K Mwita
JF-Expert Member
- Oct 11, 2016
- 356
- 314
Pole sana mkuu. Wewe ni moka kati ya watu ambao ninawaheshimu sana humu. Akupe fidia yako huyo jamaaSio wote matapeli mkuu, tuombe radhi sisi wastaarabu wachache.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole sana mkuu. Wewe ni moka kati ya watu ambao ninawaheshimu sana humu. Akupe fidia yako huyo jamaaSio wote matapeli mkuu, tuombe radhi sisi wastaarabu wachache.
Hivi Tigo wana ofisi wapi huku Katavi?Ninaona unawafanyia marketing kiujanja hao mabosi wako
Anaropoka tu huyo marketing ataijulia wapi?Ninaona unawafanyia marketing kiujanja hao mabosi wako
Tigo hawapo huko. Zantel pekee ndio wamejaa KataviHivi Tigo wana ofisi wapi huku Katavi?
Tufundishe wewe basi hiyo marketingAnaropoka tu huyo marketing ataijulia wapi?
Karibu na nyumbani kwa mkuu wa Wilaya mtaa wa LihapiHivi Tigo wana ofisi wapi huku Katavi?
Usiwe unachukulia mambo seriously sana. Mbona machinga wanaendesha biashara bila kusomea marketing?Anaropoka tu huyo marketing ataijulia wapi?
Karne hii ya leo unawaza vazi la kitaifa? Ili iweje? Watu tunahitaji maendeleo hatuhitaji mavazi ya kitaifa ili hali matumbo ya njaa, kila utamaduni umeachwa ukisema hauna maana, leo hii nyumba unayoishi unaishi na kinyesi humo humo ukiita self contained, watoto wako au wadogo zako wanasoma shule kwa lugha ya kiingereza si ungewafundisha lugha ya kabila yako tukuone wewe kweli unajali utaifa wako.Mambo vp jamiiforums.
Ninashauri sana nchi yetu ya Tanzania isiwe na vazi moja tu la taifa. Tuwe na mavazi rasmi matano (5) kutoka katika makabila yetu yatakayorasimishwa na kupewa hadhi ya utaifa. Yaaani kama inawezekana mpangilio uwe hivi au hata kama kura ya maoni inaweza kupigwa itakuwa sawa tu.
Picha hapo chini ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne mzee Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwa wamependeza vizuri kabisa katika mavazi ya kabila ya Waha (baba) pamoja na Maasai (Mama)
View attachment 1718602
(1) Kaskazini - Vazi la kimaasai (Mkoa Arusha)
(2) Kusini - Vazi la Kimakonde (Mkoa Mtwara)
(3) Mashariki - Vazi la Kisambaa (Mkoa Tanga)
(4) Magharibi - Vazi la Waha (Mkoa Kigoma)
(5) Kanda ya kati - Vazi la wagogo (Mkoa Dodoma)
Nchini Afrika ya kusini wamefanya hili kwa upande wa lugha rasmi za taifa, ila sisi tunaweza kufanya hivi hivi kwa upande wa vazi rasmi la taifa.
Kwa uhalisia tu ni kwamba, huko nchini Afrika ya Kusini kuna makabila mengi sana yaliyopo katika majimbo tofauti tofauti na matokeo yake lugha zinatawala katika majimbo yao husika ambayo inafanya kuwa lugha mahususi haswa kwa eneo/mkoa husika.
Takribani lugha thelathini na tano (35) zenye asili ya Afrika Kusini huzungumzwa katika nchi hiyo, kumi kati ya hizo ni lugha rasmi za taifa la Afrika Kusini: Ndebele, Pedi, Sotho, Swati, Tsonga, Tswana, Venda, Xhosa, Zulu na Afrikaans.
Lugha rasmi ya kumi na moja ni Kiingereza, ambayo ndiyo lugha ya msingi inayotumiwa katika mazungumzo ya kibunge na kiserikali, ingawa lugha zote rasmi zina uzito sawa katika hadhi ya kisheria na katika ya nchi hiyo.
Kama katika lugha 35 kutoka nchi nzima waliweza kuchagua lugha 11 tu kutambulika kama "official languages" na Tanzania yenye makabila takribani 120 pia inaweza kuchagua mavazi kutoka makabila 5 tu kuwa ndio mavazi rasmi ya taifa ili tumalizane na hili suala kwa maana tangia lianze kujadiliwa ni zaidi ya miaka 15 sasa na bado sijaona solution ya maana mpaka sasa.
