Tanzania insists EAC citizens MUST use passports to enter Tanzania

Hilo la karo serikali ilifanyie kazi wanyarwanda walipe ada sawa na waganda.

Cc: Mwigulu Nchemba
 
Wewe hapo ndio unaona gari mbovu, lakini sisi tunaosafiri na gari lenyewe hatuoni ubovu wake, leo hii kamuulize Mnyarwanda anayesafiri kwa kutumia ID kutokea Kigali hadi Nairobi, halafu hilo swali kamuulize Mtanzania anayefanya biashara kwenye mataifa ya EAC.
Changamoto zitakuwepo, hata waliobuni ndege walikumbana na changamoto, ila leo zinapaa. Nyie mumekaa kama fisi, hamtaki kuhusika kwenye uwindaji, mnakaa pembeni kuwacheka wanaohangaika kufanikisha, halafu mnalia mumetengwa.
Tanzania ilituzungusha kwenye mbuyu hadi ikaamua yenyewe ikae pembeni na mdogo wake maskini Burundi, baadaye mkaanza kulia eti mnatengwa.
 
We Africans tend to misunderstand the concept of federalism in my view. Federalism is about finding the balance between self rule and shared rule, about being a unified entity and maintaining diversity and difference. Harmonizing is different from unifying. If one member state wants to do something they should be allowed that freedom as long as they don't violate certain fundamental agreements.
EAC would work if we all looked at it that way.
Tatizo we think kuungana ni kufuta mipaka and all that.
 
Kenyatta ndio aliyetuweka pembeni, hata Mungu analijiwa hilo. Chuki yake binafsi ndio iliyo mfikisha hapo (sitaki kuongele ni chuki ipi lakini ukweli ipo).

Tanzania bado hatujakamilisha zowezi vitambulisho vya taifa, mfanyabiashara wa Tanzania anatambuwa ili kusafiri au kufanyabiashra nje ya Tanzania, anahitaji kuwa na hati ya kusafiria (passport). Ni swala lililo wazi kwa watanzania wote. Sasa kwanini na nyinyi mtu anaetaka kuja Tanzania kufanyabiashra anashidwa kuomba passport kama raia wengine?? Au Kenya inashindwa kugawia passport kwa raia wake?? Tunajuwa vitambulisho vya Kenya vinavyopatikana kwa njia ya rushwa. Kuna watu wengi sana hata mimi nawajuwa wanavipande vya Kenya na sio raia wa kenya. Leo hii mnaenda kukubaliana kutumia vitambulisho na kutulazimisha na sisi tukubali wakati mnajuwa jinsi idara zenu za uraia zilivyo gubikwa na rushwa.

Hatuwezi kula matapishi ya Kenyatta, mkitaka kuelewana leteni mjadala mezani tuuchambue tujiridhishe, vinginevyo mtakuwa mna jitekenya na kucheka wenyewe.
 

Kwamba Tanzania bado imechelewa kwenye kuwapa raia wake vitambulisho, sisi hatuna tatizo nalo na ndio maana mkaomba mkae pembeni mjiandae, mtafakari mfanye yote ili muwe tayari baadaye. Tatizo ni pale mnaanza kulia kwamba mumetengwa ilhali wenyewe ndiye hao baada ya kutuzungusha kwenye mbuyu baadaye mkaomba mkae pembeni kwa baadhi ya mambo.

Kuhusu ufisadi wa kuwa na vitambulisho ni tatizo linalokumba hata mataifa makubwa, hilo sio la kutupigia makelele na vijisababu vyenu visivyoisha, nakumbuka siku fulani hata waziri wenu Mwigulu Nchemba aliwahi kusema mwenyewe kawaona Wachina wana hadi vitambulisho vya kupigia kura. Sasa hadi upate cha kura lazima uwe na cha kitaifa, hebu tafakari.
 
Hata hiyo EAC hatuitaki.
 
Wanataka waje watuletee Al Shabab na kumiliki ardhi ndivyo sivyo! Kenya yenu kubwa kaeni kwenyu kha!
Acha hizi. Tazama vile watu wanadadavua hoja kisomi, wewe unakuja kuchafua na hizi hoja zako mikebe. Kaa kando kama mimi na ufiatilie tu.
 
