Tanzania iruhusu watu binafsi kujenga nyumba za kuhifadhia maiti (Mortuary rooms)

Tanzania iruhusu watu binafsi kujenga nyumba za kuhifadhia maiti (Mortuary rooms)

Biashara nyingine NI kukaribisha maroho machafu tu
Nilishawahi kumshauri mtu nimwandikie business plan ya biashara hii akaogopa ila ni biashara nzuri na kwa sasa inalipa sana kwa siku maiti ya mtu mmoja inalala kwa 30,000/- nje ya huduma nyingine hivyo ukiwa na 4 friji inayoweza kuhifandhi maiti tatu kila moja utahifadhi miili 12 zaidi ya mtu mwenye vyumba 10 vya guest unachofanya ni kutoa fungu la kumi ili ilinde biashara yako.
 
Sasa huyo marehemu atakuwa kafia wapi ?.
nyumbani au hospital?
Hahahahaha!

Hii nayo ni point nzuri mkuu. Ila mtanilaliaje? Kuingiza mwili hadi mtoe pesa, sio bure bure tu.

Mtu anaweza kuanzisha huduma hii aka target middle income eaners maeneo ya mjini kama Dar- Na akaweka huduma na bei ambazo ni za katikati (sio za juu sana). Anaweza kupata mid-income eaners wengi wafanyakazi na wafanyabiashara wa kati ambao watapenda kuhifadhi wapendwa wao kiheshima zaidi.

Au pia anaweza kutarget high income eaners wale matyta wa mjini hapa. The likes wanaotibiwa Aga Khan na zinazofanana na hizo.
Sio kwamba kitu kama hii mtu akajenge Sitimbi
 
Wadau hivi Bongo ukiachana na Mortuary zilizopo ndani ya hospitali, Mbona hakuna Mortuary ambazo Mtu/Kampuni zinamiliki private? i.e high class/ VIP mortuary?

Mfano kwa wenzetu Kenya, hii fursa watu wameitumia kweli kweli na kuna private mortuaries nyingi tu watu wamezitengeneza, na wengi wanazitumia huduma hizo pale wanapofikwa na janga la msiba kwenye familia zao.

Kwa shida ya upungufu na ubora hafifu wa vyumba vya mortuary kwa hospitali nyingi ninayoiona kwenye hospitali nyingi za bongo, hii inaweza kuwa biashara nzuri tu bongo na ikalipa vizuri tu, kama watu wenye uwezo wakiwekeza huko.

Ni watu hawajaiona hiyo fursa au wabongo hawataweza kuzilipia?

Au taratibu zetu za kisheria haziruhusu? Kama sheria zetu haziruhusu, zifanyiwe marekebisho ziruhusu hilo, ni fursa nzuri sana. Watu watapata pesa na serikali itapata kodi.
Ni wazo zuri ila kuna mambo yasiyofaa yatafanyika huko, tujifunze kutoka kwenye ubinafsishaji mwingine uliofanyika huko nyuma, possibly wawekezeji namba moja watakuwa ni hao wafanyakazi wa mochuari wa sasa
 
Hii biashara ukipata body freezers,machela za kubeba maiti,ukiweka sinki ya kuoshea maiti na mazagazaga mengine machache,
Ukiwapata na wanaojua kushikashika maiti
Biashara tayari utapiga hela mpaka basi

Ova
 
Ndo nimeanza kuulizia ulizia kwa wahusika. Seems ni kitu ambacho hakijakatazwa popote. Acha niendelee kufanyia tafiti hili suala, pamoja na gharama involved.
Daktari umeleta wazo la kimapinduzi kabisa. Ukiona wachangiaji wanavyoona ukakasi maana yake unawatia ujasiri wa kuona jambo kwa uhalisia wake.

Hii huduma ni muhimu sana kwenye jamii kama ilivyo huduma ya majeneza.
Nina imani hata waanzilishi wa biashara ya majeneza walipata upinzani mkali na pengine hata kupigwa kwa kuleta uchuro kwenye jamii...ila kwa sasa ona inavyosaidi.
Hivyo nikutie moyo, pambana.

Idadi ya watu inaongezeka kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba huko mbeleni vyumba vya maiti vya hosipitali pekee havitakidhi uhitaji.
 
Yaani hata niwe BILIONEA siwezi KUJENGA monchwari
Kwa nini mkuu? Mbona ni huduma tu mkuu kama huduma zingine? Wote tutakufa, hilo wala si jambo la shaka.
Ni kama huduma ya wanaotengeneza na kuuza majeneza tu mkuu. Wanasaidia jamii (wahitaji), na pia wanapata namna ya kuendesha maisha yao. Kwa nini watu wengi mmekua na uoga sana juu ya hii huduma?
 
