwanza kwa uzalishaji na akiba kubwa ya mafuta" Pumbavu! sana hawa watu, waliyatoa wapi? walipiganisha nchi za kiarabu wakati wakipigana wao walikuwa wakisafirisha mafuta eti kugharamia vita.

Unafikiri Mmarekani yupo Saudia miaka na miaka kuulinda ufalme wa saudia kwa malipo gani?.

Tayari wana mafuta ya kutosha miaka 100 ijayo, bado hawana hii gasi.
Umenena vema Mkuu.

Watu humu JF hawaelewi maana ya Tanzania kuwa nchi pekee duniani yenye Helium inayopatikana ardhini kwa wingi, ambayo inaweza kuua soko la nchi 6 pekee duniani zinazozalisha Helium kwa sasa, huku Marekani ikiwa imeshikilia asilimia 50% ya soko hilo. Watu wanaropoka bila kujua implications za jambo hili, bila kujiuliza kwa nini serikali imekaa kimya sana kuhusu huu ugunduzi wa Helium.
 
Mungu mpokee mja wako Lwajabe
Kumbeee! Mie naye siku hizi nimeanza kuchoka kwenye hesabu za kujumlisha, yaani 2+2 inanipa taabu kupata jawabu?
Kumbe habari ya Lwajabe ilianzia humohumo? Basi kuna mengine makubwa mno hayajajulikana, Ila hakika utawala wa chama kingine ukiingia madarakani watu wa kunyongwa watakuwa wengi mno na tutamtaka huyo Rais asaini utekelezaji haraka
 
Mkuu angalia mbali zaidi ya hapo. Tunalipwa fedha ambayo haiingii kwenye rekodi za serikali ili serikali iliyopo madarakani iseme sisi tuna tumia kodi za wananchi vizuri na kujipa kiki ya kisiasa kuwa wamefanya miradi mikubwa tofauti na viongozi waliopita?
Kwanini hao waliopita hawakulipwa wakafanya miradi mikubwa ili wapate kick?
 
Tetesi zlizopo ni kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikilipwa mabilioni ya fedha na kampuni za nje lakini fedha hizi zimefanywa siri bila kuingizwa katika kasri za serikali, na hivyo kuwa nje ya wigo wa ukaguzi wa serikali kutia na CAG. Hili ndilo simulizi lililopo.

Nitawawapa dondoo za mazungumzo yaliyofanyika.

"Asikudanganye mtu, suala la Tanzania kununua ndege kwa fedha za kodi na pia kujenga Stiegler na SGR, daraja la Salenda na hizo flyover na mabarabara na miradi mikubwa inayofanyika, sio kwamba ni fedha za kodi. Tanzania haina ubavu huo wa fedha za kodi kufanya miradi mikubwa kama hiyo. Mnadanganywa. Tanzania imekuwa ikilipwa mabilioni ya fedha ambayo zimefanywa siri, na uongozi wa nchi kutumia fedha hizo kama mtaji wa kisiasa".

Lakini je, fedha hizo zinatoka wapi, na kwa nini Tanzania ilipwe? Simulizi linaendelea.

"Fedha hizo ni fedha za Helium ya Tanzania. Katika nchi ambazo zimebarikiwa rasilimali asili Tanzania labda inaongoza. Kuanzia miaka ya 2010 dunia ilionekana kwamba inaishiwa gesi ya Helium ambayo imekuwa ikitengenezwa viwandani na kuuzwa kwa bei kubwa"

"Kuna nchi sita tu duniani zinazozalisha Helium kwa sasa, na viwanda 14 duniani. Karibu nusu ya hii gesi inatoka USA. na theruthi moja inatoka Qatar. Sasa viwanda vyote hivi 14 vilivyopo duniani, vinazalisha Helium kutokana na natural gas. Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo Helium imepetikana ardhini kwa wingi sana na ndio maana sasa iko katika nafasi ya kuongoza soko la Helium duniani".

"Hii gesi inapopatikana ardhini inakuwa na concentration ya wastani wa 2% na hivyo kufanya bei yake kuwa juu sana kwa kuchimba, na ndio maana inazalishwa viwandani. Sasa jambo moja la ajabu lilitokea. Mwaka 2015 wataalamu waligundua hii gesi Tanzania ikiwa inapatikana kwa kiwango cha juu sana, kati ya 5-15%. Hii ilifanya Tanzania kuwa nchi pekee ambayo ina Helium ardhini ambayo inaweza kuchimbwa na kuzalishwa kwa gharama ya chini kuliko inavyozalishwa na viwanda hivi 14 katika nchi 6 duniani. Na matokeo ni kwamba Tanzania ikajikuta katika nafasi ya kuongeongoza soko la Helium duniani, kama ambavyo Saudi Arabia inaongoza soko la mafuta duniani."

"Kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa Helium. Kufuatia upungufu wa hii gesi, Marekani hata walianza kuweka hifadhi kubwa ya gesi hii kwa ajili ya matumizi ya baadae. Upungufu wa hii gesi umefanya bei yake uongezeka kwa zaidi ya asilimia 135% kwa mwaka mmoja tu!"