Developer hana passport?? Basi kazi zake zote ai azifanuie naivasha mombasa kiwangare na kericho?
Ila akipata offer ya kwenda USA pasport ataipata ndani ya dakika moja.

Hivyo ina maana kila developer kwenu ana passport? Sio kila mtu huwa amekaa mkao wa kutoka nchini kwao. Hata kule USA utakuta kuna madeveloper hawajawaza kutoka hiyo USA unayoishobokea.

Binafsi kwa maisha yangu yote sikua nawaza kutoka nje ya nchi yetu, ila siku moja ghafla offer ikanikuta ya kutakiwa niende Hongkong ili kuhuduhuria mafunzo ya mfumo fulani wa teknolojia walitaka kuuanzisha EAC. Tatizo sikua na paspoti, wakati wenyewe walikua wanalipia kila kitu, usafiri na malazi na mambo mengi, nilikua bado kijana kijana hivi, hivyo niliishia kuwaona wenzangu wakivuka kwa KQ hadi ikaniuma. Baadaye nilifuata pasport, hivyo sio kila mtu hukaa mkao wa kutoka kwenye nchi yao.

Na pia developers wengi wanabadilishana mawazo hapa EAC na usije ukashangaa kuna wale wanaalikana ili wasaidiane kwenye mambo fulani fulani. Kuwekea watu vizuizi ni jambo ovyo sana.
 
Unarusha ajenda, hivi ile mikutano ya CoW Tanzania ilialikwa au Kenya ilibana mualiko?? Waambie umati wa wanamtandao kama Tanzania ndio ilikataa au Kenya ndio iligoma kutoa mualiko?

Nchi nyingi duniani hazina vitambulisho, na sisi Tanzania kama nchi baada ya uhuru tulilikataa. Hata wale walio wafundisha vitambulisho (Uingereza) hawana vitambulisho walivikataa. Vitabulisho vyenywe ya Kenya wala sio salama, wasomali, wanaigeria, walaiberia wanavitumia kila siku kuingia Kenya na kufanya mambo yao ya ajabu. Utaratibu upo na unajulikana ukitaka kuja Tanzania omba passport kama huna, imekula kwako.
 

Sio Kenya ilikua inaalika vikao vya CoW, kuna secretariat. Pili, Tanzania mara nyingi ilikua inatuma waziri au wawakilishi wake wa kuzuga maana wenyewe mlishasema tuendelee na mengine halafu mtakuja ungana nasi hapo baadaye. Tatizo mkaishia kulia lia baadaye kwamba mumetengwa.

Halafu hakuna sehemu nimerusha ajenda, nimesema waziri wenu aliwahi sema kwamba amewaona wachina na hizo stakabadhi, sasa hapo nimeruka vipi, nimekuambia tatizo la kughushi stakabadhi lipo duniani kote hata Marekani.
 
Izi figisu figisu ndo huzorotesha umoja wetu..ivi agenda kuu za EAC ninin kama hata kusafiri nako kunavizingiti
 
Haha, mikutamo mutatu ya kwanza yote Tanzania haikuona mualiko wala salamu. Mkiulizwa mnasema Oh, haya ni maswala ya nchi tatu huru, wakati nyuma yenu kuna bendera ya EAC. Mawaziri watanzania walianza kuja baada ya Museveni kuomba suluhu. Lakini hata hivyo na mpaka leo hii, yote yaliyoongelewa mnashidwa kutueleza faida iliyopatikana.

Kudakuliwa vitambulisho sio sifa kusema turuhusu mkenya yoyote aigie kwetu eti dunia nzima nyaraka zao zinadakuliwa. Miaka ya karibuni udakuzi wa hati za kusafiria umeshuka sana kutokana na usalama wa hizo hati na taarifa zake kuwekwa kwenye mitandao ya kidunia. Sasa kwanini tusitake kutumia nyaraka iliyokuwa na uhakika kuliko vitambulisho vinavyoweza kutengenezwa na wajanja wa River Road.
 
Why are we trying to convince these people on something everyone knows. Easy movement of people, more business, more revenue. As a kenyan if I want to visit any of the EAC countries, I am now more likely to go to either Ug or Rwanda, vice versa... It is a reality. I will visit these 2 countries and tz wont even be in my plan. All that hustle...
 
Visitor?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…