Tanzania inapoteza muda tungekuwa mbali kama taifa

Tanzania inapoteza muda tungekuwa mbali kama taifa

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Hili sio kwa Raisi Samia pekee ni utamaduni hata wakati wa Kikwete

1. Wakati wenzetu wa South Afica na Kenya wana enda na katiba zao za Dunia ya sasa Tanzania tunapoteza muda . Kikwete aliweka jitihada fake za kisiasa badala ya kujali nchi mwaka 2014 na 2015 kama nchi tumepoteza muda wote huu wa kuwa na katiba bora
2. Vijana kwa sasa wanatoka vyuo wanapoteza muda mitaani tu bila uchumi wala kazi za maana kwa sababu ya ubinafsi
3. Tunajua hii nchi inapenda haki lakini tunapoteza muda kwenye na chaguzi za wizi wa kura wakati kila mtu anajua hivi hatutafika
4. Kila mtu anajua jeshi letu limekuwa dhaifu tumeona hata kukimbia huko Congo lakini tunajiaminisha uongo
5. Tunajua Tanzania ni nchi ya watu wasio na furaha lakini tunajiaminisha kila kitu powa. Badala ya kutatua matatizo tunapoteza muda
6.Mkataba wa gas ni muhimu lakini tunacheleweshwa na wala rushwa wachache wanao taka 10% lakini sisi ni wapoteza muda

Tuanze utamaduni wa kujali muda wetu na vizazi vijavyo
 
Watekaji wanahitaji pambio na sio new ideas! Taifa lisilohitaji watu wa mawazo mapya, mawazo magumu, mawazo ya kuonesha pasipo wezekana panaweza kuwezekana. JPM nabalia kumpongeza alijitahidi sana yule mwamba kuonesha ukiamua unafanya jambo likaonekana
 
Wezako Wapo kalakana pumbu zinabinywa alafu unaulizwa kwa Nini baba Yako ajatumia uzazi wa Mpango
 
Hili sio kwa Raisi Samia pekee ni utamaduni hata wakati wa Kikwete

1. Wakati wenzetu wa South Afica na Kenya wana enda na katiba zao za Dunia ya sasa Tanzania tunapoteza muda . Kikwete aliweka jitihada fake za kisiasa badala ya kujali nchi mwaka 2014 na 2015 kama nchi tumepoteza muda wote huu wa kuwa na katiba bora
2. Vijana kwa sasa wanatoka vyuo wanapoteza muda mitaani tu bila uchumi wala kazi za maana kwa sababu ya ubinafsi
3. Tunajua hii nchi inapenda haki lakini tunapoteza muda kwenye na chaguzi za wizi wa kura wakati kila mtu anajua hivi hatutafika
4. Kila mtu anajua jeshi letu limekuwa dhaifu tumeona hata kukimbia huko Congo lakini tunajiaminisha uongo
5. Tunajua Tanzania ni nchi ya watu wasio na furaha lakini tunajiaminisha kila kitu powa. Badala ya kutatua matatizo tunapoteza muda
6.Mkataba wa gas ni muhimu lakini tunacheleweshwa na wala rushwa wachache wanao taka 10% lakini sisi ni wapoteza muda

Tuanze utamaduni wa kujali muda wetu na vizazi vijavyo
Prof Mama T ni shujaa wa haki na kweli miaka yoote....anayoaema hata wanaume hata wanajeshi hawawezi..kweli tunapoteza muda sanaa...chaguzi za wizi duniani tumebakia wenyeww wajinga sisi tu....sasa tunajadiki ujinga na chawa mara veta..haki lazima tunyukane ndio manbo yataenda au jeshi liamke......jeshi ni aibu kutekwa wa wanasiasa mkaacha weledi.....hata tiss ndio kabisa wapo kupanda magari yaende mbio baasii hakuna kitu....nchi imeoza kila upande wao wapo wanawalinda wanasiasa wanaibaaaaa
 
Mfano maswali machache sana
1. Tunashindwa nini kuwa na maeneo tengefu yenye vilomo vya kisasa; Mathalani huwa nawaza ukipita na treni lile eneo la Igandu upande wa kulia ukielekea Dodoma pana ardhi ndeeefu pale karibia ekari laki kadhaa! Je hatuwezi fyeka vichaka vile tukavuna maji toka ule mto wa jirani lile eneo likawekewa miundo mbinu ya kulima alizeti tuuuu na vuwanda vya kuchakata alizeti. Lile eneo linapitiwa na yreni pale kwa hiyo mzigo wa Mafuta, mashudu n.k kadhalika vinabebeka kirahisi sana. Kenya hapo wanahitaji mashudu kila siku. Nchini tuna viwanda vingi vya vyajula vya mifugo shudu likitoka hapo la kutisha bei ya vyakula vya mifugo chini.

2. Tunashindwa nini kujemga barabsra za Four ways au six way hii barabara ya Morogoro kuanzia Kibaha hafi Dodoma mjini.

3. Tunashindwa nini kuvuta maji ya kutosha kwa mda mfupi kutoka ziwa victoria na kuhudumia wananchi wetu hadi Dodoma.

4. Tunashindwa nini kugeuza ule mto pale jangwani tukaukarabati pakawa panawekwa maji, taa za urembo, boti za michezo, Mitumbwi yenye ukumbi ndani na bar (floating boats) watu wakatumia kulia bata na kufungia ndoa. Hii idea ni very common nchini Misri basi viongozi wetu wasafiri wajifunze kwa wale wenzetu

5. Tunashindwa nini kugeuza Dodoma kuwa jiji kuu la Biashara afrika Mashariki. Kwa vile treni zipo hasa za mizigo na mwendokasi, tujenge magodown na masoko makubwa na mtu yoyote anaetoa mzigo nje mfano China akionesha mzigo unaenda Dodoma anapunguziwa kodi kwa 50% kwa kifanya hivyo matani ya contena yatashukia Dodoma na vitu Dodoma vikawa bei ya chini kuliko jiji lolote Tanzania. Hivyo tunakuwa tumetoboa.


Ninayo mengi ya kushauri lakini nani atanisikiliza...ioo siku kaburi litakuwa tajiri
 
Back
Top Bottom