Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Hao Egypt "waliudindia" hata mradi mkubwa wa Tz wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria Shy-Tabora-Singida-Dodoma.

Kwa hiyo hao maustadhi ni adui wa kila mwenye interest na maji ya Nile.

Hizi serikali zinatumia pesa kuhakikisha misitu na vyanzo vingine vinavyoleta maji kwenye vyanzo vya Nile haviharibiwi halafu hao jamaa mkitaka kuyatumia wanaibuka na mkataba wa 1919 wa mkoloni.

Upande wetu unajulikana,hata tusiposhiriki.
 
Naungana na Misri kwa kuwa hawana chanzo kingine cha maji zaidi ya Nile. Wewe ungekuwa rais wa Misri ungekubali kuona watu wanakufa njaa kwa kukosa maji ya kutumia na kumwagilia mashambani?

Tatizo Ethiopia anataka ajaze maji kwa mkupuo na abadilishe mkondo wa maji. Misri anaomba mkondo wa maji usibadilike na muda wa kujaza bwawa uwe miaka kadhaa, sio mkupuo.
 
Tutakuwa wasuluhishi wa vita hiyo kwani Tanzania ni kisiwa cha amani. Hamna haja ya kuchochea mapigano kwa ishu ya maji, ni swala la kukaa chini na kuongea. Hivi mnajua athari za vita? Kama wakianza vita, mabeberu huwa wanapitia humo humo kuchochea vita na kuiba rasilimali za nchi husika
 
Ni kweli mkuu kwa maoni yangu ninaona kinacho ipa Misiri kiburi ni kwa sababu ya Udhaifu wa wale inao zozana nao, Misri siku zote imekuwa ikionesha kiburi kwenye meza ya mazunguzo.
Kiuhalisia sioni kama Ethiopia ina nguvu za kukabiliana na Misri hata kidogo hasa kijeshi hilo liko wazi.
Kingine Misri ina huungaji mkono mkubwa kutoka kwa nchi za magharibi.
Kingine nchi nyingi za kiafirika zinaongozwa na viongozi wanafiki vita ikianza hakuna msaada wowote watakao utoa kwa Ethiopia itapigwa wanaangalia tu.
Hakika Mkuu,

Ikifika wakati wa vita, haitokuwa vita ya Ethiopia na Misri, maana baada ya Ethiopia endapo Jamhuri ya Sudan ikihitaji kujenga Khartoum itazuiliwa, Sudan Kusini kujenga Juba itazuiliwa, Uganda kujenga Jinja itazuiliwa na Tanzania kuendeleza maeneo ya Ziwa Nyanza (Victoria) itazuiliwa.

Misri adhibitiwe mapema, lah sivyo atandelea na mchezo huu kwa yeyote mwenye kuhitaji kufanya maendeleo kutumia Nile.
 
Naungana na Misri kwa kuwa hawana chanzo kingine cha maji zaidi ya Nile. Wewe ungekuwa rais wa Misri ungekubali kuona watu wanakufa njaa kwa kukosa maji ya kutumia na kumwagilia mashambani?

Tatizo Ethiopia anataka ajaze maji kwa mkupuo na abadilishe mkondo wa maji. Misri anaomba mkondo wa maji usibadilike na muda wa kujaza bwawa uwe miaka kadhaa, sio mkupuo.
Mkuu,

Misri ana eneo Mediterranean Sea anaweza kuvuta maji kutokea Port Said, Alexandria na Marsa Matruh.

Misri ana eneo Red Sea anaweza kuvuta maji kutokea Sham el Sheikh, Suez, Ismailia na Hurghada.
 
Egypt ni Wabinafsi, kama kawaida ya Mwarabu....
Ukisema hivyo unakosea mkuu, sheria za kidunia haziruhusu kufanya chochote kwenye chanzo cha maji kumbuka Mbowe mashamba yake yariharibiwa kisa kuwa karibu na chanzo cha maji sasa Misri wanatumia sheria hiyohiyo iliyotumika kumuharibia Mbowe mashamba, ingawa mimi sioungi mkono hii sheria maana haiwezekani ziwa lote lile turuhusiwe kuvua samaki tu bila kunywa yale maji
 
Acha kufananisha mipaka na maji ni upuuzi ulip tukuka yani mto upite kwako usitumie maji eti kisa hayo maji yanaenda kwa jirani yako uwo si ujinga uwo maji tutatumia wote kama utaki nitumie yapitishe angani bac na sio kwenye ardhi yangu...
Na mbaya zaidi Ethiopia ndio wanaotunza misitu ya chanzo Cha Nile isikatwe. Vita hiyo itakuwa mbaya Sana kuwahi kutokea.

Mkuu hata mipaka ziko nchi ambazo zinakerwa Sana na mipaka hiyo, mfano huwezi kuwa na nchi ndogo Kama Rwanda na Burundi huku kukiwa na nchi kubwa Kama DRC Congo, Tanzania na Uganda pembeni yako. Unaambiwa kwa mujibu wa mipaka ya mkoloni hata Dar es Salaam na Morogoro Ni sehemu ya Zanzibar. Kama Kuna uwezekano nchi kuipinga sheria za mkoloni Basi ziko tayari pia kuipinga mipaka yao. Dialogue itawale kwenye hili
 
Tz tutakuwa kama kawaida yetu unafki(NAM) ila in deep tutakuwa upande wa misri kwa sababu bwala la Ethiopia ni mshindani wa bwawa letu so sisi hapa tutaombea Ethiopia ashindwe ili tuwe wauzaji wakubwa wa umeme ukanda huu

kingine ambacho hakisemwi ni kuwa misri wametupa offer nyingi mno kwenye ujenzi wa bwawa letu ili tuwe upande wao
Naanza kuelewaa...
 
Mkuu,

Misri ana eneo Mediterranean Sea anaweza kuvuta maji kutokea Port Said, Alexandria na Marsa Matruh.

Misri ana eneo Red Sea anaweza kuvuta maji kutokea Sham el Sheikh, Suez, Ismailia na Hurghada.
Hayo ni maji ya chumvi. Gharama za kuyatreat na teknolojia yake ngumu wanayotumia Israel haipatikani Misri. Hata hivyo mkataba wa mabeberu uliwapa haki hiyo, kama hawatokubaliana mezani lolote litatokea. Wiki hii kuna delegation ya Misri ilikuwa Somaliland wakizungumza possible military base, Somaliland na Ethiopia wanapakana.
 
Hakika Mkuu,

Tukitazama kwa uhalisia endapo Ethiopia amejenga bwawa kutoka katika Ziwa Tana (Blue Nile) katika mipaka yake basi ni haki yake maana chanzo hicho kinatoka kwake kuelekea Khartoum.
Sawa kabisa, Ethipia hajachota maji toka nile kuu ambayo inaanzia Khartoum kuelekea Misri. Ethiopia ana haki zote na hata akipigwa kijeshi leo madai yataendelea kuwepo. Tukikumbuka ya Lowassa, ni sawa basi tumuunge mkono Ethiopia, Angalia ramani hii,
1596188845245.png
1596188845245.png
 
Kwa Wamisri maji ya mto Nile ndio roho yao pekee. Hawana mbadala, Ni ama wafe wote au wapone wote kutetea maji hayo
Na ndio maana nimeionya Ethiopia isije jitoa ufahamu wa kukabiliana kijeshi na Misri kwa sababu hana jeshi la kupigana na Misri ataharibiwa vibaya sana, nadhani waongee waelewane.
 
Maji yangu unipangie jinsi ya kuyatumia.

Misri wapumbavu sana.

Kama wanashida ya maji wageuze bahari chanzo chao cha maji.

Waache Waethiopia wafanye watakacho. Mto Nile ni baraka ya Mungu. Hatuna mwenye mamlaka na huo mto.
 
