Tanzania kinara katika udahili wa wanafunzi elimu ya awali barani Afrika

Mtanzania siku zote ni kiumbe wa ajabu sana nyeupe huita nyekundu,njano anaita nyeusi teh,teh,....
 
..tatizo letu tangu wakati wa Mwalimu Nyerere lilikuwa kuruhusu siasa ziingie ktk uendeshaji wa sekta ya elimu.

..walioharibu mitaala ni wanasiasa. Lakini mimi siamini kama walifanya hivyo kwa nia mahsusi ya kuua shule za serekali.

..makosa yaliyotokea yalisababishwa na watu wasio na uelewa wa masuala ya elimu kuwa na sauti zaidi ktk maamuzi yaliyokuwa yakifanyika ktk sekta hiyo.

Niliposema kuua shule za serikali sikumaanisha wakati wa Mwalimu.

Yeye alifanya kadri mazingira yalivyomruhusu, kumbuka kipindi kile walimu walikuwa wachache sana wakati 'fertility rate' kwa Tanzania ilikuwa watoto saba kwa mwanamke mmoja. Waingereza wanasema, "drastic times calls for drastic measures", hivyo ili kuongeza idadi ya wanaojua kusoma na kuandika (unaweza ita sababu ya kisiasa ila mimi naona ni mazingira tuu) akaleta elimu ya UPE.

Tatizo nililikua naliongelea ni lile la mwaka 1991 baada ya Azimio la Zanzibar ambapo watu waliachiwa kufanya mambo kiholela. Nia ilikuwa nzuri (drastic times calls for drastic measures) ila hatukujua waliotushinikiza walikuwa na lengo gani.

Wahusika waliotakiwa kusimamia elimu ndiyo walioanzisha mashule binafsi na kuhakikisha kwa namna moja ama nyingine mitaala inaharibika ili shule za serikali zife na zile binafsi zishamiri.

Nakumbuka mwaka 1993 wizara ya elimu ilikuja na jaribio la kubadilisha mitaala ya shule za sekondari. Eti lengo lilikuwa ni kujiandaa na karne ya 21.Walichokifanya ni kuunganisha masomo ya arts (jiografia, siasa na historia) kuwa somo moja lililoitwa "social studies". Yale ya sayansi (physics, biology na chemistry) kuwa somo moja waliloliita unified science.Mambo ya hovyo kabisa.

Wakachagua zile shule bora za O' level za serikali Dar es salaam (Azania, Jangwani na Forodhani) kuzifanyia majaribio, huku hata vitabu vya kufundishia hawana.

Bado tunasafari ndefu ila angalau tunaweza kuona mwanga huko mbeleni.
 
..katika kila awamu wanasiasa wamejaribu na wamefanikiwa kuvamia sekta ya elimu.

..na wakati wote wamekuwa wakitumia UDAHILI kama kichaka cha kuonyesha kuwa wanajali elimu ya mtoto wa kiTanzania.

NB.

..sasa hivi naona vijana wa JPM mmekuja na "fashion" ya kulaumu Azimio la Zanzibar kama ndiyo mzizi wa matatizo ya nchi hii.

..lakini mnasahau kwamba Azimio la Arusha ambalo mnadai lilikuwa zuri liliangusha uchumi wa Tanzania.

..Mazao ya mkonge na korosho ambayo yalikuwa yakitupatia fedha nyingi za kigeni yaliporomoka kutokana na utekelezaji wa Azimio la Arusha.

..Tuwe waangalifu kidogo na "maazimio."
 
Back
Top Bottom