Hili wazo la kuungana Tanzania, Kenya na Uganda si baya, lakini tukifanya kwa pupa, linaweza kutuumiza sisi Watanzania.
Mfano wa haraka kabisa: siku sheria ya muungano itapitishwa, bei ya viwanja Dar es Salaam inaweza kupanda mara mbili au tatu. Wakenya na Waganda walio na mitaji mikubwa watanunua kwa kasi, sisi tukibaki tunaangalia au tunanunua kwa presha — bei inapanda zaidi.
Pia, ajira zitaingia kwenye ushindani mkali. Wakenya wana CV kali na wanajua kujitangaza, wanaweza kuchukua nafasi nyingi kabla ya sisi kuamka.
Vilevile, sheria za kodi, ardhi, mishahara na uraia ni tofauti. Tukichanganya pasipo mpango, tutajikuta tuna hasara kuliko faida.
Kwa kifupi: muungano uwe kwa akili, si kwa jazba.