Tanzania irudi kwenye mfumo wa chama kimoja ili kukomesha ukoloni mamboleo

Tanzania irudi kwenye mfumo wa chama kimoja ili kukomesha ukoloni mamboleo

mroki

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2021
Posts
324
Reaction score
285
Nilikuwa kwenye pitapita zangu YouTube nikakutana na video hii


View: https://www.youtube.com/watch?v=8blC9qfUya8&t=222s

Kwenye hii video utajifunza kuwa taifa le kigeni tena siyo taifa jirani bali taifa ambalo liko mbali kabisa na nchi yetu limeamua kuingilia siasa za ndani ya taifa letu bila aibu na tena linaegema upande mmoja bila kujali matakwa ya wananchi. Basi swali langu ni hili...

Kwani mustakabali wa taifa la Tanzania unaamuliwa na nani? Watanzania wenyewe au wamarekani? Vipi kama watanzania walio wengi wanapenda utawala wa CCM na hawawaelewi hata kidogo vyama vya upinzani? Kweli marekani inaweza kulazimisha mambo yake kwa taifa letu? Huo si ukoloni mamboleo sasa?

Mimi nashauri kama wapigakura watajitokeza kwa wingi mwaka huu ijapokuwa CHADEMA wamejitoa kwenye uchaguzi iyo iwe ishara ya kuwa wananchi wameridhia nchi irudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Kwa hiyo serikali iandae referendum wananchi wachague ama nchi ibaki na chama kimoja au tuendelee kwenye mfumo wa vyama vyingi na kura zipigwe kwa njia ya sms kwa maana kila laini ya simu ya mtanzania imesajiliwa kwa kitambulisho cha NIDA.

Na kama wananchi watanzania wataamua nchi ibaki kwenye mfumo wa chama kimoja basi huo ni uamuzi wao wa kidemokrasia na Marekani watakuwa hawana haki ya kusema vinginevyo. Katiba itabadilishwa na mfumo wa chama kimoja utarejea na yeyote atakeyekwenda kinyume cha sheria atashughulikiwa hatua kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom