Mfano maswali machache sana
1. Tunashindwa nini kuwa na maeneo tengefu yenye vilomo vya kisasa; Mathalani huwa nawaza ukipita na treni lile eneo la Igandu upande wa kulia ukielekea Dodoma pana ardhi ndeeefu pale karibia ekari laki kadhaa! Je hatuwezi fyeka vichaka vile tukavuna maji toka ule mto wa jirani lile eneo likawekewa miundo mbinu ya kulima alizeti tuuuu na vuwanda vya kuchakata alizeti. Lile eneo linapitiwa na yreni pale kwa hiyo mzigo wa Mafuta, mashudu n.k kadhalika vinabebeka kirahisi sana. Kenya hapo wanahitaji mashudu kila siku. Nchini tuna viwanda vingi vya vyajula vya mifugo shudu likitoka hapo la kutisha bei ya vyakula vya mifugo chini.
2. Tunashindwa nini kujemga barabsra za Four ways au six way hii barabara ya Morogoro kuanzia Kibaha hafi Dodoma mjini.
3. Tunashindwa nini kuvuta maji ya kutosha kwa mda mfupi kutoka ziwa victoria na kuhudumia wananchi wetu hadi Dodoma.
4. Tunashindwa nini kugeuza ule mto pale jangwani tukaukarabati pakawa panawekwa maji, taa za urembo, boti za michezo, Mitumbwi yenye ukumbi ndani na bar (floating boats) watu wakatumia kulia bata na kufungia ndoa. Hii idea ni very common nchini Misri basi viongozi wetu wasafiri wajifunze kwa wale wenzetu
5. Tunashindwa nini kugeuza Dodoma kuwa jiji kuu la Biashara afrika Mashariki. Kwa vile treni zipo hasa za mizigo na mwendokasi, tujenge magodown na masoko makubwa na mtu yoyote anaetoa mzigo nje mfano China akionesha mzigo unaenda Dodoma anapunguziwa kodi kwa 50% kwa kifanya hivyo matani ya contena yatashukia Dodoma na vitu Dodoma vikawa bei ya chini kuliko jiji lolote Tanzania. Hivyo tunakuwa tumetoboa.
Ninayo mengi ya kushauri lakini nani atanisikiliza...ioo siku kaburi litakuwa tajiri