Zamani ilikuwa ni Dar es Salaam kwa kabila la wazaramo ila sasa ni Dodoma kwa wagogo ndipo kumepewa hadhi ya makao makuu ya nchi na serikali. Kama mkoa wa Dodoma umeweza kupewa hadhi hiyo na kuacha mikoa mingine, kwanini makabila matano niliyoyaorodhesha hapo juu yasiwakilishe mavazi rasmi ya taifa?
Soma pia>>> Kwanini mitaa ambamo kuna Balozi za nchi tano zenye nguvu duniani isiitwe majina ya vivutio vya utalii vya Tanzania?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kama hautaki vazi la taifa huyo ni wewe na usilazimishe watu wafananeKarne hii ya leo unawaza vazi la kitaifa? Ili iweje? Watu tunahitaji maendeleo hatuhitaji mavazi ya kitaifa
Kwani ni nani amekuforce ufanane na mwingine?hakuna namna utaforce watu wafanane.
Usifananishe biashara za bei ndogo na zile za mitaji ya mamilioni ya pesaUsiwe unachukulia mambo seriously sana. Mbona machinga wanaendesha biashara bila kusomea marketing?
Jiulize kwanza ikiwa haukutaji watu wa kufanana na wewe kwa nini usishone la kwako ukavaa?Kwani ni nani amekuforce ufanane na mwingine?
Nimekulazimisha WEWE ufanane na mimi?Jiulize kwanza ikiwa haukutaji watu wa kufanana na wewe kwa nini usishone la kwako ukavaa?
Ila kumbuka nchi ya South Africa imefanikiwa katika kurasimisha lughaNi ngumu kwa tanzania kutambulika kwa vazi rasmi la Asili sababu ya diversity ya mila na tamaduni zetu..makabila yetu mengi asili zao ni za kihamiaji
Hii nimeipenda sana mkuu. Asante kwa kunipa somo zuri.Nchi ambazo wanatambulika kwa mavazi yao ya Asili utakuta makabila yao machache yameingiliana had lugha yanafana
mfano Burundi na Rwanda watutsi na wahutu ni makabila yanayofautiana kdg kidesturi ila ila
lugha moja tamaduni kias kikubwa zinafanana hadi mavazi.. ndo maana ni rahis kurasimisha
same kwa ethiopia. wanaijeria na wengine hadi west africa.. angalia mavaz ya kiwest africa.. mtu wa senegal, Cameroon .. ghana. na kwingine mavaz yanafanana maana nao wameingiliana makabila. yako machache lakini yameingiliana
Wakihisi ndio tunawapa ufafanuzi kuwa hili ni vazi la Tanzania.usishangae ukivaa kama mgogo watu wa west africa au ulaya wakahisi umevaa kama watu wa wa Namibia na zimbabwe
Kwanini lubega na mavazi ya kimasai yatambulike kuwa ni ya nchi zingine na sio Tanzania? Kwani ni nani amekwambia dunia nzima wanajua wamasai wapo Kenya pekee?ukivaaa kama lubega ya shuka jeupe kama wahaya aidha upelekwe Rwanda , au uganda
kimasai.. tumeingiliana na Kenya so huwezi kuliita vazi asili la tanzania
sie tamaduni na desturi tunashea na watu wa nchi zingine .. so hatuwez tambulika kwa vazi maana makabila yetu kiasili ni wahamiaji tu hapa
Jiulize kwanza ikiwa haukutaji watu wa kufanana na wewe kwa nini usishone la kwako ukavaa?Kwani ni nani amekuforce ufanane na mwingine?
Kwa hiyo umetoka kwenye vazi umeenda kwenye lugha, na mbona tanzania imerasimisha kiswahili unahitaji lugha gani? ni kijiji gani Tanzania utaenda uongee kiswahili watu washindwe kukuelewa?Ila kumbuka nchi ya South Africa imefanikiwa katika kurasimisha lugha
Wakihisi ndio tunawapa ufafanuzi kuwa hili ni vazi la Tanzania.
Alafu kwanini wahisi umevaa kama Namibia? Kwanini akivaa mtu wa Namibia wasihisi amevaa kama mtanzania?