Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.

Vita kamili inanukia Kati ya Ethiopia na Misri kupigana kwaajili ya matuzi ya maji ya mto Nile, hasa baada ya Ethiopia kujenga bwawa (Gerd) kubwa la kufua umeme kwa kutoa maji ya mto Nile kujaza bwawa hilo litakalotumia mabilion ya ujazo ya maji ya Nile.

Misri kwa upande wake inahofia kuwa ujazo wa maji ya mto Nile yatakayofika Misri utapungua hivyo kuathiri maisha na uchumi wa Misri.

Kwenye ugomvi huu Ni vema Tanzania ikaunga mkono upande upi na kwasababu gani?
 
Endapo ikitokea vita basi hata Misri na Ethiopia watapigana pasipo sababu za msingi, na Tanzania katika vita hiyo inabidi iwachape wote.

Vyanzo vya mto Nile ni mkanganyiko mkubwa na watu wanachukulia kwa wepesi.

White Nile, inawezekana* chanzo chake ni Rwanda/Burundi, Mto Kagera au Ziwa Nyanza (Victoria).

Blue Nile kwa hakika chanzo ni Ziwa Tana, Ethiopia.

Great Nile the mixer of White and Blue Nile inaanzia Khartoum, Jamhuri ya Sudan baada ya White x Blue Nile kuungana na kuendelea Ardan, Cairo hadi Alexandria.

Sasa sijaelewa wanaenda kupigana sababu ya Greater Nile, White Nile au Blue Nile?

Kama wanapigana sababu ya Greater Nile basi Tanzania awaadhibu wote kwa kushirikiana na Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Sudan. Endapo chanzo cha mapigano ni Blue Nile basi Ethiopia ana haki ya kumpiga Misri na kwa White Nile bado Tanzania ana haki ya kuwachapa wote.
 
Misri bhana wapuuzi kweli eti wana mkataba Tanzania tusitumie yale maji nilimkubali sana Lowasa kulisimamia lile mpaka maji kuanza kutumika ukanda wa kaskazini huko. Ilikua ajabu sana maji mengi ila hawaruhusiwi kutatumia Kama ilivyo sasa. Misri alibebwa na wakoroni hapo mwenye haki ni Ethiopia maji yanapita kwake ayatumie.
 
Misri bhana wapuuzi kweli eti wana mkataba Tanzania tusitumie yale maji nilimkubali sana Lowasa kulisimamia lile mpaka maji kuanza kutumika ukanda wa kaskazini huko...ilikua ajabu sana maji mengi ila hawaruhusiwi kutatumia Kama ilivyo sasa....Misri alibebwa na wakoroni hapo mwenye haki ni Ethiopia maji yanapita kwake ayatumie.....
Tuwe waangalifu tunapoikataa mikataba iliyowekwa na wakoloni wakati ukoloni. Mkataba uliowapa Misri haki ya kwanza kwenye utumiaji wa maji ya mto Nile uliwekwa wakati wa ukoloni na wakoloni kwa manufaa ya wakoloni, sawa na mipaka ya nchi zetu iliyoko Sasa.

Je, nchi zetu ziko tayari kuachana na mipaka ya wakoloni ili tuligawe upya Bara la Africa? Iko nchi itakubali kuwa mipaka ya wakoloni haifai tuanze upya. Hata Misri kwenye hili inawezekana kuwa Ina hoja
 
Hahah Magu alisemaga acha majirani wachapane tuwauzie chakula.
Hiyo itawezekana kama tutakumbatia Kilimo cha matrekta, kumwagilia na uongezaji thamani ya mazao ya kilimo kwa miaka 5 ijayo badala ya kujenga kujenga kujenga. Ni muda wa kuchimba mabwawa ya umwagiliaji na kununua meli kubwa za uvuvi tuvue ili tuwauzie unga na mboga wanaopigana.
 
Wachapane tu sisi tuwauzie korosho, choroko kama ikiwezekana tutumie namna wachapane, wengine tukamate totoz za huko juu kama wakimbizi
Haha, si watakimbia pamoja na wanaume wao?
 
Acha kufananisha mipaka na maji ni upuuzi ulio tukuka yaani mto upite kwako usitumie maji eti kisa hayo maji yanaenda kwa jirani yako uwo si ujinga uwo maji tutatumia wote kama utaki nitumie yapitishe angani bac na sio kwenye ardhi yangu ...
 
Tz tutakuwa kama kawaida yetu unafiki (NAM) ila in deep tutakuwa upande wa Misri kwa sababu bwala la Ethiopia ni mshindani wa bwawa letu so sisi hapa tutaombea Ethiopia ashindwe ili tuwe wauzaji wakubwa wa umeme ukanda huu

kingine ambacho hakisemwi ni kuwa misri wametupa offer nyingi mno kwenye ujenzi wa bwawa letu ili tuwe upande wao
 
Sisi ni wazee wa kujiramba na kula Pop Corn kwenye hilo movie tukiwa tumeweka hela zetu za vyakula kibindoni
 
Tanzania iwe upande wa Ethiopia hiyo mikataba aliikataa Nyerere baada ya kupata uhuru kila nchi inabidi kupata maendeleo kwa rasilimali ilizonazo hao Misri waliwahi kufunga mfereji wa Suez Canal walipogombana na Israel
 
Hakika Mkuu,

Tukitazama kwa uhalisia endapo Ethiopia amejenga bwawa kutoka katika Ziwa Tana (Blue Nile) katika mipaka yake basi ni haki yake maana chanzo hicho kinatoka kwake kuelekea Khartoum.
Ni kweli mkuu kwa maoni yangu ninaona kinacho ipa Misiri kiburi ni kwa sababu ya Udhaifu wa wale inao zozana nao, Misri siku zote imekuwa ikionesha kiburi kwenye meza ya mazunguzo

Kiuhalisia sioni kama Ethiopia ina nguvu za kukabiliana na Misri hata kidogo hasa kijeshi hilo liko wazi.
Kingine Misri ina huungaji mkono mkubwa kutoka kwa nchi za Magharibi

Kingine nchi nyingi za kiafirika zinaongozwa na viongozi wanafiki vita ikianza hakuna msaada wowote watakao utoa kwa Ethiopia itapigwa wanaangalia tu
 
Back
Top Bottom