Tanzania isiwe na vazi moja tu la Taifa, tuwe na mavazi rasmi matano kutoka katika makabila yetu

Tanzania isiwe na vazi moja tu la Taifa, tuwe na mavazi rasmi matano kutoka katika makabila yetu

Vazi linapaswa li emerge kutokana na tamaduni za watu husika siyo watu kubebeshwa mavazi wasiyoyajua.
Mbona Dodoma hawapajui lakini wanapaita makao makuu ya nchi? Watanzania wote ni ndugu kumbuka hilo. Mbona Mzee Kikwete na Mama Salma wanavaa mavazi ya makabila mengine na wako poa tu? Hao wazee wasivae kwani wao ni akina nani?
 
Najaribu kuwaza uwaambie wazee wa kichaga (na walivyo jeuri) wakavae mashuka ya kimasai yanayowafanya watembee makalio yakiwa wazi, hili haliwezekani.
Mbona mzee Ole Sendeka anavaa sana nguo za kimasai na hayo maumbile yake hayabaki wazi? Matatizo ya watu kadhaa ndani ya jamii hayapaswi kutumika katika kutoa hukumu kwa jamii nzima (wamaasai)
 
Tufafanulie wewe basi mzee baba
 
Taifa hili lina mambo mengi sana ya kuweka sawa badala ya kupoteza muda kwenye petty issues(tuvitu tudogo tudogo tusitokuwa na manufaa yoyote ya maana)
Mkuu, kama vazi la taifa ni ushamba kwa maoni yako sawa ila kwa maoni yangu mimi na wengine huo sio ushamba hata kidogo.
 
Nikiabfali picha za Mwalimu na Kawawa naona kuna mtindo walikuwa wakitumia kama aina fulani ya shuka, mtindo ule unatokana na kabila gani hapa Tanzania ?
 
Suti zinatupendeza sana watanzania, tuache mawazo ya kupuyanga na kupoteza muda.
Mbona Dodoma hawapajui lakini wanapaita makao makuu ya nchi? Watanzania wote ni ndugu kumbuka hilo. Mbona Mzee Kikwete na Mama Salma wanavaa mavazi ya makabila mengine na wako poa tu? Hao wazee wasivae kwani wao ni akina nani?
 
Mbona mzee Ole Sendeka anavaa sana nguo za kimasai na hayo maumbile yake hayabaki wazi? Matatizo ya watu kadhaa ndani ya jamii hayapaswi kutumika katika kutoa hukumu kwa jamii nzima (wamaasai)
Labda hujui vizuri nguo za Kimasai, Ole Sendeka huwa hapigi full, huwa anavaa suti zake na juu anaweka shuka moja. Vazi la Kimasai ni full mashuka na yana style yake ya ufungaji. Sasa niambie ni lini ulimwona Ole Sendeka kapiga full shuka.
 
Waliopeleka makao makuu Dodoma kwa wagogo walifanya utafiti gani?
Sioni ni namna gani inahusiana na mada husika, Makao Makuu hayakuwekwa Dodoma simply kwa sababu ya Wagogo bali kutokana na geographical position hasa hasa kutokana na sababu za kiusalama tu. Hili huwa linafundishwa hata shule za msingi, kwa nini Dodoma ikawa Makao Makuu.
 
Mbona Dodoma hawapajui lakini wanapaita makao makuu ya nchi? Watanzania wote ni ndugu kumbuka hilo. Mbona Mzee Kikwete na Mama Salma wanavaa mavazi ya makabila mengine na wako poa tu? Hao wazee wasivae kwani wao ni akina nani?
Unachanganya vitu vingi sana, eneo kuwa makao makuu huwa na sababu tofauti na zile za vazi la taifa. Eneo linaweza kuwa makao makuu kutikana na sababu za kiusalama, sababu za kijiographia, historia ya eneo husika etc. hili haliegemei kivile katika tamaduni za watu husika.
Ila vazi la taifa, lazima litokane na tamaduni za watu husika.JK alikuwa anavaa vile kama kiongozi wa nchi, ili kuonyesha mshikano na kabila husika, ikumbukwe hii hutokea wakati wa ziara za mikoani.
Labda nikuulize, baada ya JK kumaliza uongozi wake, ni lini tena umemwona kapiga mavazi ya hivyo?
 
Unachanganya vitu vingi sana, eneo kuwa makao makuu huwa na sababu tofauti na zile za vazi la taifa. Eneo linaweza kuwa makao makuu kutikana na sababu za kiusalama, sababu za kijiographia, historia ya eneo husika
Hayo mavazi ma-5 pia yanaweza kuwa ya kitaifa kwa sababu ya kujenga mshikamano na umoja wa kikabila...
 
Back
Top Bottom