Hakika Mkuu,

Ikifika wakati wa vita, haitokuwa vita ya Ethiopia na Misri, maana baada ya Ethiopia endapo Jamhuri ya Sudan ikihitaji kujenga Khartoum itazuiliwa, Sudan Kusini kujenga Juba itazuiliwa, Uganda kujenga Jinja itazuiliwa na Tanzania kuendeleza maeneo ya Ziwa Nyanza (Victoria) itazuiliwa.

Misri adhibitiwe mapema, lah sivyo atandelea na mchezo huu kwa yeyote mwenye kuhitaji kufanya maendeleo kutumia Nile.
Tatizo wanao takiwa kuidhibiti Misri ndio hao hao walio saini mkataba huo unao ipa haki Misri kuidhibiti huu mto ,nikimaanisha ni nchi za magharibi zenye uwezo wa kuidhibiti Misri

Hakuna nchi ya kiafrika yenye ubavu wa kuidhibiti Misri.
 
Na ndio maana nimeionya Ethiopia isije jitoa ufahamu wa kukabiliana kijeshi na Misri kwa sababu hana jeshi la kupigana na Misri ataharibiwa vibaya sana, nadhani waongee waelewane.
Vita huwa inamatokeo ya kushangaza sio kama misri atajaribu kufanya ujinga wa kuishambulia kijeshi Ethiopia

tusiwabeze Ethiopia ni taifa kongwe na wana historia nzuri saana kijeshi sasa sioni kama misri anaweza kuipiga na kufikia malengo kwa kutumi kuweka military base Somaliland dhidi ya Ethiopia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo ni maji ya chumvi. Gharama za kuyatreat na teknolojia yake ngumu wanayotumia Israel haipatikani Misri. Hata hivyo mkataba wa mabeberu uliwapa haki hiyo, kama hawatokubaliana mezani lolote litatokea. Wiki hii kuna delegation ya Misri ilikuwa Somaliland wakizungumza possible military base, Somaliland na Ethiopia wanapakana.
Mkuu, Misri anafanya ukorofi tu mwenyewe katika mipaka yake kupitia Ziwa Nasser lililotengenezwa kutokana na Mto Nile amejenga bwawa la Aswan, mjini Aswan.

Jamhuri ya Sudan kupitia Port Sudan mji wa mashariki wanachukua maji Red Sea.

Eritrea kupitia Massawa anachukua maji Red Sea, Saudia kupitia Jedda, Mecca na Al Taif anachukua Red Sea.

Libya kupitia Tripoli, Benghazi, Al Bayda, Darnah, Surt na Al Khums anatumia maji ya Mediterranean Sea hivyo hivyo kwa Tunisia kupitia Tunis.

Kisiwa cha Crete - Uyunani, Limassol na Nicosia - Cyprus, Catania, Sicily - Italia wanatumia maji ya Mediterranean Sea.

Misri anapowekeza kwenye jeshi akumbuke anaweza kuwekeza ku-treat maji ya chumvi. Hata Dar es Salaam anatumia maji ya Bahari ya Hindi yenye chumvi.
 
Hayo ni maji ya chumvi. Gharama za kuyatreat na teknolojia yake ngumu wanayotumia Israel haipatikani Misri. Hata hivyo mkataba wa mabeberu uliwapa haki hiyo, kama hawatokubaliana mezani lolote litatokea. Wiki hii kuna delegation ya Misri ilikuwa Somaliland wakizungumza possible military base, Somaliland na Ethiopia wanapakana.
Kwamba kuna tech anaweza kui afford Israel Egypt ikamshinda? Miaka ya 70 Mexico (kama sikosei) walijenga plant ya kubadili maji bahari kuwa maji baridi hapa Tanzania kwa ombi la Nyerere halafu leo Egypt ashindwe ku-afford gharama za hiyo teknolojia!

Sidhani labda wana sababu zingine za kwanini hawafanyi ila haiwezi kuwa gharama
 
Back
Top Bottom