Tanzania inaweza kuanza kuzalisha ndege za watu wachache

Tanzania inaweza kuanza kuzalisha ndege za watu wachache

Kampuni ya kutengeneza ndege ya nchini Czech, inapanga kuanzisha kituo chake cha utengenezaji wa ndege nchini Tanzania.

Hii imenikumbusha aliwahi kuwepo mzungu mmoja aliunda ndege yake kwa kutumia injini za pikipiki mbao na mabati kule Njombe, inasemekana alipewa saa 24 aondoke, lakini miaka ya 1990s kulikuwepo wazungu walikuwa wanaunda ndege zao kule Kibidula Mufindi sijui waliishia wapi
 
Hivi kile cha simu kilishaanza fanya kazi?
Uki track anga ya dunia ilivyo bize kwa biashara ya ndege. Sidhani kama mwekezaji huyo yuko serious, kuanzisha huduma hiyo hapa nchini.
Aaaah wapiiii!!!
Kwa umeme gani tulio nao wakutupa jeuri hyo
Ata kwa Million za Kitanzania 1,000,0000,0000,000,000 cash, sipandi.
Tuna tatizo kubwa la kisaikolojia.
 
Uki track anga ya dunia ilivyo bize kwa biashara ya ndege. Sidhani kama mwekezaji huyo yuko serious, kuanzisha huduma hiyo hapa nchini.
Kuna fulsa ameiona mkuu, sidhani kama mkoloni atakuwa mjinga kuja hapa tena Mtwara gizani huko.
 
Ila wabongo kwa maneno wanajua kuunda vitu

Ova
 
Hio kampuni imefanya tafiti za kutosha kweli kuhusu soko. Bora wazalishe matreka au pikipiki
 
Kama wakiziuza bei chee mfano 10 M, ah lzm ninunue yaan route za kijijin nakiwasha fasta
 
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kipo hatua za mwisho za majadiliano na kampuni ya Skyleader yenye makao makuu nchini Czech ili waje kuwekeza nchini Tanzania.

Skyleader ni kampuni inayotengeneza ndege ndogo za wazi ambazo huwa na siti moja hadi mbili. Kampuni hiyo inaweza kuanza uzalishaji wa ndege hizo nchini.

View attachment 2120860
Duh.....
Sisi ndio ambao hatuko makini kabisaaaaa, mgonjwa wa kichwa tunampasua mguu, na wa mguu tunabomoa kichwa.

Hiyo ndege landing gear itasababisha ndege ikate kona
 
Mbona tunaenda spidi sana?,
Sasa hivi boda boda zinalipa sana tungeanza na hizo kwanza
 
Tanzania Ni Tajiri Ndugu Zangu
Tutavaa Nguo Sisi Halafu Ulaya Tutawauzia Mitumba
Jiwe Huyo
 
Hata kama hii nchi ni kichwa cha mwendawazimu, jaribuni kutuheshimu hata kidogo basi. Akili za kuvuka barabara tunazo.
 
Back
Top Bottom