Tanzania isiwe na vazi moja tu la Taifa, tuwe na mavazi rasmi matano kutoka katika makabila yetu

Karne hii ya leo unawaza vazi la kitaifa? Ili iweje? Watu tunahitaji maendeleo hatuhitaji mavazi ya kitaifa ili hali matumbo ya njaa, kila utamaduni umeachwa ukisema hauna maana, leo hii nyumba unayoishi unaishi na kinyesi humo humo ukiita self contained, watoto wako au wadogo zako wanasoma shule kwa lugha ya kiingereza si ungewafundisha lugha ya kabila yako tukuone wewe kweli unajali utaifa wako.
Haya mambo yalishindikana enzi za myerere alipokuja na maduka ya ujamaa, vijiji vya ujamaa nk, hakuna namna utaforce watu wafanane.
 
Ni ngumu kwa tanzania kutambulika kwa vazi rasmi la Asili sababu ya diversity ya mila na tamaduni zetu..makabila yetu mengi asili zao ni za kihamiaji


Nchi ambazo wanatambulika kwa mavazi yao ya Asili utakuta makabila yao machache yameingiliana had lugha yanafana

mfano Burundi na Rwanda watutsi na wahutu ni makabila yanayofautiana kdg kidesturi ila ila
lugha moja tamaduni kias kikubwa zinafanana hadi mavazi.. ndo maana ni rahis kurasimisha

same kwa ethiopia. wanaijeria na wengine hadi west africa.. angalia mavaz ya kiwest africa.. mtu wa senegal, Cameroon .. ghana. na kwingine mavaz yanafanana maana nao wameingiliana makabila. yako machache lakini yameingiliana

sasa sie makabila yetu kiasili yameshabihiana na makabila na tamaduni za watu wa inchi zingine maana kiasili makabila mengi hapa wahamiaji..

mmakonde kahamia, huko kaskazin ndo yale yale
wachaga na wamburu plus wamasai.. hapo kati wasandawe, wabarbaig wagogo hawana tofauti na watu wa jangwa la namibia na zimbabwe. warangi hawana tofauti na waethiopia

usishangae ukivaa kama mgogo watu wa west africa au ulaya wakahisi umevaa kama watu wa wa Namibia na zimbabwe.. maana wao kule watu wao wabush kwa ujumla wao ndo vazi lao na wanajulikana dunian utaonekana umeiga

ukivaaa kama lubega ya shuka jeupe kama wahaya aidha upelekwe Rwanda , au uganda

kimasai.. tumeingiliana na Kenya so huwezi kuliita vazi asili la tanzania

sie tamaduni na desturi tunashea na watu wa nchi zingine .. so hatuwez tambulika kwa vazi maana makabila yetu kiasili ni wahamiaji tu hapa
 
Ni ngumu kwa tanzania kutambulika kwa vazi rasmi la Asili sababu ya diversity ya mila na tamaduni zetu..makabila yetu mengi asili zao ni za kihamiaji
Ila kumbuka nchi ya South Africa imefanikiwa katika kurasimisha lugha
 
Hii nimeipenda sana mkuu. Asante kwa kunipa somo zuri.
 
usishangae ukivaa kama mgogo watu wa west africa au ulaya wakahisi umevaa kama watu wa wa Namibia na zimbabwe
Wakihisi ndio tunawapa ufafanuzi kuwa hili ni vazi la Tanzania.

Alafu kwanini wahisi umevaa kama Namibia? Kwanini akivaa mtu wa Namibia wasihisi amevaa kama mtanzania?
 
Kwanini lubega na mavazi ya kimasai yatambulike kuwa ni ya nchi zingine na sio Tanzania? Kwani ni nani amekwambia dunia nzima wanajua wamasai wapo Kenya pekee?
 
Kwani ni nani amekuforce ufanane na mwingine?
Jiulize kwanza ikiwa haukutaji watu wa kufanana na wewe kwa nini usishone la kwako ukavaa?
Ila kumbuka nchi ya South Africa imefanikiwa katika kurasimisha lugha
Kwa hiyo umetoka kwenye vazi umeenda kwenye lugha, na mbona tanzania imerasimisha kiswahili unahitaji lugha gani? ni kijiji gani Tanzania utaenda uongee kiswahili watu washindwe kukuelewa?
 
Wakihisi ndio tunawapa ufafanuzi kuwa hili ni vazi la Tanzania.

Alafu kwanini wahisi umevaa kama Namibia? Kwanini akivaa mtu wa Namibia wasihisi amevaa kama mtanzania?


simple jamii yao kule ni famous tayari.. ni kama vile huko ghana kuibuke kabila wanavaa kama
wamasai.. we unafikir ukiona picha utajuankama ni kabila la ghana.. hapana utajua ni mmasai wa east africa sababu tayar vazi wamasai kwa wingi wao wameshalitawala hilo vazi..

so hata kama kuna kabila dunian wanavaa kama hivyo inabid mvaaji awe anatoa maelezo yanziada vinginevyo anatupwa east africa

so kwa makabila yetu toka enzi na enzi hatujawa popular kwenye mavaz ya asili dunian isipokuwa
wamasai sasa ukianza leo itabid uanze kutoa maelezo ya ziada tena ili wayashike hayo maelezo inabid ufanye kitu unique

masai life style yao ya kuhama hama ni kama
jamii zingine ila ile ya wao kuishi na mavaz yao na silaha popote alipo hata town ndio imefanya vaz likawa famous

wengine sie wagogo au wahaya akija town anatupa lubega anaingia mjini sarawili

halafu pia tunataka dunia itutambue kwa mavaz asili vaz wakat humu ndan wenyewe inatupa shida kujua kabila gani vaz lake la asili ni lipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…