"Hii gesi ya Helium ni muhimu sana na itaipaisha Tanzania kiuchumi kuliko hata kama ingekuwa na mafuta. Matumizi ya hii gesi ni pamoja na kwenye mambo kama welding na hata utaalamu wa space (kwa kiingereza uses of Helium gas: are arc welding, chromatography, medical lasers, optical fiber, intercontinental ballistic missiles, space travel, etc)"

"Lakini sasa kukawa na tatizo. Ikiwa Tanzania ingeruhusiwa kuchimba hii Helium na kuuza, basi ingeuza kwa bei poa kiasi kwamba ingeua kabisa uzalishaji wa hivi viwanda 14, USA akiwa mzalishaji mkubwa. Basi inaonekana kulikuwa na makubaliano kwamba Tanzania icheleweshe uzalishaji wa Helium hadi wakati unaokubalika. Lakini kwa kufanya hivyo, lazima kulikuwa na makubaliano kwamba Tanzaia ilipwe fedha nyingi kama "compensation" ya kuzuia uzalishaji wa Helium ili kunusuru kampuni zinazouza Helium kwa sasa. Hiyo ndiyo fedha inayofanya miradi yenu ambayo wanasiasa wenu wanawaambia eti ni kodi za wananchi ili kuji-promote kisiasa. Habari ya ugunduzi wa Heluim Tanzania na umuhimu wa hii gesi katika soko la dunia, ilipaswa kuwa kubwa kuliko kama Tanzania ingegundua mafuta. Sasa jiulize, kwa nini wanasiasa wenu wamekaa kimya kuhusu huu ugunduzi mkubwa uliofanyika Tanzania? Tanzania ni nchi pekee duniani unapata Helium ardhini na utatawala soko la dunia kama ilivyo kwa Tanzanite, na mnakaa kimya, kwa nini?"

NB: Kwa wale mnaochangia mada hii bila kufikirisha sana ubongo wenu, jiulizeni jambo hili: Je implications za Tanzania kuwa nchi pekee duniani yenye Helium inayopatikana ardhini kwa wingi, ambayo inaweza kuua soko la nchi 6 pekee duniani zinazozalisha Helium kwa sasa, huku Marekani ikiwa imeshikilia zaidi ya asilimia 50% ya soko hilo, ni nini? Jiulizeni pia kwa nini serikali yetu imekaa kimya sana kuhusu huu ugunduzi wa Helium nchini ambayo itatatuweka karibu sawa kimapato na nchi zinazozalisha mafuta?

Reference: In Photos: Massive Underground Helium Reserve Found in Tanzania
Reference: That huge helium deposit under Tanzania is even bigger than we thought
Reference:

Taarifa ya Bloomberg Businessweek juu ya Helium ya Tanzania
2019-08-28


Helium is produced on Earth by the natural radioactive decay of uranium and thorium, which are present in all rocks. But that process takes a long time—as in billions of years—so you’d need some seriously old stones. And because such old rocks don’t have a lot of gas-trapping formations, you’d need some geologic activity to break them apart and form fractures through which the helium could escape. Then you’d need heat to push the helium up through the fractures, and sedimentary formation at the surface to store it in traps between the layers of sediment, as in a reservoir.

Ballentine and colleague Diveena Danabalan identified Tanzania as one place with this kind of interplay at work. Ancient rocks formed in the African tectonic plate about 2 billion years ago, making them sufficiently old for radioactive decay to produce a lot of helium. Thirty million years ago, the plate began to pull apart, forming the Great Rift Valley, which reaches 1,700 miles from southern Tanzania up to Eritrea and the Red Sea. That process created fractures that allow magma to escape; the magma would provide the heat necessary to force the helium upward. Meanwhile, at the surface, sediments were deposited, providing the reservoirs where helium could be found. “That combination of factors makes possible helium accumulation at the surface,” says Emmanuel Kazimoto, a geology lecturer at the University of Dar es Salaam.

Among the key uses for helium today are arc welding, chromatography, medical lasers, optical fiber, intercontinental ballistic missiles, and space travel. The Large Hadron Collider, the particle accelerator outside Geneva wrestling with the biggest questions of physics, needs 120 metric tons of helium a week to keep running. Helium can make things superconductive, meaning they can transmit electricity basically forever without generating any heat, and other helium properties make the element essential for semiconductor manufacturing. Every MRI machine in the world bathes its magnetic coils in liquid helium to prevent overheating.

Like the price of lithium, the price of helium is one of the more opaque among commodities, but reports said it jumped 135% from the previous year. With such extreme sensitivity in this market, a big new helium source could, just maybe, transform a whole country’s economy. A country such as, say, Tanzania.
Mbona deni la taifa linaongezeka kama kuna pesa mbadala?? Kumbe ni tetesi! Huu ndio umbea aliosema naniliu
 
Kwanini hao waliopita hawakulipwa wakafanya miradi mikubwa ili wapate kick?
Fikirisha akili kidogo. Confirmation ya Helium Tanzania ilikuwa 2015. Sasa hao waliopita wangelipwaje kwa kitu ambacho hakikuwepo?
 
Back
Top Bottom