Tanzania inayotaka kujitegemea kiuchumi sasa inarudi zama za kutembeza bakuli ughaibuni

Si bora huyu anayekuwa muwazi kuwa anatembeza bakuri, kuliko lile jamaa lililokuwa linatembeza bakuli kwa kujificha!! Hilo deni la taifa kwa miaka yake mitano limeongezekanaje kwa trilioni 25?!! Kukaa unapika data ndio ushujaa? Hadi hao WB, IMF, wanakushangaa kwani huyu jamaa hizo data zake anazitoa wapi!!

Jamaa alikuwa mshambaa sana, yaani vyombo vya dunia vilivyo na kazi ya kutathimini ukuaji wa uchumi wa dunia, hutaki kuviamini eti unalazimisha watu waaamini hicho chako? Dunia nzima uchumi kila leo unayumba ila wa kwake unakuwa tu hadi kuna kipindi hiki cha covid 19, akiwa mkoani alisema umefikia 8%, hahaa ila mwendazake jamani!!

Wanaokupa pesa wako hoi ila wewe unaepewa uko vizuri!!! Sasa huo uchumi wa kati wa chini JK alituacha kwenye nadhania kwenye pato la tsh.1070, sasa tupo kwenye 1090 ongezeko la 20 kwa miaka 6! Na malengo ya serikali ilikuwa kufikia 2025 tuwe uchumi wa kati wa juu 1200!! Hapo tusingeweza kutoboa!! Bora mama anakwambia kwa sasa tupo kwenye 4.7%. Muacheni afanye kazi.
 
Wafadhili wagharamie uchaguzi mkuu! Wao uchaguzi wao unagharamiwa na nani?!

..tunatumia billion 180 kwa uchaguzi, halafu tunakwenda kuomba wafadhili watusaidie kwenye elimu na afya?

..mimi kwa mtizamo wangu ni bora tutembeze bakuli kwa ajili ya uchaguzi, lakini afya na elimu tutumie fedha za ndani.
 
..tunatumia billion 180 kwa uchaguzi, halafu tunakwenda kuomba wafadhili watusaidie kwenye elimu na afya?

..mimi kwa mtizamo wangu ni bora tutembeze bakuli kwa ajili ya uchaguzi, lakini afya na elimu tutumie fedha za ndani.
Hatuwezi kugharamia hivyo vyote bila kutembeza bakuli?! Siku hao wafadhili wakigoma kusaidia serikali inaanguka? Nakumbuka Kenya kipindi cha Kibaki walikatiwa misaada yote toka nje pasipo kutetereka.

Mimi naona tatizo kubwa la nchi yetu ni kwenye vipaumbele. Kama taifa hatujui tunahitaji nini, na wakati gani.
 
Vipi bei huko na vipi halmashauri hawamind?
Bei ya soko Bado sijajua ila mimi huu ni utaratibu wangu tu huwa nawahi mapema Sana, nanunua kwa kilo 1000[ maana huu ni ule wa mwanzo unaowahi kukauka na wanunuzi wanakuwa hawapo

Halmashauri huja kuanzia wa sita katikat ukichanganya
 
Bei ya soko Bado sijajua ila mm huu n utaratibu wangu tu huwa nawah mapema Sana nanunua kwa kilo 1000 maana huu n ule wa mwanzo unaowah kukauka na wanunuz wanakuwa hawapo

Halmashauri huja kuanzia wasita katkat ukichanganya
Poa mkuu mimi nipo huku Dodoma ndiyo unaanza
 

Hivi hujui kwamba budget ya Afya ni pesa ya Marekani $600 kwa Mwaka hii nayo ni bakuli au mpaka waseme. Tofauti ni kuishi kwa tabia za uongo
 
Kuna mkataba gani uliosainiwa awamu ya 5 ambao uliwekwa hadharani?
 

..hapo kwenye vipaumbele nakubaliana na wewe.

..kwa mfano, mimi napinga manunuzi ya ndege ambayo yametugharimu trillions of shillings.

..yaani tumewekeza kwenye viwanda vya mabeberu kununua madubwasha yatakayotutia hasara kwa miaka mingi ijayo.

..halafu baada ya hapo tunakwenda kuwaomba haohao mabeberu watusaidie ktk sekta za afya na elimu.

..kwenye kutembeza bakuli kwa ajili ya uchaguzi nilikuwa nazungumzia mfano halisi. tumetumia billion 180 kuendesha uchaguzi wa hovyo. ni afadhali fedha za uchaguzi zingekuwa za wafadhili, halafu hizo bilioni 180 za ndani zikatumika kwenye miradi ya maendeleo.
 
Mfuate jiwe
Kwa hasira hizo utanitangulia wewe ukaniandalie makao...Maisha hayana stress ukiwa na moyo wa upendo...Ukiwa na gundu kama lako utakufa kwa shinikizo la damu kwakua kila mara usiyempenda anakujia...
 
Mkuu Mambo ya uchumi waachie uchumi.

Ukiharibu uchumi ni sawa na kutoa mimba. Itabidi ukae muda fulani upite mwili urecove Kisha mchakato wa kupata mimba ingine ifanyike.

Kwa lugha nyepesi ukiubomoa uchumi utahitaji muda mrefu kuujenga kuliko muda uliotumia kuubomoa.

Sasa mjengaji lazima atumie mbinu mpya na mabadala kuujenga upya. Sasa mama Samia anaujenga upya uchumi wetu.

Kuna kitu kinaitwa open and closed economy, mwendazake alichukua approach ya kufunga uchumi.

Fanya kila kitu mwenyewe, timua wawekezaji wa nje na hata kufrustrate wa ndani na kuondoka kwenye Kenya, Rwanda, Zambia na Malawi. Sasa tunaenda kufungua upya uchumi.

Suala la kukusanya Kodi lipo pale pale
 
Kwa hasira hizo utanitangulia wewe ukaniandalie makao...Maisha hayana stress ukiwa na moyo wa upendo...Ukiwa gundu kama lako utakufa kwa shinikizo la damu kwakua kila mata usiyempenda anakujia...
Like son like father
 
Mataga sasa hivi watalaumu kila mtu anaye msifia mama Samia
 
Kwa hasira hizo utanitangulia wewe ukaniandalie makao...Maisha hayana stress ukiwa na moyo wa upendo...Ukiwa gundu kama lako utakufa kwa shinikizo la damu kwakua kila mata usiyempenda anakujia...
Interahamwe kazi mnayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…