Biashara nyingine NI kukaribisha maroho machafu tu
Roho chafu kivipi mkuu? Roho chafu zipo tu mkuu unafikiri zinapatikana kwa kuanisha mochwari au kuuza majeneza?
Hii concept sio sahihi mkuu. Unaweza ifanya hii biashara kwa ufanisi na uaminifu mkubwa bila kuhusisha roho chafu; Roho chafu kukaribishwa ni tabia ya mtu tuu... Wapo wanaouza chakula tu ila roho chafu ndo zimejaa kwenye maeneo yao ya biashara kwa sababu wamezikaribisha na kuzitegemea mkuu!
 
Ni kweli ni huduma muhimu lakini mfanyabiashara si ana haki ya kuchagua biashara anayoitaka? Biashara ya kudeal na wafu inatisha Mkuu.
Nimekuelewa mkuu. Mimi naendelea kufuatilia zaidi. I am excited about this opportunity. Wacha nifuatilie upande wa gharama. Nimesha conform hii kitu inaruhusiwa nchini, wala haijakatazwa, tena kuna miongozo kabisa ya wizara ya vitu gani uzingatie.
 
Daktari umeleta wazo la kimapinduzi kabisa. Ukiona wachangiaji wanavyoona ukakasi maana yake unawatia ujasiri wa kuona jambo kwa uhalisia wake.

Hii huduma ni muhimu sana kwenye jamii kama ilivyo huduma ya majeneza.
Nina imani hata waanzilishi wa biashara ya majeneza walipata upinzani mkali na pengine hata kupigwa kwa kuleta uchuro kwenye jamii...ila kwa sasa ona inavyosaidi.
Hivyo nikutie moyo, pambana.

Idadi ya watu inaongezeka kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba huko mbeleni vyumba vya maiti vya hosipitali pekee havitakidhi uhitaji.
Kwa kweli hata mimi watu wanavyokua negative na kuipondea ndo nazidi kuwa excited kuifuatilia zaidi.
Risk takers na wafanyabiashara wakubwa wanajua kuwa idea ya biashara ambayo kila mtu anaipinga hiyo ndo ya kuifanya, na the opposite is also true.
Kumbe hiyo kitu inaruhusiwa nchini na kuna miongozo kabisa ya vitu gani vya kuzingatia, na ni mamlaka zipi zinatoa kibali. Naendelea kufuatilia zaidi na zaidi.
Mkuu, ukweli ni kwamba hata kwa hali ya sasa hivi tu mochwari zilizopo mahospitalini hazitoshi kabisa kulingana na uhitaji mkubwa uliopo. Hii kitu kama nikitengeneza mjini Dar hapa, inaweza ku take off vizuri tuu. Wacha niendelee kujifunza zaidi.
 
Uendeshaji wake nafikiri utakuwa mkubwa sana kutokana na wateja wachache
Umeme pia ni shida kwa hiyo ni lazima uwe na backups ya generator on site

Kama itatokea una maiti chache sana itabidi uwashe tu umeme 24/7

Ni idea nzuri ila lazima uwe umewekeza vizuri
 
Hii biashara ukipata body freezers,machela za kubeba maiti,ukiweka sinki ya kuoshea maiti na mazagazaga mengine machache,
Ukiwapata na wanaojua kushikashika maiti
Biashara tayari utapiga hela mpaka basi

Ova
Kuna muongozo nilikua napitia hapa mkuu juu ya utaratibu wa kuanzisha hii kitu; Ni lazima pia uwe na mtaalamu/wataalamu wenye mafunzo ya kutreat mwili ambao wamefuzu mafunzo ya mortuary attendant; Pia, ni lazima hii biashara isimamiwe na mtu ambae ni dakatri (MD/DDS), au muuguzi, au mtaalamu wa maabara.
Hivyo, ni lazima uajiri wataalamu pia mkuu!!
 
Uendeshaji wake nafikiri utakuwa mkubwa sana kutokana na wateja wachache
Umeme pia ni shida kwa hiyo ni lazima uwe na backups ya generator on site

Kama itatokea una maiti chache sana itabidi uwashe tu umeme 24/7

Ni idea nzuri ila lazima uwe umewekeza vizuri
Yes mkuu, ni idea ambayo inahitaji uwekezaji mkubwa, hilo nakubaliana na wewe!
 
Zipo kuna sehem ilikuwepo wakahamia sehem flan hiyo nyumba hadi leo haipati wapangaji tetesi ni imeuzwa tena ilikua karibu na kituo kikubwa cha radio...

Ilikua ni mortuary na Pia wanafanya maandalizi ya msiba nk
 
Back
Top Bottom