Tanzania iruhusu watu binafsi kujenga nyumba za kuhifadhia maiti (Mortuary rooms)

Profesa Shaba ali import vifaa kabisa nadhani mpaka leo 30 years later bado viko bandarini.
Alipata upinzani na ukiritimba mkubwa sana kutoka serikali pendwa.
Nilishasikia hii kitu. Mpaka mwekezaji aliyekua patna na shaba akaondoka nchini akasusa na project yenyewe. Sijui kama kuna ukweli au la
 
Nilishasikia hii kitu. Mpaka mwekezaji aliyekua patna na shaba akaondoka nchini akasusa na project yenyewe. Sijui kama kuna ukweli au la
Duuhhhh....!!! Noma sana. Sijawahi kabisa kuisikia hii story. Ngoja, nitafuatilia zaidi kwa wadau nipate insights zaidi juu ya hiyo story na kujua kama ni ya kweli
 
Kuna mji fulani hospitali haina hiyo watu wakifa mait inalazwa chini au ipelekwe umbali wa zaid kilomita 25 kuifadhiwa kisha ifuatwe cku ya mazishi sasa nikamshauli mdogo wangu afanye biashara hiyo alikataa na hata alipowaambia watu ktk familia walikataa kabisaaa
 
Wabongo tuna uoga fulani wa ajabu hivi...!!
Wakati ni kitu kizuri kabisa, tena kwa wale waamini unapata thawabu kwa Mwenyezi Mungu, maana unashiriki kitu muhimu sana katika kuupatia hifadhi na heshima inayostahili mwili wa binadamu mara baada ya roho kuachana na mwili. Haina ubaya wowote. Basi tu mawazo ya watu.
 
Mleta mada wewe ni katili. Nyinyi ndo watu mnaomba kila wakati watu Wafe biashara zenu zichanganye
 
Zipo kuna sehem ilikuwepo wakahamia sehem flan hiyo nyumba hadi leo haipati wapangaji tetesi ni imeuzwa tena ilikua karibu na kituo kikubwa cha radio...

Ilikua ni mortuary na Pia wanafanya maandalizi ya msiba nk
Karibu na mawingu?
 
Mbonq mortuary zipo nying sana za jumuiya nje ya government kama dar misikiti mikubwa karibu yote zina mortuary temeke kina masjid alqadiria kariakoo kuna manyema mtoro upanga kuna maanur town kuna masjid jabir bin zaid na magomen pia kuna masjid nying zina huduma hizo ilala pia
 
Pale Himo, Moshi nimewahi kuona Private hospital moja ina mortuary yake nzuri tuu na huduma safi kabisa,sema siyo kubwa sana.
 
Mleta mada wewe ni katili. Nyinyi ndo watu mnaomba kila wakati watu Wafe biashara zenu zichanganye
Mkuu vipi tena kuniita katili hata hunijui?
Kwa hiyo wauza majeneza nao ni makatili? Wao wanapata faida pale watu wanapofariki na kutoa huduma ya majeneza.
Na madaktari wa binadamu pia ni makatili? Maana wao watu wanavyoumwa ndo wao wanapata faida.
Mawakili je? Wao nao makatili, maana watu tusipoibiwa, tusipotapeliwa, tusipobakwa watapata wapi faida?
Mkuu ukiangalia maisha kwa namna hiyo basi watu wengi sana hapa duniani ni makatilil.
Look at it this way: Mtu anatoa huduma ya mortuary ili kuwezesha pale ambapo mtu amefariki basi aweze kuhifadhiwa kwa heshima na kwa stahiki inayotakiwa.
 
Ok. Hii nilikua sijui mkuu kiukweli. Kumbe misikiti mikubwa Dar wana mortuary zao kabisa ambapo wanai-treat na kulaza miili ya marehemu? Nitajaribu kutembelea kwenye msikiti mmojawapo nijifunze pia.
Shukrani.
nanawoo
 
Pale Himo, Moshi nimewahi kuona Private hospital moja ina mortuary yake nzuri tuu na huduma safi kabisa,sema siyo kubwa sana.
Yeah, kwenye hospitali mortuary zipo... Sema ndo hivyo hazikidhi mahitaji kama ulivyosema hiyo ambayo umeitaja ni ndogo. Ndio maana nikawaza kuwa na kitu cha private kwa huduma hiyo tuu! (siyo hospitali, bali mortuary room tu).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…